JWTZ: Tunamsaka aliyesema tumeongezewa Mshahara

Wakipewa ushahidi watasema fabricated 🤣🤣🤣🤣
Probably kinachozungumziwa ni ration allowance na sio mshahara
 
Jwtz ni taasisi kubwa na inayo aminika, sioni sababu ya hii taasisi pendwa kujibu mambo ya mitandaoni maana wana majukumu mengi ya maana zaidi ya haya ya kubishana na raia

Vitu kama hivi Jwtz wawaachie wale wanao sema kuna uhaini wa kumuondoa Mh. Rais madarakani.
 
Tafadhali haina tija .....tunaomba mtafuteni alie draft mkataba mbovu vile anataka kuuza power ya Rais na nchi piaa .....mliapa kulinda katiba na nchi na rasilimali zake ........wanasiasa wanawachezea sharubu .....isije kuwa mnaongexewa kupoozwa....tunaliamini sana Jeshi tafadhali
 
Hii account ni ya Godbless lema wanaitumia na Maria sarungi na anayeiendesha yuko Japan uwa wanamtumia cha kupost hivo kumpata si rahisi Ila suala la kushangaza uzushi unakuwa mwingi! Ila jeshi ilibidi likanushe tu waendelee na shughuli zao maana nimeangalia kwa makin nikagundua jamaa hakutaja JWTz Ila Kasema jeshi, sijui Kama picha inamfunga maana katumia picha tu na kusema jeshi laongezewa salary

Britanicca
 
Na akipatikana yeye ndo atawaongezea mshahara
 
 
Kama ni habari ya kizushi hiyo ni kazi ya polisi, hivyo basi Jeshi liende likatoe taarifa polisi.

Kazi ya Jeshi ni kuzuia DP World wasitie mguu kwa sababu bandari ni mipaka na ni kazi ya jeshi kulinda mipaka. Lakini pia ule mkataba unavunja katiba na ni kazi ya jeshi kulinda katiba.

Kazi ya jeshi siyo kudeal na makosa ya uchochezi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…