Kaa na ujenge nami

Kaa na ujenge nami

Pambana kaka pambana sanaaa tutatoboa
 
Mwaka huu mwezi wa tatu kwa kipato changu nikaamua kujipiga piga na mimi nianze ujenzi.
Kwanza nilianza kwa kununua tofali za msingi inch 6 kila tofali ilikuwa Tzs 1200 na nikanunua tofali 1400, kufunga mkanda nilitumia nondo 28. Tofali. Kisha tukapata na fundi ujenzi hadi kufunga mkanda wa msingi. Baada ya hapo akanishauri tujenge mashimo ya choo ili kile kifusi kitumike kwenye kujaza msingi.
Tofali zilibaki nikaongeza tena tofali 150 za inch 6 kwa ajili ya kupata tofali za kutosha kwa ajili ya kujengea mashimo. Napo zimebaki kama tofali 30 za inch 6 ambazo fundi kasema zitatumika kujengea ngazi.

Hapana ndipo nimemaliza mwaga zege shimo la mwisho. Nishaweka tofali 800 nitaongeza tofali nyingine 1000 aanze kuinua. Huku tofali za kujengea kuta ni Tzs1100 ambazo ni ngumu. Mpaka sasa ikiwemo hizo tofali 800 nishatumia milion 6.3.
View attachment 2706304View attachment 2706305View attachment 2706306
Nikupe hongera lakini ngoja nikuulize kitu mbona unachafua mazingira
 
Hongera sana. Kujenga ni heshima mjini. Hata ukikosa kipato au luku ikaisha hakuna wa kukuambia kitu! Utapanda matembele na mchicha hukosi mboga au utafuga Bata hukosi kitoweo!
mkuu lile jambo letu vipi,
 
Mie nilitumia mawe kujenga shimo , fundi alitumia fumo wa kupanga mawe bila cement kisha anafunga mkanda baada ya kozi . aliweka kozi 5 na mawe trip 9 zilitumika . kufunika alitumia ndondo 18 , 12mm. Ni very strong sana.
 
Mh tofari nchi 6 kwa 1200, seriously? .huku kwetu nchi 6 no 1700 kwa ratio ya 30 Hadi 32
 
Makadirio yangu hapo nitaongeza tofali 1000 kila tofali ni 1100 so itakuwa 1100000, hapo nna assumu nitatumia kama mifuko 25 ya cement ambapo kila mfuko ni 16000 kwa sasa, mbao za kukodi na mirunda ya kununua kama 4 kwa ajili ya kupandaia. Mchanga upo ila nitaongeza trip nyingine ya 70000 uko. Kokoto zipo ila nitaongeza trip 1 ya 140000. Na nondo n.k na ufundi roughky sitegemei kama sitafika mls 4. Lakini una estimate hivi zinakuja gharama za vitu vidogo vidogo zinaongezeka
Wapi huko mkuu!
 
Back
Top Bottom