K Lyn afunguka kuhusu maisha yake na muziki

K Lyn afunguka kuhusu maisha yake na muziki

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
MENGI.jpg

Ni nadra sana kukutana na Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi maarufu kama K-Lynn, lakini kupitia Tuzo za Watu tulifanikiwa kupiga story mbili tatu. K-Lynn ameiambia Bongo5 kuwa maisha akiwa kama mama watoto wawili mapacha yamekuwa ya aina yake na anayafurahia kila sekunde.

"Nimejifunza kuwa mvumilivu, nimejifunza upendo ambao sijawahi kujisikia kabla. Jinsi unavyompenda mtoto ni tofauti ambavyo unaweza kumpenda mtu yoyote yule katika maisha yako," alisema.

Katika hatua nyingine, Miss Tanzania huyo wa zamani alisema hakuna uwezekano wowote wa yeye kurejea tena kwenye muziki.

"Kwa bahati nzuri sana baada ya kufanya uamuzi wa kutokuwa kwenye muziki. Niliweza kupata kitu kingine ambacho kimeuteka moyo wangu. Kufanya interior design kunanifurahisha kuliko hata muziki. Nafurahi sana kujua kwamba kuna watu wangependa kunisikia ama kusikia nikiimba, lakini nafikiri moyo wangu umehamia kwenye sanaa nyingine''.

Chanzo: BONGO5
 
Attachments

  • 1432658810280.jpg
    1432658810280.jpg
    51.7 KB · Views: 2,193
Mi nilijua utaelezea jinsi mengi alivyokutongoza ilikuwaje na siku ya kwanza ku do ilikuwaje, unatuletea habar za watoto na mzik mxiuuu
 
Afanye mziki halafu video iweje?Mzee machache hawezi kuvumilia kumuona 'baby' anakumbatiwa sijui nini kama kwenye nalia kwa furaha au nipe mkono.
 
warumi

Hahahahaaa wazee huwa hawatongozi, ni kutolewa dinner tu na mshiko basi kamaliza.
Msiniulize nimejuaje jama nimewahi kuhadithiwa sound za wazee kama machache zilivyo.
 
Last edited by a moderator:
Hahahahaaa wazee huwa hawatongozi, ni kutolewa dinner tu na mshiko basi kamaliza.
Msiniulize nimejuaje jama nimewahi kuhadithiwa sound za wazee kama machache zilivyo.

Ndo ukweli Nifah kutongoza wanatongoza watoto
 
Hahahahaaa wazee huwa hawatongozi, ni kutolewa dinner tu na mshiko basi kamaliza.
Msiniulize nimejuaje jama nimewahi kuhadithiwa sound za wazee kama machache zilivyo.

Mzee anayetongoza hana pesa au kawa chizi!!! Kawaida wazee nguvu za mdomo wazihamishia kidogo chini ili wahifadhi heshima ,,
 
Mzee anayetongoza hana pesa au kawa chizi!!! Kawaida wazee nguvu za mdomo wazihamishia kidogo chini ili wahifadhi heshima ,,

Hahahahaa sipati picha mzee anatongozaje jamani!
Basi nimekumbuka mzee mmoja lecture alimtongoza mwanafunzi mwenzetu eti katika sound zake alimuambia "NIMEKUPENDA ULIVYO MREFU KAMA MBUNI"
Hili jambo kila nikilikumbuka hua nacheka sana.
 
Michejo yake na mzee Mengi inawahusu nini maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua, kula maisha mtoto nakukubali sana
 
Back
Top Bottom