Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona sioni hoja ya msingi ya kujadili hapa?
kwani wanasoma bure! labda muwe vitani ndio tungeweza kukataa...ni mafunzo ya Officer Cadet course ya mwaka mmoja inayotolewa Tanzania Military Academy, Monduli.
..zaidi ya askari toka CoW, nchi nyingine zilizofaidika na mafunzo toka kwa jeshi letu ni Seychelles, DRC, Mozambique, na Zimbabwe.
..habari hii inazima zile propaganda kwamba Tanzania ina mahusiano mabaya na majirani zake.
habari nzima soma hapa: Home
habari nyingine hii hapa:http://www.dailynews.co.tz/index.ph...congo-president-in-arusha-for-special-mission
cc lawmaina78, jMali, Ngongo, Nguruvi3, Bulldog, Kishimbe wa Kishimbe
Suala la maofisa wa kijeshi kwenda kujifunza mbinu za kivita kwenye nchi nyingine ni la kawaida hivyo siyo ajabu maafisa wa jeshi la Kenya kujifunza kwenye chuo cha maafisa wa kijeshi Tanzania kama ambavyo sio ajabu kwa maafisa wa JWTZ kujifunza kwenye chuo cha maafisa wa kijeshi cha Kenya. Hilo Linatokea kwa nchi nyingi na siyo kwa Kenya, Tanzania, Rwanda! na Uganda pekee.Hata mimi sioni hoja hisiyo ya msingi ya kutojadili hapa
Ukiona Alumni yeyote ta tanzania iko katika nchi ya kigeni, basi ujue kuna mission za udukuzi za ki-intel zinafanyaka.. tanzania has nothing to learn from anycountry in the field ya militarism.
kwani wanasoma bure! labda muwe vitani ndio tungeweza kukataa.
..ni jambo la kawaida lakini nani alikuwa anajua?
..nimeileta habari hii ile ku-balance habari mbaya zinazoandikwa dhidi ya Tz ktk magazeti ya wenzetu.
..kuna vyombo vya habari kama rwanda newtimes, the eastafrican magazine, na blog mbalimbali zimekuwa zikiwaaminisha wasomaji wao kwamba hakuna jema linaloweza kufanywa na Tanzania au Mtanzania.
..kwa mfano, kulikuwa na habari ya Tanzania kujitenga, na kutokuchangia chochote kile, ktk East Africa Standby Force. Sasa hailezwi kwamba Tanzania tayari tuko kwenye Souther African/SADC standby force, na zaidi imekuwa ikishirikiana ktk mafunzo na mazoezi ya pamoja na majeshi mbalimbali ya East Africa na Afrika kwa ujumla.
..lakini kitu cha ajabu, na ambacho sikukitegemea, ni reaction ya baadhi ya wachangiaji ambao ni ndugu zetu toka baadhi ya nchi majirani. michango yao inaonyesha kwamba wamekerwa sana na kitendo cha cadets wao kupata mafunzo toka kwa majeshi yetu.
cc mossad007, lawmaina78, waltham, Geza Ulole, Ab-Titchaz