Kabila linaweza kubadilika kutoka kabila moja hadi jingine?

Ulitakiwa uchambue umalize hiyo historia unayoieleza kuna Wachaga wa Vunjo/ Wamarangu, Wachaga wa Moshi na Wachaga Wa Rombo ..mbona hujaelezea wao wanatoka wapi?
Wachaga walianza kutambulika lini kwa hilo jina? Walifika Kilimanjaro wakiwa Wachaga au Uchaga ulizaliwa kwenye ardhi ya Kilimanjaro?
 
Bado mtazamo wako unafikirisha, unaweza ukawa nautamaduni wa watu fulani lakini kabila lako la asili linabaki vilevile halibadiliki kamwe
Siku hizi watu wana tamaduni za wazungu, lakini huwezi kuwa mzungu sababu unafuata tamaduni za kizungu. Utabaki muhaya tuu.
 
Kabila ni asili/trait lipo associated 100% na biological traits, kuna mtu ukimuangalia tu unajua huyu ni kabila fulani, kuna makabila watu wengi ni wafupi, lingine ni warefu, lingine ni weupe, lingine ni weusi tii, utamaduni ni namna ya kuishi, suala la kununua ukoo au kabila halibadilishi asili yako kibaiolojia hata siku moja, unless kuwe na interracial.

Nb kama unataka kununua ukabila unaruhusiwa, karibu uchaggani tukuuzie ukoo
 
k
Kabila halina uhusiano na damu ila ni jamii zenye life style au tamaduni moja ingawa kutokana na kuishi pamoja na kuoana hawa watu wanakua wanavinasaba vinavyoelekeana.
Hao unaosema masai wa uchagani kama wameoa wachaga basi nao watakua na vinasaba vya uchaga kwasababu ya kuoana

Hii ndio tofauti ya ukoo na kabila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…