Hii ingefika nadhani JF kabla hata shirika la habari le nje kuinyaka. Mimi nimekamatika na habari katika Gazeti la Habari Leo yenye kichwa cha habari "Simba yapokwa pointi za Azam", kitu kilichokuwa kinanishangaza kwanini Simba wanyang'anwe pointi kwa kuchezesha mchezaji mwenye kadi mbili za njano, wakati ni tatu. Lakini nilikasirika zaidi kuona vipi hawa viongozi wanarudia kosa lile lile lililotugharimu nyuma kwa kumchezesha Mgosi wakati alikuwa na kadi tatu. Mwisho wa habari nikakuta "Leo ni siku ya wajinga". Nikabaki nimenyong'onyea mbele ya Computer.