Marcostilone
JF-Expert Member
- Jun 25, 2023
- 7,018
- 17,932
Unachokipanda ndicho unachovuna.
Ameenda kinyume na kiapo chake kuna viapo vya USIRI DAIMA yani hata ikatokea ukafa Gwajima akakufufua hutakiwi kutoa SIRI na kiapo hicho unakula ukiwa na akili zako timamuPolepole ameuawa kwa kuitukana tusi gani serikali?
Polepole alikua anatoa siri za serikali au siri za kundi la wana mtandao ndani ya CCM?Ameenda kinyume na kiapo chake kuna viapo vya USIRI DAIMA yani hata ikatokea ukafa Gwajima akakufufua hutakiwi kutoa SIRI na kiapo hicho unakula ukiwa na akili zako timamu
Sasa kama serikali yenyewe hujui maana yake huoni unachoandika hapa ni mwendelezo uleule wa kuitukana serikali?. Anyway serikali Ina msemaji wake Mr Msigwa Wacha kuchukua kazi zisizokuhusu, pambana kulisha wanaokutegemea men.Watu wengi wanaolalamikia Serikali wakati mwingine hawajui Serikali ni kitu gani. Mnachanganya mambo. Serikali si Rais peke yake wala Waziri peke yake, ni mfumo mkubwa sana wenye watu wengi. Nesi wa zahanati yuko Serikali, mwalimu yuko Serikali, fundi wa mamlaka ya maji yuko Serikali, injinia wa Halmashauri yuko Serikali, Mtendaji wa kijiji yuko Serikali, watumishi wa wizara wapo Serikali, Mbunge yupo kwenye mfumo wa Serikali na Waziri pia ni Serikali. Kwa hiyo unaposema Serikali imefanya hivi au vile, unatakiwa kuelewa unaongelea mfumo mkubwa wenye watu wengi, na ndani ya mfumo huo kuna watu wema na wabaya, wenye misimamo tofauti na wengine wanafanya maamuzi yao wenyewe. Hata mimi niko kwenye mfumo wa Serikali lakini haimaanishi kwamba kila kinachofanywa na kila mtu ndani ya Serikali nakihusika nacho. Tatizo ni kwamba watu wengine wanaingia mitandaoni na kudhani kila kitu ni mchezo, wanatukana viongozi kwa sababu tu wanajua wako nyuma ya keyboard. Kama unaona Serikali imekosea, ikosoe kwa hoja, leta ushahidi, uliza maswali. Lakini usichanganye kukosoa na kumtukana mtu binafsi.
Mfano unaona post ya Mkuu wa Majeshi kuhusu suala la ugaidi, mtu anaingia comment na kuandika “huyu ni Mkuu wa Majeshi, msengerema” au matusi mengine. Sasa hapo unajitafutia nini? Kama sio kuchezea wembe sijui ni kitu gani. Sisema hivi kumtisha mtu wala kuhalalisha mtu yeyote kuumiza mwingine, ila tunapaswa kuelewa binadamu tunatofautiana na si kila mtu ana kiwango sawa cha kuvumilia maneno. Usidhani kwa sababu umemtukana Samia Facebook, Instagram au Jamiiforums basi umeonyesha ushujaa. Kama una hoja, sema hoja yako. Kama una ushahidi, uweke wazi. Lakini matusi ya kutafuta likes na sifa yanaweza kukuingiza kwenye matatizo ambayo hukuyatarajia. Tunaishi kwenye dunia yenye watu wa aina nyingi, na kujua hilo si jambo dogo. Chunga sana ulimi wako, maana wakati mwingine mtu anajichezea mwenyewe wembe halafu baadaye anashangaa kwa nini umemkata. Uhuru wa kukosoa ni muhimu, lakini kutumia huo uhuru kwa busara ni muhimu zaidi.
Hivi unaamini kama kuna watu tu katika mfumo wamelishwa sumu kiasi kwamba wanaweza kuona umemtukana kiongozi basi wakaamua tu kujichukulia mambo wanelewa zao pombe wakaamua tu acha tule sahani moja na huyu dogo ukajikuta matatizoni na hapo hata hawajatumwa na huyo kiongozi nyakati sio hizi msifananishe Africa na nchi za watu waliostaraabika zamani.
Taarifa hizo alizipata akiwa wapi ? Kama zilikuwa kutokana na majukumu yake na zikawa vetted SIRI basi wanaishia hapoPolepole alikua anatoa siri za serikali au siri za kundi la wana mtandao ndani ya CCM?
Rostam ana cheo gani ndani ya serikali?
NakaziaHili lijamaa ni kati ya machawa wapumbavu tu🚮
Uko sahihi,Kwa uelewa wangu, mwalimu, nesi, injinia wa serikali n.k, hao sio serikali... Bali ni watumishi wa serikali.
Mfano, Aziz Ki, Mrisho Ngasa n.k hao sio Yanga, ila ni wachezaji wa Yanga... Maana yake siku yoyote wanaweza wasiwe wachezaji wa Yanga.
Lakini serikali, ni serikali milele, kamwe haiwezi kuwa private!!
Ila ningependa kuelimishwa zaidi!
