Kabila Joseph ulingoni tena kwenye siasa za uwazi za Congo DR.Hii imekaaje kwa mustakabali wa taifa hili chini ya utawala mpya wa Rais Tshekedi?

Kabila Joseph ulingoni tena kwenye siasa za uwazi za Congo DR.Hii imekaaje kwa mustakabali wa taifa hili chini ya utawala mpya wa Rais Tshekedi?

hapa
Nimemsikiliza mh.Kabila akiwa Seneta Mpya....

BUNGE limeendelea kuiona NGUVU YAKE NA USHAWISHI MKUBWA mpaka Kufikia mwenyewe kusema;anatamani kuwa SENETA WA MILELE....

Kabila anaijua vyema Congo..tunatumai Atashirikiana na Rais Tshisekedi Kuwafurusha Wale Magaidi wa ADF NALU kutoka Kule Misitu Ya Virunga....

Japo Yeye Binafsi Alishindwa kuwamaliza..Basi hiki ni kipindi Mujarabu washirikiane na Serikali Mpya kuwapatia ufumbuzi Wakongomani hao,wanaoteswa na vikundi vyenye uchu wa Raslimali ardhi,Raslimali Misitu na Raslimali PENDWA Madini....
mimi ndo huwa sielewi kabisa hivi rais wa nchi analalaje usingizi mwonono huku akijua sehemu ya nchi yake haitawali?
 
Huyu Kabila yale yaliyomkuta baba yake ndio yatakuja kumkuta kwani ana tamaa sana ya madaraka na wacongomani wanafahamu vyema kuwa yeye ni mtu wa kuja tu.
 
Basi Kabila naye alimu anderweigh jamaa kama aliamin hata furukuta.
Power ni kitu kingine hata kama yeye ndio alimpa (kama inavyodaiwa).
Kwa misukosuko aliyopitia dingi ake wa huyu rais Tshekedi chini ya utawala wa kabila mpaka mauti yanamkuta, Joseph kabila hakupaswa hata kidogo kufikiri atam manage Fatshi.Isingewezekana.Je ni miscalculation alifanya au aliamua kuupuzia uhalia wa mambo anakuja kushtuka mambo si mambo?

Anyway, kwa mtazamo wangu, Rais Tshekedi, bado hajamaliza kazi ya kum neutralize Kabila ,bado..ana kaz kubwa tu ya kufanya na hasa ukizingatia hiv sasa ambapo ameingia bungeni.Asilale, awe naplan B ya kukabiliana na tishio la Kabila.

Pia , mara nyingi rais anapostaaf, ni kama anakua kastaafu siasa kwa ujumla, endapo katiba haimrusu kujishughulisha na majukumu ya kitaifa openly n legally.

Lakin kwa hili la Kabila kurudi bungeni ka seneta, inampa mamlaka ya kugain influence so mbali na zile siasa za chini kwa chini za hila na vificho, jamaa naona ataitumia kuweka mtandao wake kwa namna nyingine ambao unaweza kumpa tabu Rais Tshekedi
Tokea kabila anaunda serikali ya mseto Fatshi alionekana loyal pekee kati ya wapinzani wengine. Nadhani akamuona ni lesser devil kuliko kuwaachia kina Fayulu/Katumbi et al.

Wanasema kinyago ulichotengeneza mwenyewe hakiwezi kukutisha!!
 
Mkuu, kitu cha kujiuliza kwanza Ituri inapakana na Nchi gani - kwa nini adhamini wazi wazi waasi - kama mnafikiri vurugu za waasi lengo lao ni la kisiasa ndani ya taifa la DRC - you are dead wrong, FYI lengo lao ni tofauti kabisa, wanatumika na kuwa funded from outside DRC for hidden agenda.
Kma yupo funded na mabeberu au yule jamaa wa jirani kwanini atumie waasi ilihali alikua na majeshi yote ya kumsaidia kuchota anachotaka?

Kikubwa zaidi anatumia waasi wa jamii ya kilendu na sio wale waliokuwa wanawatumia zamani wahema (Jamii ya Kitutsi) kweli Yule jirani adhamini vikundi vya wabantu na kuacha vya kitutsi??

Kuna vitu havijakaa sawa hapa, nadhani ni movie kali inachezwa
 
Ningekuwa Tshekedi, ningeshughulika na microphone anayotumia kabila bungeni, pia kiti anachokalia bungeni ningekifanyia mambo. Yani Mimi Rais alafu mtu anitishe hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii??
 
Mkimchagua magufuli basi ndugai anaenda kufanya maajabu ya usikteta nchi hii lkn mkimchagua Tundu Lissu basi ndugai atatenguliwa hata ubunge wake maana Lissu haamini mtu kuwakilisha wananchi ambao hawajakuchagua....
 
Hizi katiba zilizoandikwa na nchi za ulaya ni za kutunza wanasiasa badala ya kuhudumia wananchi.
Si wanajua kuwa watawahitaji kwa matumizi ya baadae!!!
Nadhan hiz nchi ambazo tuliachiwa uhuru bila fujo, inawezekana kuna some sorts of agreements tuliafikiana na wakoloni kiroho safi like we have to be paying some dews kila muda fulani then wao wakajiweka kando kuendelea na mambo mengine.

Kuna clip flan acha niitafute nikupandishie hapa, kuna mama mmoja msomi (nadhan ni m senegal) anapiga kelele namna nchi yao inalipa pesa nyingi kwa mwaka kwa aliekuwa mkoloni wao (france kama sikosei)
 
Sawa Sawa!!!ningekuwa Mimi,siku akienda hospitali kutibiwa,harudi tena.Zizi Moja madume mawili.noo
Kwakua na yeye ana experience ya kuwaondoa watu kwa namna moja au nyingine , am sure hiz ni mbinu ndogo sanaa ambazo hata yy tayar ana precaution dhidi yazo
 
Ningekuwa Tshekedi, ningeshughulika na microphone anayotumia kabila bungeni, pia kiti anachokalia bungeni ningekifanyia mambo. Yani Mimi Rais alafu mtu anitishe hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii??
Kumbuka huyu jamaa ame serve kama mwanajeshi pale congo pia ameshakua sponsor wa "tiss" yao kwa miaka mingi huoni kama hiz ni issue ambazo anazijua nje ndani maana mara nying mbinu huwa hazibadilik sana kiviiilee
 
Asubiri kulinywa. Atapigwa risasi kama Baba yake.
 
Mkimchagua magufuli basi ndugai anaenda kufanya maajabu ya usikteta nchi hii lkn mkimchagua Tundu Lissu basi ndugai atatenguliwa hata ubunge wake maana Lissu haamini mtu kuwakilisha wananchi ambao hawajakuchagua....
Kote kote hakueleweki mkuu, Lissu naye ana shaka(mashaka) zake zinazoondoa matumaini hasa ukizingatia ukaribu uliopo kati yake na mataifa ya nje.
Rejea ziara zake na mikutano katika mataifa ya ulaya na marekani.
Na Magufuli naye upande wa bunge na spika Ndugai nako kuna giza tupu. Kitendo cha spika kuondolewa kinga ni hatari sana hasa ukipata spika asiye na busara.
 
Duuu.... Sio kwamba ccm na magufuli ndo wenye ukaribu na mataifa ya nje..... Mbona mikataba ya madini yote wamesainiana nao. Mbona ndege zimenunuliwa canada kwa usiri mkubwa.....
Sasa lissu kaifanya kitu gani mkuu mbona km tunajitoa ufahamu kabisa
 
Back
Top Bottom