JWTZ yaonya wanaovaa sare zake

JWTZ yaonya wanaovaa sare zake

Hahahahhahhahah! Kwani hujui kuwa nusu ya daladala ni za hao!
Inakera mkuu, mtu analipwa mshahara mara mbili kwa mwezi (nasikia). MAhitaji yote maishani ananunua kwa bei iliyopunguzwa, hadi pombe halafu anashindwa kulipa mia nne ya nauli.

Ubabe unaenda hadi wakiwa na nguo za raia wanataka wasilipe nauli... Wanakera sana kaka.
 
Tatizo la wanajeshi wengi ni shule, misuli mingiii ubongo kisoda.

Hakyanani we hamnazo, nitajie chuo chochote cha elimu ya juu ambacho hakina wanajeshi wanaosoma hapo. They are everywhere!
 
mimi siwezi kuacha kuvaa pensi langu..ila mkinikamata mnipeleke mahakamani sio kambini kwenu
 
Inahitajika elimu kwa wananchi kuhusu sheria ya mavazi ya majeshi ili hata ikitokea mtu kakiuka basi hata raia walioko mtaani watasaidia kumkamata na kumfikisha mahala husika.

Kwa upande mwingine nafikiri kuna tatizo hata kwenye majeshi yetu yaani JWTZ, Polisi na Magereza. Utakuta vifaa vya jeshi yakiwemo mavazi vinawafikia raia wa kawaida kupitia hao hao askari. Mfano buti, kombati na hata bunduki na hatimaye kukamatwa ktk matukio mbalimbali ya kihalifu.
 
Hakyanani we hamnazo, nitajie chuo chochote cha elimu ya juu ambacho hakina wanajeshi wanaosoma hapo. They are everywhere!

Unaongelea wanaoshinda wanafyeka majani pale Lugalo?? Jamaa kasema kweli...wanajeshi wengi wanatumia nguvu tu kufikiri kwa kina ni sufuri...
 
Mbona sare za shule hamvai?

kwani hakuna shule nzuri hapa TANZANIA?

VAENI SARE ZA FEZA, ILBORU, TABORA SCHOOLS, NGANZA, SHULE YA MSINGI JANJA JANJA NA T-SHIRTS ZA VYUO VYETU KAMA MLIMANI NA UDOM...

JAMANI JESHI NI SECTOR NYETI... IACHENI KAMA ILIVYO..!
 
umeisahau Igowole ndiyo inaongoza.
 
Mbona sare za shule hamvai?

kwani hakuna shule nzuri hapa TANZANIA?

VAENI SARE ZA FEZA, ILBORU, TABORA SCHOOLS, NGANZA, SHULE YA MSINGI JANJA JANJA NA T-SHIRTS ZA VYUO VYETU KAMA MLIMANI NA UDOM...

JAMANI JESHI NI SECTOR NYETI... IACHENI KAMA ILIVYO..!

Kwanza hata hizo za jeshi zenyewe hazipendezi sanasana ni watoto, mateja na
wavuta bangi wanaonyanyua chuma ndo huzipenda.
 
Inahitajika elimu kwa wananchi kuhusu sheria ya mavazi ya majeshi ili hata ikitokea mtu kakiuka basi hata raia walioko mtaani watasaidia kumkamata na kumfikisha mahala husika.

Kwa upande mwingine nafikiri kuna tatizo hata kwenye majeshi yetu yaani JWTZ, Polisi na Magereza. Utakuta vifaa vya jeshi yakiwemo mavazi vinawafikia raia wa kawaida kupitia hao hao askari. Mfano buti, kombati na hata bunduki na hatimaye kukamatwa ktk matukio mbalimbali ya kihalifu.

Mbona hilo la kuvaa sare za jeshi kwamba ni kosa linajulikana hadi huku kwetu vijijini, kinachosumbua ni kiburi tu cha raia. Aisee, siku raia ajichanganye anga zangu na hizo sare atasimulia.
 
Mkuu, kijiji ulichopo ni moja ya vijiji vichache Tanzania ambapo ufahamu wa sheria ya vifaa na mavazi ya jeshi upo juu, sehemu zingine hawajui kitu.
 
Back
Top Bottom