Hili lijamaa ni kati ya machawa wapumbavu tu🚮
Bwashee ,sijakasirika kabisa, nakula bia ila haibadilishi maana kuwa wewe ni lichawa fulani hiviKula bia bwashee acha makasiriko hayasaidii
Watu wengi wanaolalamikia Serikali wakati mwingine hawajui Serikali ni kitu gani. Mnachanganya mambo. Serikali si Rais peke yake wala Waziri peke yake, ni mfumo mkubwa sana wenye watu wengi. Nesi wa zahanati yuko Serikali, mwalimu yuko Serikali, fundi wa mamlaka ya maji yuko Serikali, injinia wa Halmashauri yuko Serikali, Mtendaji wa kijiji yuko Serikali, watumishi wa wizara wapo Serikali, Mbunge yupo kwenye mfumo wa Serikali na Waziri pia ni Serikali. Kwa hiyo unaposema Serikali imefanya hivi au vile, unatakiwa kuelewa unaongelea mfumo mkubwa wenye watu wengi, na ndani ya mfumo huo kuna watu wema na wabaya, wenye misimamo tofauti na wengine wanafanya maamuzi yao wenyewe. Hata mimi niko kwenye mfumo wa Serikali lakini haimaanishi kwamba kila kinachofanywa na kila mtu ndani ya Serikali nakihusika nacho. Tatizo ni kwamba watu wengine wanaingia mitandaoni na kudhani kila kitu ni mchezo, wanatukana viongozi kwa sababu tu wanajua wako nyuma ya keyboard. Kama unaona Serikali imekosea, ikosoe kwa hoja, leta ushahidi, uliza maswali. Lakini usichanganye kukosoa na kumtukana mtu binafsi.
Mfano unaona post ya Mkuu wa Majeshi kuhusu suala la ugaidi, mtu anaingia comment na kuandika “huyu ni Mkuu wa Majeshi, msengerema” au matusi mengine. Sasa hapo unajitafutia nini? Kama sio kuchezea wembe sijui ni kitu gani. Sisema hivi kumtisha mtu wala kuhalalisha mtu yeyote kuumiza mwingine, ila tunapaswa kuelewa binadamu tunatofautiana na si kila mtu ana kiwango sawa cha kuvumilia maneno. Usidhani kwa sababu umemtukana Samia Facebook, Instagram au Jamiiforums basi umeonyesha ushujaa. Kama una hoja, sema hoja yako. Kama una ushahidi, uweke wazi. Lakini matusi ya kutafuta likes na sifa yanaweza kukuingiza kwenye matatizo ambayo hukuyatarajia. Tunaishi kwenye dunia yenye watu wa aina nyingi, na kujua hilo si jambo dogo. Chunga sana ulimi wako, maana wakati mwingine mtu anajichezea mwenyewe wembe halafu baadaye anashangaa kwa nini umemkata. Uhuru wa kukosoa ni muhimu, lakini kutumia huo uhuru kwa busara ni muhimu zaidi.
Hivi unaamini kama kuna watu tu katika mfumo wamelishwa sumu kiasi kwamba wanaweza kuona umemtukana kiongozi basi wakaamua tu kujichukulia mambo wanelewa zao pombe wakaamua tu acha tule sahani moja na huyu dogo ukajikuta matatizoni na hapo hata hawajatumwa na huyo kiongozi nyakati sio hizi msifananishe Africa na nchi za watu waliostaraabika zamani.
Huyu mtu kaongea UKWELI haswa! Sijui tutakavyomjibu ila ni wazo linaloweza kuokoa watu wengi dhidi ya kiitwacho 'HASIRA DHIDI YA SERIKALI'.
Tuwaze hivi, rais anateua watu mbalimbali na kama anaondoka basi ni kawaida hata wateule wake wengi wanaondoka, vp ikiwa wataona hatari ya anayewateua kuondoa, hawatamlinda kwa vyovyote ili waendelee kuwa salama ktk teuzi zao?
Binafsi umenisaidia kuoanza kuona hili dude 'serikali'
Pumzika kwa amani POLEPOLETofautisha kutukana na kutoa Maoni ,wanaokamatwa wengi ni wale wanaotoa maoni.
Kutukana ni kesi ya jinai ,kesi za mitandao zina sheria zake ,wakamate wapeleke mahakamani na si kutekwa na kuuawa.
Polepole alikuwa anatukana?
Naunga MKONO hoja zoteeKwani kusema "huyu mkuu wa majeshi naye msengerema tu" kwa tafsiri yako hili ni tusi...?
Tafsiri ya tusi kutoka ktk kauli fulani ya mtu ni ya mtu mwenyewe..
Kama wewe umeona ni tusi, thibitisha hivyo kwa kwenda mahakamani kupata tafsiri iwapo hilo ni tusi au kauli tu ya kuudhi..
Silaha kuu katika maisha haya hapa duniani ni KUVUMILIANA. Ukikosa Roho wa uvumilivu, itafika wakati hata ukiwa usingizini utakuwa unahisi unatukanwa tu, na kila mtu anayekusemesha, utamuona anakutukana...
Vumilia, focus kwenye mambo yako, acha mambo mengine yapitie sikio la kulia yatokee sikio la kushoto...
Lakini la mwisho ili kuiondoa hiyo "guilty conscious", TUEPUKE KUTENDEANA MABAYA. TUEPUKE TAMAA YA KUJIPATIA MADARAKA NA KUJILIMBIZIA MALI KWA NJIA HARAMU IKIWEMO KUCHUKUA VISIVYO VYAKO. TUPENDANE. MUONE MWENZIO KAMA WEWE. KILA MMOJA AWE MLINZI WA MWENZAKE. Ni kwa namna hii maisha yatakuwa smooth sana..