Kabla hatujaanza na ''Operesheni ya Waganga wa Kienyeji'' tunapaswa kushughulika na baadhi za Redio zinazorusha matangazo ya Waganga

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Naam, baada ya mauaji ya mtoto mwenye uremavu wa ngozi nimesikia baadhi ya wakuu wa mikoa akiwemo comrade Chalamila akisema kuwa ataanza kula sahani moja na waganga wa kienyeji.

Ni wazo zuri tena wakuu ama viongozi wanastahili pongezi katika hilo lakini NALIA NGWENA akili nyingi kama wanavyoniita huko jukwaa la michezo haswa watani zangu Simba SC.

Natumia jukwaa hili kuishauri serikali haswa wizara husika inapaswa kuangalia au kuchuja matangazo yanayorushwa na baadhi ya redio ikiwemo REDIO RFA, KISS FM N.K nyakati za usiku kuna matangazo ya waganga waijinadi kuwa wao wanatibia na kuwapa mali watu na wazee wa kubeti.

Kupitia vyombo vya habari hivyo Jamiii inajfunza na kuamini kuwa ushirikina ni jambo la kawaida sana maana kama redio tu inawatangaza waganga kwa mantiki hiyo siku mtu akienda kwa mganga akaambiwa leta kiungo cha mtu ili afanikiwe kimaisha hawezi kukataa maana anaona kabisa hawa waganga ni msaada katika taifa maana mpaka vyombo vya habari vinawatangaza hawa waganga.

My take: Vyombo vya habari vinapaswa kuchukua hatua katika hili kwani likipuuzwa tutaendelea kutengeneza jamii yenye imani za kishirikina na jamii dumavu kimawazo badala kufanya kazi kwa bidii inawaza kwenda kutafuta mafanikio kwa waganga.
 
Upo sahihi kabisa,hayo matangazo yanakera sana maan wengine habari za uganga hatuzipendi,alafu mara nyingi kuna wadada wanapangwa kutoa ushuhuda mpaka tunajua kabisa ni mambo ya ubabaishaji tu
 
Naam, baada ya mauaji ya mtoto mwenye uremavu wa ngozi nimesikia baadhi ya wakuu wa mikoa akiwemo comrade Chalamila akisema kuwa ataanza kula sahani moja na waganga wa kienyeji.

Ni wazo zuri tena wakuu ama viongozi wanastahili pongezi katika hilo lakini NALIA NGWENA akili nyingi kama wanavyoniita huko jukwaa la michezo haswa watani zangu Simba SC.

Natumia jukwaa hili kuishauri serikali haswa wizara husika inapaswa kuangalia au kuchuja matangazo yanayorushwa na baadhi ya redio ikiwemo REDIO RFA, KISS FM N.K nyakati za usiku kuna matangazo ya waganga waijinadi kuwa wao wanatibia na kuwapa mali watu na wazee wa kubeti.

Kupitia vyombo vya habari hivyo Jamiii inajfunza na kuamini kuwa ushirikina ni jambo la kawaida sana maana kama redio tu inawatangaza waganga kwa mantiki hiyo siku mtu akienda kwa mganga akaambiwa leta kiungo cha mtu ili afanikiwe kimaisha hawezi kukataa maana anaona kabisa hawa waganga ni msaada katika taifa maana mpaka vyombo vya habari vinawatangaza hawa waganga.

My take: Vyombo vya habari vinapaswa kuchukua hatua katika hili kwani likipuuzwa tutaendelea kutengeneza jamii yenye imani za kishirikina na jamii dumavu kimawazo badala kufanya kazi kwa bidii inawaza kwenda kutafuta mafanikio kwa waganga.
Matamko ya baadhi ya wateule kama haya kwa vile hayatokani na utafiti wowote wa kisayansi, huwa yanaishia kuleta madhara/mateso yasiyo ya haki kwa baadhi ya watu wanoukuwa victims. Watu wameanza kufunguka macho sasa. Ukiwasababishia mateso au kuwavunjia heshima mbele ya macho ya jamii, wanakwenda kukushtaki mahakamani uwafidie. Nadhani kesi dhidi ya DC wa Ubungo na kesi nyingine ambazo zimeshaamriwa zitakuwa zinatoa mwanga kwa jamii kujua haki zao na kuchukua hatua kuzidai. Ushirikina/uchawi huwezi kuuondoa kwa kutumia matamko au operesheni, ufumbuzi wake ni mmoja tu: jamii kuelemika/kutaalamika na hii huchukua muda. Experience yangu ni kwamba hata waumini unaowaona ni good practising baadhi yao mambo yakiharibika, huwa wanaacha uumini wao kwa muda, wanakwenda kwa waganga na wakiona kuna improvements ndipo huwa wanaendelea na imani yao tena. Unadhani ni kwa nini? Unadhani operesheni za hawa wakubwa zinaweza kuleta/kuwa na majibu sahihi kwa watu kama hawa? Siamini.
 
Inasemekana waganga sahvi wana ruka live mpaka kwenye mitandao kama tiktok na instagram 😄 wanatibu huko

Ova
 
Nyota njema huonekana jioni pia
Hata baada ya miaka 60 ya uhuru bado watu wako na imani na waganga na wachawi na mitume feki
 
Umeeleweka,

Bila kusahau wanaotutumia meseji kujitangaza kupitia mitandao ya simu.
 
Matamko ya baadhi ya wateule kama haya kwa vile hayatokani na utafiti wowote wa kisayansi, huwa yanaishia kuleta madhara/mateso yasiyo ya haki kwa baadhi ya watu wanoukuwa victims. Watu wameanza kufunguka macho sasa. Ukiwasababishia mateso au kuwavunjia heshima mbele ya macho ya jamii, wanakwenda kukushtaki mahakamani uwafidie. Nadhani kesi dhidi ya DC wa Ubungo na kesi nyingine ambazo zimeshaamriwa zitakuwa zinatoa mwanga kwa jamii kujua haki zao na kuchukua hatua kuzidai. Ushirikina/uchawi huwezi kuuondoa kwa kutumia matamko au operesheni, ufumbuzi wake ni mmoja tu: jamii kuelemika/kutaalamika na hii huchukua muda. Experience yangu ni kwamba hata waumini unaowaona ni good practising baadhi yao mambo yakiharibika, huwa wanaacha uumini wao kwa muda, wanakwenda kwa waganga na wakiona kuna improvements ndipo huwa wanaendelea na imani yao tena. Unadhani ni kwa nini? Unadhani operesheni za hawa wakubwa zinaweza kuleta/kuwa na majibu sahihi kwa watu kama hawa? Siamini.
NAUNGA MKONO 💪
 
Hao viongozi wenyewe wanaenda huko huko kupigwa chale
 
ndio huyu jamaa anajiita BABU .. na mm ndio nashangaa hapa ajabu anajiita babu ila iyo sauti yake ni sauti ya kiijana
 
Back
Top Bottom