Kabla na baada ya ndoa

Huyu mwamba alichokosea hakumchunguza mwanamke! Hakujipa muda wa kuchunguzs past yake, hakujipa muda wa kuchunguza marafiki zake, hakujipa muda wa kuchunguza familia ya binti anayotoka. Hakujipa muda wa kuchunguza kupitia sehemu ambayo mwanamke anayofanyia kazi angalau kuwauliza mwenendo wake upoje!

Halafu angejipa muda wa kusikilizia huku anamchunguza. Katika hayo lazima kuna kitu angekigundua! Angeliliepuka tatizo mapema. Si kila mwanamke wa kuolewa!
 
Hongera
 
Mie sijawahukumu single mothers wengine... Nimemuhukumu huyu wangu. By the way nilivyoanza nae alikuwa material kwelikweli nikafunika kombe... Ila weeee
Ulikuwa mtego huo ili uingie mzima mzima kwa hiyo ameshakuona umenasa mwili wote sasa anakuonyesha rangi zake halisi na anajua huna cha kumfanya ameshajua madhaifu yako yote huwezi kuchomoka utajifanya kuja kuomba ushauri huku ili ukachukue action ukiingia naye ndani unafyata kimya unakuwa mpole kama sio wewe
 
Be strong brother at your crossroad. You will eventually win the battle soon or later.
 
Shida ya vijana mkiwa humu mnajidai kuwaponda Single Maza lakini ndio hao hao mnawamendea. Kiukweli ni watamu.

Mkuu mechi iluanza na 0 kwa ngapi vile?
 
Nimechunguza nikagundua ndivyo alivyo lakini pia past yake imechangia kumfanya awe hivyo alivyo
Mkuu hawa wenzetu wanapitia Past ngumu sana ambazo zinaacha makovu kwenye mioyo yao.

Wewe ndio Dawa yake. Be patient hui mwaka mmoja sio mkubwa
 
Hakuna cha past, we past yake inakuhusu nini au inahusu nini kwenye maisha yenu ya sasa? Kama anaipenda sana past akaishi nayo, piga chini
Kama hujaingia kwenye ndoa unaweza ona ni rahisi kuachana au kuwa na mchepuko ndo kutakupa furaha. Furaha haipatikani kwa kuchepuka Bali kuchukua maamuzi magumu.

Huenda kwako inakuwa vigumu kuachana nae kwaajili ya uchumi. Kuna wengine wanaandikaga majina ya wake zao kwenye Mali walizonazo, sasa ukimuacha ghalfa unafilisika. Sidhani kama angekuwa nae mpka sasa kwa hivyo visa kama kungekuwa na ishu za kiuchumi.

Ushauri wangu...
1. Kama Kuna share za kiuchumi ambazo ukimuacha basi imekula kwako , Anza kwanza hapo kushughulikia swala la uchumi awe hawezi kujimudu kiuchumi. Mwanamke akijiweza kiuchumi ujue umeisha wengi hawawezi kuwa mlaini tena lakini akiwa tegemezi ananyenyekea anakuwa mpole.

2. Kama haiwezekani kushughulikia mambo ya kiuchumi ( yaani haiwezekani kbsaa) basi ukubali kuanza upya kwa furaha na Amani ya moyo wako.

Ndoa isiwe sababu ya kukosa Amani . Maana lengo la mwanzo la ndoa ni Utulivu, kama Utulivu hakuna na lengo lishapotea, utataka kuitafuta furaha Yako sehemu nyingne ambazo zikakuzamisha kwenye majanga makubwa.

Kama mwanaume ni kuoneshwa msimamo wako uko wapi, nataka hiki na hiki sitaki, ikiwezekana unamhama Hadi kitanda hata chumba. Unakuwa serious na unamaanisha.

Ukimya hauta saidia Chochote ataona yeye yupo sawa na wewe unazingua kumbe yeye ndo anazingua.
 
Hawaaminikagi hao jitathmini sana usuushi kwa kuwaza watu watakuonaje kwa sababu wewe ndio unaexperience uhalisia na sio wao.
 
Endelea kuishi naye... pengne Kuna sababu inafanya anakuwa hivo Anza kumfatilia pengne utagundua
 
Muombe Mungu jaribu kushirikisha viongozi wa Dini ...pia hakuna mkamilifu wewe pia una changamoto zako anakuvumilia
 
Kila siku humu mnapewa somo juu ya kuoa bikra hamuelewi ,sasa wewe huyu single maza wako alikuonyesha mahali alipozikwa mume wake wa kwanza au mada za humu mnaona wanaozichapisha ni akina shilole sio? Basi kaza home boy huu ni ushauri mzuri kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…