Kabla na baada ya ndoa

Kabla na baada ya ndoa

Vpn01

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2024
Posts
245
Reaction score
801
Nipo kwenye ndoa huu mwaka wa sita na nilioa single mother ila kwa yanayoendelea najikuta nipo kwenye wakati mgumu sana wa kimaamuzi juu ya mustakabari wa ndoa yangu

KABLA YA NDOA
Mwanamke alikuwa ananielewa sana, ananisikiliza, ananiheshimu, ni mwepesi kusema samahani

Mwepesi sana kutoka nae out na ni kama alikuwa anaenjoy kiasi flani

Kitandani hakuwa haba, kujituma kama kote mpaka nakuwa nammiss kila nikiwa mbali nae, tulikuwa na uwezo kugegedana popote pale tunapojihisi tupo peke etu, iwe ofisini, garini, dkn, jikoni, sebuleni fainali chumbani ndiyo balaa zito

Nazimiss sana nyakati zile

BAADA YA NDOA
Mwanzo haukuwa mbaya sana wala mzuri sana ila ni vile unajipa moyo kwamba yanapita tu

Kusema samahani ni mpaka tuwe tunakaribia kuachana

Nikimuomba tutoke out haoneshi kufurahia tena kama zamani lakini pia hata akikubali mpo maeneo lakini akili yake ipo nyumbani, ni kama anatoka kuniridhisha mimi na haachi kulalamika kwamba pesa inaharibika, wakati mara nyingi anasisitiza tutume hela kwa ndugu zake na tunatuma na huwa halalamiki kwamba tunaharibu pesa

Penzi ni kama nimesusiwa(D2) nikimuuliza mbona hunyumbuliki au kujituma kama enzi zile anasema hana mazoezi. Na mimi nikimpotezea anaanza kulalamika eti sina hisia nae. Kiufupi anataka mie nifanye kila kitu(inaboa). Kiukweli kuna muda nakuwa na hamu sana ila kumfikia ndiyo nashindwa mpk natamani kujichukulia sheria mkononi

Nimeshaongea nae sana kuhusu tofauti zetu ila hakuna linalobadilika moja kwa moja. Kwa sasa namezea japo naumia ndani kwa ndani

Kitu kingine nimekuja kujua kwamba ni mkali sana hasa kwa watoto kiasi mpaka najisikia vibaya. Kwake yeye hakuna mtu anayejua zaidi yake.

Najikuta mpweke zaidi kuliko nilivyokuwa mpweke kabla sijaoa. Na kabla sijaoa vita yangu kubwa ilikuwa kujiweka vizuri kiuchumi ila baada ya ndoa nahisi nimejiongezea vita nyingine tena kubwa kuliko ile niliyokuwa napigana nayo kwa kipindi kirefu

Nikisema bado nampenda nitakuwa ninaudanganya moyo wangu unless naendelea tu kuishi nae kwa sababu ya watoto na heshima niliyojijengea kwa jamii ila nawaza mpaka lini nitaishi maisha haya

Taasisi ya ndoa ni ya wachache sisi wengine tumedandia tu na ndiyo zinatutafuna. NACHOMOKAJE HAPA?
JamiiForums1510494404.jpg
 
Mkuu, usisahau kuna single mothers wengine wanajitambua.

Huwezi kuwahukumu single mothers wote kwa makosa ya baadhi ya single mothers.
Mie sijawahukumu single mothers wengine... Nimemuhukumu huyu wangu. By the way nilivyoanza nae alikuwa material kwelikweli nikafunika kombe... Ila weeee
 
Past yake imechangiaje kubadilika ndani ya ndoa?

Kama ndivyo alivyo basi badilika wewe ili uishi kwa amani (najua ni vigumu)
Umeongea point sana, niliamua kubadilika ili kuitafuta amani... Ila kubadilika kwenyewe sasa kunanipa maumivu ya ndani kwa ndani... Niliaamua kuacha kumrekebisha ninapohisi anakosea maana ukali umezidi mno... Kwa sasa hata akisema hii 9 wkt mimi naona ni 6 hata sibishani nae

Past yake : kuna nyakati alipitia magumu sana huko nyuma yakamfanya awe monster kwa muda
 
Huyu kama yangu, ila nilifanya maamuzi magumu sana mpaka leo haamini. Single mother ili muende sawa, kule alipoanzia waachane kwa uhasama haswa tofauti na hapo single mother mtihani
Single mothers wana historia tofauti tofauti na wazazi wenza, ukiotea ukampata mzuri utafurahi... Sie tuliojichanganya sasa tunakula sana za uso
 
Pole sana mkuu. Nenda naye taratibu kushughulikia hiyo past yake.

Mi wa kwangu alikuwa anapenda sana kugomba na lugha ya matusi. Nikajua chanzo cha hiyo tabia yake. Nikawa nafanya kumwelimisha taratibu kila anapogomba au kutoa lugha ya matusi. Huu mwaka wa tatu, amebadilika sana.

Anapobadilika positively usiache kumsifia.

Nilimwoa single mother, tuko na amani sana
Umeongea point sana, niliamua kubadilika ili kuitafuta amani... Ila kubadilika kwenyewe sasa kunanipa maumivu ya ndani kwa ndani... Niliaamua kuacha kumrekebisha ninapohisi anakosea maana ukali umezidi mno... Kwa sasa hata akisema hii 9 wkt mimi naona ni 6 hata sibishani nae

Past yake : kuna nyakati alipitia magumu sana huko nyuma yakamfanya awe monster kwa muda
 
Back
Top Bottom