Kabila linaweza kubadilika kutoka kabila moja hadi jingine?

Ukurya wangu utatokana na damu ya kikurya maana ndio asili yangu.

lakini mimi ni mkurya nikalelewa na mchaga huwezi kusema kabila langu ni mchaga ila utasema ni mkurya ambaye malezi yangu ni meyapata kupitia kabila la kichaga.
Labda niseme kwa namna nyingine!

Ulipozaliwa na kufikia hatua ya kujielewa, ulimkuta mama yako akiishi na baba yako, au mama yako alikujulisha baba yako na kabila lako.

Lakini ujue mama yako naye ni binadamu. Inawezekana alichokuambia ni alichotaka uamini na si ulichopaswa kufahamu.

Pengine, alikuambia kuwa baba yako ni Mkurya hivyo na wewe ni Mkurya, lakini moyoni mwake akawa anujua ukweli mwingine kuwa mimba yako aliipatia kwa mwanaume wa Kichaga.

Kwa mfano huo basi, utamkuta huyo mtu ni Mkurya kwa sababu ya makuzi, lakini ukienda Kisayansi, DNA yake ni Mchaga.

Wewe unafikiri kwa nini Serikali haijarahisisha utoaji wa huduma ya kupima DNA?

Uganda mwanaume mmoja alivunja ndoa baada ya vipimo kuonesha kuwa watoto wote 5 alioamini ni wa kwake hawakuwa damu yake.

Kabila, kwa asilimia nyingi, ni makuzi na si damu.
 
Huwezi kubadili kabila, hiyo ni kama ngozi ya mwili
Ila unawesa kujifunza na kuishi kama makabira mwengine
Huyo mtoa mada kaeleza vizuri sana tu.

Sasa hivi mwingiliano wa kijamii ni mkubwa sana, hasa kutokana na siasa za nchi hii kwamba kila raia ana uhuru wa kwenda atakako mradi asivunje sheria.

Kwa hiyo kabila fulani ukiwpima DNA zao, siyo wote utawakuta kuwa na vinasaba na kabila hilo.

Tena waweza kutwa una Dna za kabila unalolidharau na kulichukia.

Ndiyo maana kahitimisha kwa kusema kabila ni utamaduni na siyo damu.
 
Lp
πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
kabila ni utaratibu wa kuishi jinsi mlivyojiwekea kipi tufuate na kipi tuachane nacho hakuna jipya hata wewe hapo kwako unaanzisha kabila lako na kukana misingi ya kabila ulilozaliwa na kuendeleza lako
 
Ngoja nicheke kwanza πŸ˜… mm ni msukuma na home Kahama ila Mama ni Mnyiramba wa Singida baba ni mzanaki Musoma, Singida nmewah kuish kdg ila Musoma ndio sijawahi hata kufka.
 
Ngoja nicheke kwanza πŸ˜… mm ni msukuma na home Kahama ila Mama ni Mnyiramba wa Singida baba ni mzanaki Musoma, Singida nmewah kuish kdg ila Musoma ndio sijawahi hata kufka.
Sijakuelewa mkuu!

Huo ni uhalisia wako au unatania?
 
Kuna boss wangu wa zamani yeye anadai asili yake ni Songea na ata ubini wake ni watu wasongea ila Babu yake alihamia Tanga Toka enzi za Mwalimu, Hadi Leo hii wao wanaonekana kama watu wa Tanga kaka yake alifariki tukaenda kuzika Tanga, kiufupi wameshakuwa kama wabondei ID ya songea imebaki ukoo tu,
 
Unafikiri vizazi vyao, mfano watoto watakaozaliwa miaka hamsini ijayo watajinasibu kabila gani? Si ajabu watakuwa wakijitambilisha kabila lao ni Wabondei.
 
Sahihi kabisa.
 
Kilichopo Jamii fulan ambayo ni inferior hupenda kujitambua kama jamii ambayo ni superior

mfano wasomali wanapenda kujiita waarabu,
wairaq,wasyria nao hujiona waarabu au kama ilivo watu wa Kaskazini mwa Africa hujiita waarabu kwasababu walivamiwa na waarabu.

ndivo ilivo Kuna watu hutoka sehemu moja na kuanza kujiita jina la hilo kabila kwakua tu kabila hilo ni superior au wanawakubali.

Hata koo iko hivo hivo,,,ingawa si sana.

Mtoa maada yupo sahihii
 
Hii ipo hasa uchagani kuna koo uchagani wengine wamasai wengine ni wasambaa wengine ni wakikuyu wengine wataita wakamba na wasomali , mfano kwenye asili yetu kuna babu yetu zamani alikimbia vita huko Somalia akaja moshi yeye na mke wake, na alikua mwislamu, akapewa shamba na mangi , mwisho wa siku kizazi na kizazi kikapita tukazaliwa sisi tukawa wachaga na wengi ni wakristo wala kiti moto vizuri tu.
 
Wachaga asili waliishi sehemu inaitwa mbokomu old moshi wale ndio wenye mila na tamaduni za kichagga ,wakaja wasambaa , wataita , wakikuyu , wasomali ,warabai na maasai wakachangamana na hili kundi dogo likatokea kundi kubwa lenye tamaduni moja na lahaja tofauti zinazoendana kwa ukaribu kulingna na eneo husika.
 
Mkuu, wewe ni miongoni mwa walionielewa.

Kwa hiyo wewe kabila lako ni Mchaga, ila vipimo vya kinasaba vikifanyika Uchaga utakukataa.

Umekuwa Mchaga si kwa sababu ya damu bali makuzi.

Na huo ndiyo ukweli kwa Watanzania wengi.

Utakuta "Mngoni" anamponda "Mjaluo" kwa kuamini kabila lake la "Kingoni" ni bora kuliko la "Kijaluo" kumbe yeye mwenyewe damu yake ni ya "Kijaluo".
 
Sure
 
Mkuu, kwa nini unaweza kubadili kabila? Kabila ni jina tu mkuu.
 
Ulitakiwa uchambue umalize hiyo historia unayoieleza kuna Wachaga wa Vunjo/ Wamarangu, Wachaga wa Moshi na Wachaga Wa Rombo ..mbona hujaelezea wao wanatoka wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…