peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Kuna waarusha wanajiita Wamasai.
Mila zao waarusha ni za ajabu sana na tabia zao pia
Mila zao waarusha ni za ajabu sana na tabia zao pia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda niseme kwa namna nyingine!Ukurya wangu utatokana na damu ya kikurya maana ndio asili yangu.
lakini mimi ni mkurya nikalelewa na mchaga huwezi kusema kabila langu ni mchaga ila utasema ni mkurya ambaye malezi yangu ni meyapata kupitia kabila la kichaga.
Umeishia njiani mkuu. Hebu elezea utofauti wao na makabila mengine.Kuna waarusha wanajiita Wamasai.
Mila zao waarusha ni za ajabu sana na tabia zao pia
Huyo mtoa mada kaeleza vizuri sana tu.Huwezi kubadili kabila, hiyo ni kama ngozi ya mwili
Ila unawesa kujifunza na kuishi kama makabira mwengine
Labda niseme kwa namna nyingine!
Ulipozaliwa na kufikia hatua ya kujielewa, ulimkuta mama yako akiishi na baba yako, au mama yako alikujulisha baba yako na kabila lako.
Lakini ujue mama yako naye ni binadamu. Inawezekana alichokuambia ni alichotaka uamini na si ulichopaswa kufahamu.
Pengine, alikuambia kuwa baba yako ni Mkurya hivyo na wewe ni Mkurya, lakini moyoni mwake akawa anujua ukweli mwingine kuwa mimba yako aliipatia kwa mwanaume wa Kichaga.
Kwa mfano huo basi, utamkuta huyo mtu ni Mkurya kwa sababu ya makuzi, lakini ukienda Kisayansi, DNA yake ni Mchaga.
Wewe unafikiri kwa nini Serikali haijarahisisha utoaji wa huduma ya kupima DNA?
Uganda mwanaume mmoja alivunja ndoa baada ya vipimo kuonesha kuwa watoto wote 5 alioamini ni wa kwake hawakuwa damu yake.
Kabila, kwa asilimia nyingi, ni makuzi na si damu.
👏👏👏Labda niseme kwa namna nyingine!
Ulipozaliwa na kufikia hatua ya kujielewa, ulimkuta mama yako akiishi na baba yako, au mama yako alikujulisha baba yako na kabila lako.
Lakini ujue mama yako naye ni binadamu. Inawezekana alichokuambia ni alichotaka uamini na si ulichopaswa kufahamu.
Pengine, alikuambia kuwa baba yako ni Mkurya hivyo na wewe ni Mkurya, lakini moyoni mwake akawa anujua ukweli mwingine kuwa mimba yako aliipatia kwa mwanaume wa Kichaga.
Kwa mfano huo basi, utamkuta huyo mtu ni Mkurya kwa sababu ya makuzi, lakini ukienda Kisayansi, DNA yake ni Mchaga.
Wewe unafikiri kwa nini Serikali haijarahisisha utoaji wa huduma ya kupima DNA?
Uganda mwanaume mmoja alivunja ndoa baada ya vipimo kuonesha kuwa watoto wote 5 alioamini ni wa kwake hawakuwa damu yake.
Kabila, kwa asilimia nyingi, ni makuzi na si damu.
Sijakuelewa mkuu!Ngoja nicheke kwanza 😅 mm ni msukuma na home Kahama ila Mama ni Mnyiramba wa Singida baba ni mzanaki Musoma, Singida nmewah kuish kdg ila Musoma ndio sijawahi hata kufka.
Unafikiri vizazi vyao, mfano watoto watakaozaliwa miaka hamsini ijayo watajinasibu kabila gani? Si ajabu watakuwa wakijitambilisha kabila lao ni Wabondei.Kuna boss wangu wa zamani yeye anadai asili yake ni Songea na ata ubini wake ni watu wasongea ila Babu yake alihamia Tanga Toka enzi za Mwalimu, Hadi Leo hii wao wanaonekana kama watu wa Tanga kaka yake alifariki tukaenda kuzika Tanga, kiufupi wameshakuwa kama wabondei ID ya songea imebaki ukoo tu,
Sahihi kabisa.Huwa ninawashangaa watu wanaojisifia makabila yao katika msingi wa damu. Naamini, kama vipimo vya DNA vingefanyika, kuna watu wangejishangaa kufahamu kuwa hawana uhusiano wa damu na kabila analojinasibu nalo.
Kabila, kwa mtazamo wangu, msingi wake ni utamaduni na si damu.
Miaka ya nyuma, nilikutana na watu kadhaa ambao makabila yao yalikuwa na asili ya kabila jingine.
Mmoja aliniambia kuwa yeye ni Mchaga wa Marangu, lakini babu yake na bibi yake walikuwa ni Wamasai kutoka Arusha. Babu yao aliamua kwenda kununua ukoo kwa Wachaga baada ya kutokea ugomvi baina yake na ndugu zake na kupelekea kulikana kabila lake. Kipindi babu yake anaenda kuomba ukoo kwa Wachaga, tayari baba yake msimuliaji alishazaliwa. Hiyo inamaanisha Mmasai alihamia uchagani na watoto wake aliowazaa Arusha Umasaini, hivyo uzao wake uliopatikana Uchagani ni wajukuu.
Mwingine aliniambia yeye ni Mnyakyusa lakini babu na bibi yake walikuwa Wapare.
