NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
Naam, baada ya mauaji ya mtoto mwenye uremavu wa ngozi nimesikia baadhi ya wakuu wa mikoa akiwemo comrade Chalamila akisema kuwa ataanza kula sahani moja na waganga wa kienyeji.
Ni wazo zuri tena wakuu ama viongozi wanastahili pongezi katika hilo lakini NALIA NGWENA akili nyingi kama wanavyoniita huko jukwaa la michezo haswa watani zangu Simba SC.
Natumia jukwaa hili kuishauri serikali haswa wizara husika inapaswa kuangalia au kuchuja matangazo yanayorushwa na baadhi ya redio ikiwemo REDIO RFA, KISS FM N.K nyakati za usiku kuna matangazo ya waganga waijinadi kuwa wao wanatibia na kuwapa mali watu na wazee wa kubeti.
Kupitia vyombo vya habari hivyo Jamiii inajfunza na kuamini kuwa ushirikina ni jambo la kawaida sana maana kama redio tu inawatangaza waganga kwa mantiki hiyo siku mtu akienda kwa mganga akaambiwa leta kiungo cha mtu ili afanikiwe kimaisha hawezi kukataa maana anaona kabisa hawa waganga ni msaada katika taifa maana mpaka vyombo vya habari vinawatangaza hawa waganga.
My take: Vyombo vya habari vinapaswa kuchukua hatua katika hili kwani likipuuzwa tutaendelea kutengeneza jamii yenye imani za kishirikina na jamii dumavu kimawazo badala kufanya kazi kwa bidii inawaza kwenda kutafuta mafanikio kwa waganga.