Kabila linaweza kubadilika kutoka kabila moja hadi jingine?

Kawaulize watoto wake na watoto wa watoto wake wa kiume! Watakuambisma wao ni Wamasai.

Katafute na taarifa zake za NIDA. Utakuta zinasoma ni Mmasai.

Asili yake ni kabila la Kimeru, lakini kwa sasa ni Mmasai kwa sababu wazazi wake walilowea Umasaini.

Wamasai wa Tanzania na Kenya wanamtambua Lowassa kuwa ni Mmasai mwenzao. Nafikiri alishawahi kupewa hata cheo cha Kimila Umasaini.
 
Kiasili huwezi kujipa kabila.

Kabila unapewa na watu wengine. Kwa mfano wapare walipewa jina hilo na wachaga.
Wachaga nao walipewa jina hilo na mvumbuzi Rebman akimaanisha makundi ya wataita, wakamba, na nilo hamitic walioshi kwenye mitelemko ya mlima Kilimanjaro.

Kujibagua kikabila ni masalia tu ya fikara za mfumo wa kikabaila ambao kwa kweli umekataa kuondoka kwenye jamii karibia zote duniani.

Naunga mkono hoja mkuu.
 
Nashukuru mkuu, umeniongezea kitu.

Nimesikia hata Wasafwa wa Mbeya nao wakipewa hilo jina, nafikiri, na mahasimu wao.

Naomba kujua kuhusu Wachaga! Kwenye miaka ya 1500 hakukuweko na kabila la Kichaga? Inawezekana kabila jingine jipya kuja kuzaliwa maiaka ya mbeleni?
 
DNA only Works For Heredity ya 4 GENEARATION BEYOND THAT HAIWEZI KUFANYA KAZI kwa Hiyi Kwa GENERATION YA sasa hivi hakuna mwenye kabila lake hata moja
Dr, nimeshasikia watu wakidai baadhi ya makabila yaliyopoTanzania yana asili ya Mashariki ya kati. Kuna waliosema Watusi wana vinassba vya Kikushi, wengine wakasema Wamasai wana vinasaba vya Kiyahudi. Lakini ukijaribu kufikiri, naona haiji kabisa.

Inawezekana kwa mtu mweusi kuwa na vinasaba vya watu weupe, au watu weupe kuwa na vinasaba vya watu weusi?
 
Yeah Kuna Reaseach zimefanyika Nyingi zinaprove hivyo...

Na pia kuna Research inaprove kuwa Watu weusi ndo Chanzo cha watu wote Duniani..
kasome kuhusu Euroasian Evolution

 
Mike Mwakatundu (Mike Tee) anajiita mnyalu lakini Mwa Mwa wengi ni wanyakyusa. Babu yake alisogea tu from Mbeya to Iringa miaka hiyo
 
Aisee!

Kwa kweli Dr. uko vizuri. Hongera sana mkuu.

Asante kwa Elimu🙏
 
kuna kabila la wana ccm :
yafatayo
*kabila la chawa wa ccm
hawa hawajulikani koo zao ni zipi kwenye ilo kabira.
*kabila la ccm wazawa
kabila ili linaelekea kutoweka duniani
*kabila la ccm kizazi kipya
hawa ni wafugaji waliongia rumumba na kuloea.
*kabila la ccm wanyonge
hawa wapo wapo hata mtemi wa kabila ili yupo yupo.
*kabila la ccm chifu angaya
ili kabila limebakisha step moja kumaliza kabila lingine ccm wazawa
 
Kabila haswa ni utamaduni na sio damu au DNA. Mzungu aweza kuwa Msambaa.
 
Wachagga ni Mkusanyiko wa makabila mengi ya Tanzania na Kenya.
Ukitaka kupata Historia ya Wachagga nenda pale Chagga caves...na watakueleza vizuri

Wachaga wa Machame wao kiasili ni Wamasai

Waarusha wengi ni Wakibosho hata neno LARUSA ni Ukoo uliopo Kibosho, na Wamasai wanawaita Waarusha "Larusa"

Wapare wa Ugweno wengi ni Wachagga kiasili nq walihamia kule zamani, kule kuna koo za Kimaro, Temba, Msechu n.k
 
Angalia akili ya mtu mweusi inachowaza! Huyu ataisaidia nini nchi yake? Ni aybu! Ndio maana kuanzia mwarabu, waesia na wazungu wanawadharau watu weusi. Wanachoweza ni fitna kati yao wenyewe na kubaguana. Karne hii mtu unajadili ukabila si bora ya nyani kuliko wewe maana anaingizia nchi hii mapato?
 
Jibu ni ndio Kabila linaweza kubadilika na kua kabila lingine ingawa kuna kitu commoni utakikuta pande zote mbili inaweza kuwa phonentic sound au mtindo wa maisha nikupe mfano wa khoi,wasan,wahdzabe na wasandawe hili kiuhalisia ni kabila moja ukilichunguza kutokana na mtindo wao wa maisha na phonentic sound pindi wanapoongea to cut it short "inawezekana"
 
Acha nichukulie wewe ni Mkurya. Ukurya wako utakuwa umetokana na damu ya Kikurya au malezi ya Kikurya?
Ukurya wangu utatokana na damu ya kikurya maana ndio asili yangu.

lakini mimi ni mkurya nikalelewa na mchaga huwezi kusema kabila langu ni mchaga ila utasema ni mkurya ambaye malezi yangu ni meyapata kupitia kabila la kichaga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…