Kabla hujasoma Kitabu cha Kabendera, nashauri sana tungesikiliza Mahojiano ya Ghassan na Kabendera

Swali alilouliza kabendera ni kwanini alishindwa kuonyesha kujutia kwa kufanya chichote kwa familia inayomtegemea Ben? Je aliijali? Baada ya kumuua baba yao? Aliwapa kitu gani ili wasiteseke?

Mimi ningekuuliza kabendera watoto wa Ben wanaishi vipi kukidhi maisha yao? Magu alikuwa anataka aonekane mwema kwa jamii na kutoogopq hata muunba wake kutoa uhai wa kiumne baba wa familia??
 
Ushauona uzungu tayari brainwashed and fuc.ked
 
Nimesikiliza haya mahojiano juzi..sikuwahi waza kama Tanzania kuna waandishi smart hivi.. kumbe wazazi tuna mchango mkubwa kwenye future ya watoto wetu..TUWEKEZE
Ukisikiliza makini, utagundua kama mtoto ameandaliwa, kwanza huyu hakuhitaji kuajiriwa. Alikuwa anapata pesa kimataifa. Unaandika unapata mpunga.

Niliishawahi kupendekeza investigative title moja ya tafiti yangu msimamizi aliikataa, kwa sabb iliguza maeneo yasiyotakiwa kufanyiwa utafiti.

Kwa hiyo uki investigate jambo lazima uwe umeandaliwa. Na ndio maana azori alifanya uandishi wa hatari akapotezwa, hajaandaliwa.

Kumuandaa mtoto sio kumwambia fanya hivi, muachie katika uwanda wa vitabu na kusoma.

Niliguswa na alivyosema mama ake kufa ni kama kuchoma maktaba.

Wengine wazaz wetu wametangulia, halafu eti anakuja mtu anataka aubebe umama. Haipo hiyo
 
Tatizo la kufuga wakimbizi ndani ya nchi.serikali ichukue hatua warundi na wanyarwanda warudishwe makwao wataharibu nchi yetu.hao wako wengi sana serikalini na mitaani tunawalea tu!
 
Tatizo la kufuga wakimbizi ndani ya nchi.serikali ichukue hatua warundi na wanyarwanda warudishwe makwao wataharibu nchi yetu.hao wako wengi sana serikalini na mitaani tunawalea tu!
Ukienda kwa mwendo huo utajikuta hata Wewe Sio Mtanzania, Magufuli walisema hakua Mtanzania pia, au Umesahau?
 
Umesema vyema Sana Ndugu yangu, ukweli wazazi wetu walikua na mchango Mkubwa sana kwetu. Ukifundishwa na mzazi ni tofauti na Mwalimu
 
Hicho kitabu angekiandika kwa kiswahili ningeshakisoma
 
Halafu role ya walinzi ni nini?

Historia inaonesha pale mtawala anapokuwa dikteta, huweza kufanya baadhi ya watu wake wa karibu waliomzunguka kushindwa kuwa waadilifu na kukengeuka kama bosi wao
Watekaji ni watu wasiojulikana lakini wanafahamika. Lengo ni kueneza hofu mitaani, vijijini na katika vitongoji ili kuweza kubakiza madarakani watawala.

Kote duniani watawala madikteta wametumia na wanaendelea kutumia mbinu hizi.

TOKA MAKTABA:

'Demons do not live in hell; they live here'

The Tonton militia, a feared paramilitary organization, was created by President Duvalier of Haiti


View: https://m.youtube.com/watch?v=pNcipLHJ0po
Paramilitaries main task was to spread his terror and crush any resistance to his regime. Led by ruthless henchmen and fanatical followers, the Tonton militia carried out violent assaults, massacres, and torture in the name of Papa Doc Duvalier. The impact of Duvalier's reign of terror was devastating and continues to shape Haiti's history to this day.
 
TOKA MAKTABA:

30 Julai 2019
SACP MAMBOSASA Afunguka SAKATA La MWANDISHI Kukamatwa - "Hajatekwa, Tulimuita Akakataa"


View: https://m.youtube.com/watch?v=HPCOxMN5A54Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro B. Mambosasa, leo Jumanne Julai 30, 2019, amezungumza na waandishi wa habari na amesema walimkamata mwandishi wa habari, Erick Kabendera, Jumatatu, Julai 29, 2019, baada ya kupelekewa wito wa kufika polisi lakini akakaidi na bado wanaendelea kumshikilia kwa mahojiano kuhusu uraia wake.

“Mwandishi huyo aliandikiwa barua ya wito kwa ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito huo. Kila mmoja anapaswa kutii wito bila shuruti na kila mmoja anapaswa kutii ili kuondoa msuguano usiokuwa na lazima. Polisi tunapomwita kwa hiari akakaidi; tunatumia mamlaka tuliyopewa kisheria,” amesema SACP Mambosasa na kuongeza:

“Baada ya kukamatwa, tumesikia taarifa mbalimbali na waandishi wa habari wengine wakisema ametekwa. Niseme kuwa mwandishi huyo hakutekwa, aliitwa lakini kwa ujeuri akawa amekaidi wito huo.


“Tunaendelea kuwasiliana na maofisa uhamiaji ili lile alilotuhumiwa nalo linawekwa mezani kwa yeye kuwahakikishia hao wanaohoji Utanzania wake, na ni rahisi kuthibitisha hilo. Lakini kwa kuwa yeye mwenyewe ana mashaka, akakataa kutii sasa tunaye na taratibu zingine zinafuata.”

N.B;
Tufahamu hilo kuwa Dola ikitumika vibaya siku zote ni kandamizi. Misuli ya dola kuhusu uraia wa Eric Kabendera kama anavyosisitiza kama kamanda wa polisi SACP Lazaro Mambosasa... kamata kwanza, fungua kesi, tupa raia rumande, mnyime raia dhamana, mtupe jela magereza halafu chunguza baadaye...


Dr. Lazaro B. Mambosasa (SACP) LLB (UDSM) Ph.D. Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) kamishna Msaidizii Mwandamizi wa Polisi SACP- Dkt.Lazaro Mambosasa
 
Tatizo la kufuga wakimbizi ndani ya nchi.serikali ichukue hatua warundi na wanyarwanda warudishwe makwao wataharibu nchi yetu.hao wako wengi sana serikalini na mitaani tunawalea tu!

...Magufuli naye alikuwa anatuhumiwa kuwa sio Mtanzania, kwamba Baba yake alikuwa Mrundi.
 
Wewe ndo unashida, waliona tukio ndio waliovujisha hiyo habari, kitendo kilifanyika na aliekifanya ni huyo Mzee wako mbele ya maafisa usalama. na watumishi wengine wa ikulu. Kuanzia siku hiyo wafanyakazi wa ikulu walishikwa na uoga hatari maana kazi ya kusafisha sakafu iliyo loa damu ya binadamu sio mchezo, hayo ni ya kabendera. Mengine tunajaribu tu kutengeneza picha hasa tuzingatia unyeti wa ikulu
 

Abdul Nondo na maswali ya Salim Kikeke


View: https://m.youtube.com/watch?v=w6YJvxUGiKMSimu yangu ilichukuliwa na watekaji ikiwa haina chaji, wakaenda kui charge kisha wakasema nitoe password ... kwanini wapelelezi wameshindwa kujua location niliyokuwa nikiwa na watekaji? Ahoji kiongozi wa ngome ya vijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo akiwa ktk mahojiano na Crown Media yaliyoongozwa na mwandishi nguli Salim Kikeke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…