Kabla hujatukana Serikali, kwanza elewa Serikali ni nini?

Kabla hujatukana Serikali, kwanza elewa Serikali ni nini?

Serikali ni Rais, Baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, tarafa....pamoja na apparatus zake yaani jeshi, polisi, usalama, magereza....
Hizo za nesi kuwa sehemu ya serikali kisa ni mfanyakazi wa serikali ni porojo tu!
Serikali za Africa hazipendi kukosolewa/kutukanwa lazima wakinukishe
 
Acha kutisha watu kindezi, kama i.d yangu ikifichuliwa basi JF inahusika moja kwa moja mana kwenye kujiunga nina haki ya privacy na kulindwa identity yangu lasivyo ningekua najianika platforms zengine.

Kama ni mnufaishwa na asali lazima utetee mzinga kwa namna yoyote ata si ajabu.
 
Yupo bwana mmoja anaitwa Roy alisema shida ya CCM hawajibu hoja kwa hoja halafu hawasomi.
Hoja ikiwashinda wanamshambulia mtoa hoja.
Akaendelea kusema: Chadema wanasoma (wanapenda kujifunza mambo mapya) hawakurupuki.
 
Tukitoka kujua serikali ni nini? Tuangazie Demokrasia ni nini pia
 
Nimejitahidi kusoma hili shairi reeeefu lakini sijaelewa kabisa au ndo akili za katuga zimeanza kuniingia
 
Uchochezi , hakuna nchi inavumilia uchochezi hata huko USA walipopewa uraia hawana ruhusu wa kukosoa wala kufanya uchchezi .
Uchochezi wa nyoko ,mbwa takataka wewe ,unajua nini kuhusu USA condom ya ccm na Malaya samia wewe ?
Yaani raia waache kukosoa uovu na kupigania haki na demokrasia ? ,mpuuzi Kabisa
 
Tofautisha kutukana na kutoa Maoni ,wanaokamatwa wengi ni wale wanaotoa maoni.

Kutukana ni kesi ya jinai ,kesi za mitandao zina sheria zake ,wakamate wapeleke mahakamani na si kutekwa na kuuawa.

Polepole alikuwa anatukana?
Sentensi 6 zimefunga uzi kama gazeti.
Kwa hiki ulichoandika ndugu King Kong III , basi nategemea (kama utimamu upo) mleta uzi aufunge uzi wake.

Ukweli na uhalisia ndio huu ulioandikwa na King Kong III .
 
Watu wengi wanaolalamikia Serikali wakati mwingine hawajui Serikali ni kitu gani. Mnachanganya mambo. Serikali si Rais peke yake wala Waziri peke yake, ni mfumo mkubwa sana wenye watu wengi. Nesi wa zahanati yuko Serikali, mwalimu yuko Serikali, fundi wa mamlaka ya maji yuko Serikali, injinia wa Halmashauri yuko Serikali, Mtendaji wa kijiji yuko Serikali, watumishi wa wizara wapo Serikali, Mbunge yupo kwenye mfumo wa Serikali na Waziri pia ni Serikali. Kwa hiyo unaposema Serikali imefanya hivi au vile, unatakiwa kuelewa unaongelea mfumo mkubwa wenye watu wengi, na ndani ya mfumo huo kuna watu wema na wabaya, wenye misimamo tofauti na wengine wanafanya maamuzi yao wenyewe. Hata mimi niko kwenye mfumo wa Serikali lakini haimaanishi kwamba kila kinachofanywa na kila mtu ndani ya Serikali nakihusika nacho. Tatizo ni kwamba watu wengine wanaingia mitandaoni na kudhani kila kitu ni mchezo, wanatukana viongozi kwa sababu tu wanajua wako nyuma ya keyboard. Kama unaona Serikali imekosea, ikosoe kwa hoja, leta ushahidi, uliza maswali. Lakini usichanganye kukosoa na kumtukana mtu binafsi.

Mfano unaona post ya Mkuu wa Majeshi kuhusu suala la ugaidi, mtu anaingia comment na kuandika “huyu ni Mkuu wa Majeshi, msengerema” au matusi mengine. Sasa hapo unajitafutia nini? Kama sio kuchezea wembe sijui ni kitu gani. Sisema hivi kumtisha mtu wala kuhalalisha mtu yeyote kuumiza mwingine, ila tunapaswa kuelewa binadamu tunatofautiana na si kila mtu ana kiwango sawa cha kuvumilia maneno. Usidhani kwa sababu umemtukana Samia Facebook, Instagram au Jamiiforums basi umeonyesha ushujaa. Kama una hoja, sema hoja yako. Kama una ushahidi, uweke wazi. Lakini matusi ya kutafuta likes na sifa yanaweza kukuingiza kwenye matatizo ambayo hukuyatarajia. Tunaishi kwenye dunia yenye watu wa aina nyingi, na kujua hilo si jambo dogo. Chunga sana ulimi wako, maana wakati mwingine mtu anajichezea mwenyewe wembe halafu baadaye anashangaa kwa nini umemkata. Uhuru wa kukosoa ni muhimu, lakini kutumia huo uhuru kwa busara ni muhimu zaidi.

Hivi unaamini kama kuna watu tu katika mfumo wamelishwa sumu kiasi kwamba wanaweza kuona umemtukana kiongozi basi wakaamua tu kujichukulia mambo wanelewa zao pombe wakaamua tu acha tule sahani moja na huyu dogo ukajikuta matatizoni na hapo hata hawajatumwa na huyo kiongozi nyakati sio hizi msifananishe Africa na nchi za watu waliostaraabika zamani.
Screenshot_20260816-150515~2.png
 
Shida ni kwamba kuna double standards.

Mfano viongozi wetu wa ccm wakisema jukwaani "hao watu tukiwapoteza msiwatafute" inaonekana hoja nzuri na hakuna hatua kwa huyu mtu itachukuliwa.

Kuna mtu amekua maarufu kwa kutishia uhai wa watu na hakuna hatua zimechukuliwa.

Kuna mtu alisema anajulikana kwa kuvunja watu miguu na hakuna hatua zimechukuliwa.
 
Back
Top Bottom