Kabla hujasoma Kitabu cha Kabendera, nashauri sana tungesikiliza Mahojiano ya Ghassan na Kabendera

Kuna taarifa kuwa Ben aliuliwa na bwana mkubwa mwenyewe kwa mikono yake. Mungu anamuona huko aliko.
 
Nimemsikiliza vizuri Kabendera. Nimefurahi sana kwa kuthibitisha kwamba yule Mwamba alikua chuma kuliko tulivyofikiria. Kwa nchi iliyopigwa kama ya kwetu,tulihitaji chuma kile kitawale hata miaka 20 angalau....
 
Sasa anakuja mtu katoka zake huko Isanjandugu Kala matoborwa anambishia Kabendera
Hahahahahaa eti kala matoborwa...... Huyu Kabendera hakua fala kama watu wanavyojiaminisha. Usalama wa taifa walikua wanamfahamu na seems nimesema na SEEMS walikua wanampa taarifa nyingi au yeye Kabendera alikua mbele ya wakati wa Usalama wa Taifa.
 
Nimemsikiliza vizuri Kabendera. Nimefurahi sana kwa kuthibitisha kwamba yule Mwamba alikua chuma kuliko tulivyofikiria. Kwa nchi iliyopigwa kama ya kwetu,tulihitaji chuma kile kitawale hata miaka 20 angalau....
Hautaelewa maumivu ni kitu gani hadi Ben Saanane awe kaka yako, Azory Gwanda awe baba yako, Tundu Lissu awe mjomba wako...

Hao wote wanafamilia, kuna siku itakujia utautamani utu badala ya SGR, utaitamani huruma badala ya Fly over..

Mungu anatenda kazi yake katika namna ya ajabu sana.
 
umeongea vyema sana sana
 
Nakala yangu itawasili kesho hapa nilipo.

Nilikuwa naongea na mdau mmoja akasema jamaa kajiamini sasa kuandika lile tukio kulikoni nimemjibu kwa level ya Kabendera na huko alipo hawezi kuwa amekurupuka kuandika hivyo ni anao ushahidi kuhusu hilo ambao mimi na wewe hatuna .

Na akaenda mbele kuwa huenda familia na serikali zikaenda kortini kumshtaki nikamjibu sioni hilo likitokea kirahisi ila napenda litokee maana kupitia hilo tukio tutajua mengi zaidi hadi waliotumwa kumleta ikulu japo nina wasiwasi kama wote bado wako hai ila ni chain ndefu ya watu na matukio mengi hivyo serikali wala familia anytime soon sioni wakienda huko maana hata mtu mwenyewe character yake ilijionyesha hata kama hujakaa nae muda mrefu.
 
Nimesikiliza hayo mahojiano na sasa niko njiani kununua kitabu hicho.

Dikteta aliyekufa ni rahisi sana kumuandika lakini pia tuwe na ushujaa wa kuwaandika na hawa walio hai.
 
Nimemsikiliza hadi mwisho. Hajaelezea ya kwake binafsi (hasa sehemu ya msamaha) kama alivyoelezea kwa wengine
 
Hivi ilitokea nini JPM akamweka ndani wengine hatukuyajua hayo
Sikiliza dakika za mwanzo pale, Jamaa alikua na taarifa nyingi sana na walimshakosakosa kwa risasi
 
Pia kwa nyongeza kujiwezesha kiufahamu, Ili kusadiki baadhi ya masuala yaliyomo katika kitabu cha Eric Kabendera kuwa siyo riwaya ya kusadikika, kuna ukweli kwa vithibitisho, basi msikilize mwalimu huyu :

Jinsi mitandao ya simu inavyotumiwa na wasiojulikana kufuatilia nyendo za watu:

Jinsi ya Kuepuka Kutekwa nyara na watu wasiojulikana ambao pia hawajulikani na 'Serikali Nzima' - MORARA KEBASO AFICHUA


View: https://m.youtube.com/watch?v=inj9f4BUxVwKifaa chako cha kieletroniki kinavyoweza kuwasaidia watu wasiojulikana kukufuatilia kwa njia zifuatazo :
  • Trailing and surveillance
  • Triangulation
  • SIM CARD
  • IMEI
  • LUKU malipo ya umeme kujua makazi
  • APPS za mikopo kuruhusu kufahamu contacts /picha / mikopo chechefu unayodaiwa kama ipo n.k
  • Hacking Software
  • Text msg
  • Dating sites
  • SIMU kuwa ya moto bila kuitumia
  • Microphone ya simu
  • Camera ya simu kuchukua mazingira uliyopo
  • Hata simu za kiswaswadu si salama
  • N.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…