JWTZ yaonya wanaovaa sare zake

JWTZ yaonya wanaovaa sare zake

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeonya juu ya matumizi ya sare na vifaa vingine vya majeshi kwa watu wasiohusika. Limetangaza kuwa hatua kali za kisheria, zitachukuliwa dhidi ya watu hao.

Limehadharisha juu ya uvaaji, uingizaji nguo nchini ikiwemo mitumba, kwamba kama itatokea, zinafanana kwa aina yoyote ile na ikadhaniwa ni za jeshi hilo, mtu anayehusika atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zinazohusu sare za majeshi zilizopo.

"Msisitizo uliwekwa hapa katika vifungu vya sheria ni kwamba sio lazima ukutwe na sare ambazo zinatumiwa na JWTZ. Hasha!. Hapa sheria inasema hata kama tu nguo hiyo itaelekea kufanana kwa namna yoyote ile na sare za JWTZ, ni kosa la kisheria kuitumia," ilisema taarifa ya Jeshi kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo ilitolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano, Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam, jana. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtu yeyote yule asiye na ruhusa ya kushona, kuuza au kuingiza nchini sare za jeshi, atakuwa ametenda kosa, hivyo atafikishwa mahakamani.

Tamko hilo la jeshi linasema kwa muda mrefu sasa katika miji mikubwa, hasa Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma na mikoa mingine, kumekuwa na ongezeko la matukio ya wizi na uhalifu wa kutumia silaha.

"Imeonekana kuwa wanaohusika na vitendo hivyo, baadhi yao huonekana wamevaa sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na zimekuwa zikitumika katika matukio yenye sura ile ile," ilisema.

Taarifa hiyo ilisema, "Hivi karibuni vichwa vya habari vimetawala sana kwenye vyombo mbalimbali vya habari sehemu mbalimbali hapa nchini, mara utasikia ‘Mwanajeshi feki mbaroni Tanga' au Aliyejifanya Ofisa wa JWTZ akamatwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na mengine mengi."

Ilisema pia kumejitokeza mtindo wa baadhi ya wasanii hasa wanamuziki wa kufokafoka maarufu bongo fleva, kurekodi video zao wakiwa wamevaa sare za jeshi, kama vile suruali, viatu, fulana, kaptula, mabegi au kofia.

Kulingana na taarifa hiyo, mitaani nako kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi, hasa vijana, wanaovaa sare za jeshi, ambao wakiulizwa wanakozitoa, hudai wamenunua kwenye mitumba au kwenye maduka ya nguo.

"Ukipita kwa wauza mitumba nao utakuta wanauza nguo za jeshi, ingawa wao hufanya biashara hiyo kwa kificho, kwani huziweka sare hizo kwa nyuma ndani kwenye maghala yao na kuziuza kwa kificho na usiri mkubwa kwani wanafahamu kuwa ni kinyume cha sheria ya nchi kuuza sare hizo, ingawa wapo baadhi yao ambao huziuza hadharani wakidai kuwa ni mitumba," ilisema.

Taarifa hiyo ilisema inawezekana kuwa kwa namna moja ama nyingine, baadhi ya watumiaji wa sare hizo, hawafahamu kuwa ni kinyume cha sheria ya nchi, kukutwa na sare yoyote ile ya kijeshi, lakini kutokujua sheria, siyo utetezi mbele ya mahakama.


Chanzo: Habari leo
 
Hili neno linanichanganya sana 'kutokujua sheria siyo utetezi mbele ya mahakama' msaada pliz
 
Hili neno linanichanganya sana 'kutokujua sheria siyo utetezi mbele ya mahakama' msaada pliz
Tutaamini vipi kwamba we ulikuw hujui.., mfano najua kabisa kwamba kuiba ni kosa ila nikaamua kuiba.., then mkinikamata nasema nilikuwa sijui kwamba ni kosa.., besides hata kama hulikuwa hujui bado madhara ya kuvunja sheria yako palepale hivyo adhabu lazima ifuate.., its quite logical actually..
 
Kuvaa mfananio na jeshi huwahamasisha vijana kupenda jeshi toka utotoni. Marekani ni ruksa kuvaa toka umri mdogo ndio maana huchangamkia kujiunga na jeshi wakati wa vita.

Wasanii wa marekani mfano Rihanna ni ruks kuvaa vya jeshi, wacheza sinema wa Hollywood nao ni ruksa. Si mmeona picha za akina Shwazznegaer . Hawa huruhusiwa kutumia mpaka ndege za Kivita (Top Gun) na vifaru. Wasani hukuza uchumkhiv


 
Na wanaoweka kwenye siti za magari, akikamatwa kwa kosa la barabarani basi hushusha kioo na jamaa wale wakiona kombati baaaas!!!
 
Kama kuna mambo yananikera; hakuna kama haya mawili, la kwanza ni watu kung'ang'ania kuvaa sare zinazofanana na JWTZ, na lingine ni baadhi ya maaskari kuzurura mitaani na sare mchanganyiko; haswa ni suruali za kijeshi kuchanganya na shati au fulana za mitaani na kingine ni baadhi ya polisi wetu kutembea barabarani bila ya kuvaa kofia na baadhi wakivuta sigara!
Ndiyo maana naunga mkono kikamilifu tamko hilo la JWTZ na ningefurahi kama hatua hizi zingewahusu pia maaskari wasiozingatia nidhamu za uvaaji kijeshi.
 
"Msisitizo uliwekwa hapa katika vifungu vya sheria ni kwamba sio lazima ukutwe na sare ambazo zinatumiwa na JWTZ. Hasha!. Hapa sheria inasema hata kama tu nguo hiyo itaelekea kufanana kwa namna yoyote ile na sare za JWTZ, ni kosa la kisheria kuitumia," ilisema taarifa ya Jeshi kwa vyombo vya habari.

575686_171810116354558_542460542_n.jpg
 
Kuvaa mfananio na jeshi huwahamasisha vijana kupenda jeshi toka utotoni. Marekani ni ruksa kuvaa toka umri mdogo ndio maana huchangamkia kujiunga na jeshi wakati wa vita.

Wasanii wa marekani mfano Rihanna ni ruks kuvaa vya jeshi, wacheza sinema wa Hollywood nao ni ruksa. Si mmeona picha za akina Shwazznegaer . Hawa huruhusiwa kutumia mpaka ndege za Kivita (Top Gun) na vifaru. Wasani hukuza uchumkhiv



Lakini hoku hazitumii ktk kuibia watu, kufanyia ujambazi, na sio kila kinachofanyika Marekani na ulaya kinafaa kukifuata.
 
Back
Top Bottom