Mwingine ni familia moja ambayo japo walikuwa wakijitambilisha kuwa kabila lao ni Waarusha, asili yao ni Wameru. Udadisi wangu uliniwezesha kufahamu kuwa japo kwa damu wao ni Wameru, kabila la Waarusha walilipata kupitia babu yao aliyehamia kwa Waarusha.
Miaka ya nyuma, mtu alipotaka ardhi kutoka kwa Waarusha, akiuziwa au kupewa bure, anakuwa sehemu ya hiyo familia iliyompa ardhi. Kwa sababu huyo Mzee alipewa ardhi na Mwarusha, alijihesabu kuwa yeye ni ukoo mmoja na mtu aliyemwuzia/ aliyempa shamba (sikumbuki kama aliuziwa au alipewa bure).
Huyo Mzee japo aliaga dunia mwaka 2006, mpaka sasa uzao wake (watoto, wajukuu, vitukuu) wanajitambulisha kuwa ni kabila la Waarusha japo wana ndugu zao wa damu Meru ambao kabila lao ni Wameru.
Kwa mifano hiyo michache, ni wazi kuwa kabila la mtu si damu pekee, bali utamaduni. Mtu anaweza akawa na damu tofauti na ya kabila analojinasibu nalo
Inafahamika kuwa chimbuko la Mzee Lowassa ni Wameru. Hata sasa anaweza akawa ana ngmdugu zake wa damu kule Meru ambao ni WA kabila la Wameru. Lakini Mzee Lowassa yeye na familia yake kwa sasa kabila lao ni Wamasai.
Hata Wachaga, inasemekana ni mchanganyiko wa Wamasai, Wakamba, Wakahe, Wasambaa, na Wataita.
Kwa sababu hiyo basi, hata ikitokea umeamua kumuasili mtoto mchanga ambaye katelekezwa na kabila lake haijulikani, usione tashwishwi kumwita kabila lako.
Kabila si damu. Ni utamaduni.
Makabila yanaweza kubadilika!
Wachaga asili waliishi sehemu inaitwa mbokomu old moshi wale ndio wenye mila na tamaduni za kichagga ,wakaja wasambaa , wataita , wakikuyu , wasomali ,warabai na maasai wakachangamana na hili kundi dogo likatokea kundi kubwa lenye tamaduni moja na lahaja tofauti zinazoendana kwa ukaribu kulingna na eneo husika.Nashukuru mkuu, umeniongezea kitu.
Nimesikia hata Wasafwa wa Mbeya nao wakipewa hilo jina, nafikiri, na mahasimu wao.
Naomba kujua kuhusu Wachaga! Kwenye miaka ya 1500 hakukuweko na kabila la Kichaga? Inawezekana kabila jingine jipya kuja kuzaliwa maiaka ya mbeleni?
Mkuu, wewe ni miongoni mwa walionielewa.Hii ipo hasa uchagani kuna koo uchagani wengine wamasai wengine ni wasambaa wengine ni wakikuyu wengine wataita wakamba na wasomali , mfano kwenye asili yetu kuna babu yetu zamani alikimbia vita huko Somalia akaja moshi yeye na mke wake, na alikua mwislamu, akapewa shamba na mangi , mwisho wa siku kizazi na kizazi kikapita tukazaliwa sisi tukawa wachaga na wengi ni wakristo wala kiti moto vizuri tu.
SureMkuu, wewe ni miongoni mwa walionielewa.
Kwa hiyo wewe kabila lako ni Mchaga, ila vipimo vya kinasaba vikifanyika Uchaga utakukataa.
Umekuwa Mchaga si kwa sababu ya damu bali makuzi.
Na huo ndiyo ukweli kwa Watanzania wengi.
Utakuta "Mngoni" anamponda "Mjaluo" kwa kuamini kabila lake la "Kingoni" ni bora kuliko la "Kijaluo" kumbe yeye mwenyewe damu yake ni ya "Kijaluo".
Mkuu, kwa nini unaweza kubadili kabila? Kabila ni jina tu mkuu.Mimi nilishauliza hapa je naweza kubadili kabila?
Nawezaje kubadili kabila?
Habari wana JF Ninajua mtu anaweza kubadili mambo makubwa kabisa kama dini, uraia, mke, na timu ya kushabikia. Kwasasa nimelichoka kabila langu, naona kama linakosa swagger. Nifanyaje ili nibadili kabila? Kuoa na kuhamia ukweni au kuhama sehemu niliyopo ni hatua ambazo sitaki kuzichuawww.jamiiforums.com
🙏🙏🙏Lp
👏👏👏
Ulitakiwa uchambue umalize hiyo historia unayoieleza kuna Wachaga wa Vunjo/ Wamarangu, Wachaga wa Moshi na Wachaga Wa Rombo ..mbona hujaelezea wao wanatoka wapi?Ukitaka kupata Historia ya Wachagga nenda pale Chagga caves...na watakueleza vizuri
Wachaga wa Machame wao kiasili ni Wamasai
Waarusha wengi ni Wakibosho hata neno LARUSA ni Ukoo uliopo Kibosho, na Wamasai wanawaita Waarusha "Larusa"
Wapare wa Ugweno wengi ni Wachagga kiasili nq walihamia kule zamani, kule kuna koo za Kimaro, Temba, Msechu n.k