Kabla sijawa tajiri kama kuna mtu anataka kufa, afe kabisa

Kabla sijawa tajiri kama kuna mtu anataka kufa, afe kabisa

Wa kuwa tajiri uwe wewe
Kuna wengine zali linawadondokea tu kuna jamaa namfahamu alitoka kwao mara akaja kwa shemeji yake dsm, kutokana na elimu yake kuwa ndogo jamaa akamtafutia kazi kampuni moja ya ulinzi badae wakampanga lindo hoteli moja kubwa hapo mitaa ya posta ya zamani,

Kuna siku wazungu mtu na mke wake wanaondoka wanawahi ndege ya flying emirates so wakamuomba awasaidie kubeba maboksi wanatoa hotelini yy anazipakia kwenye buti la gari inayowapeleka airport, yalikuwa maboksi 12, bila kujua kuna nini akachukua boks moja akalificha kwenye crumbs cha walinzi pale getini, wale wazungu walipofika airport wakapakia zile boks harakaharaka walifika dubai wakaunga ndege kufika Amsterdam ndio wanastuka box moja halipo wakahisi huenda limesahaulika dubai kuwasiliana na watu wa dubai wanaangalia CCTV camera zinaonekana box 11 tu kurudi bongo wanaogopa coz kama walitumia ujanja kukwepa kodi wakija dili itasanuka,

Yule mlinzi kuja kuchek box ndani lina dhahabu yeye na shemej yake wakaenda kwa mhindi mhindi kupima mzigo akawaambia anatoa MIL400, shemeji mtu akamwambia wakaze maanake kama mhindi anawapa ofa ya mia nne kiurahisi yawezekana mzigo uzidi hiyo bei, wakakomaa mhindi akakubali kuongeza hamsini, jamaa alimpa shemeji yake MIL50 tu, akahama kwa shemeji yake akaenda kuishi Golden tulip zamani Sheraton hotel akanunua Mark two grande enzi hizo ziko kwenye chati alikula hizo na malaya pamoja na kubalisha hotels after four months akanunua nyumba tabata MIL40, akaendeleza bata na warembo kwa sana,

Hashauriki kwa lolote akaenda kwao mara akanunua ngombe bei anataka ya juu kuliko watu wengine after seven months akaanza akauza gari, akaendeleza matanuzi akawa anatembelea tax bubu per day 50,000 baada ya muda akaanza kuuza ngo'mbe zake anapanda ndege anaenda anauza kundi la ng'ombe anarudi dar anafanya vurugu za matanuzi mbaya baadae ndugu wakaona ng'ombe zinaisha wakagawana nao wakauza zilizobaki,

Baada ya mwaka pesa yote ikakata akaanza kumtembelea shemeji yake shemeji akamtolea uvivu alimshauri wafungue biashara ya usafirishaji aligoma akimwambia aende wapange mipango ya maendeleo anamwambia yuko busy anakula bata, jamaa baada kufulia wapambe na warembo wote wakamkimbia akawa anashinda tu ndani, hali ilivyozidi kua ngumu akaanza kuuza vitu vya ndani kimojakimoja vilivyoisha akaanza Kung'oa milango ya vyumbani anauza mpaka akamaliza nyumba yote,

Baadae akaamua kuuza nyumba alipata pesa nzuri tu akahamia mwanza ambapo hawajui akawa anawaambia watu kuwa yeye ni mfanyabiashara wa madini akaendeleza bata kama kawa pesa ilipokata akaenda kijijini napo hakuweza kaa manake watu walikua hawajasahau zle bwebwe zake, bdae akaamua kurud dar sasa hv anachonga mihuri hapo posta kachoka balaa, wale madem waliokua wanakula nae bata sasa hv wakimuona wanamwita shem, kuna jamaa yangu mmoja alimkuta pale stanbic bank jamaa kuona kuna teller karembo basi akasogea akakaomba amwangalizie salio dah anakuta kuna more than 300 mil jamaa akamuomba no. Akapewa wikiendi akapelekwa zenj wakala bata akamhonga na gari

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba si kla mtu amezaliwa ili awe tajiri na si kla mtu anaepata pesa mingi basi atakua tajiri, lakini pia utajiri una vinasaba vya ukoo, kabila,dini na ukanda mfano kuna koo ambazo ili utajirike huitaji kutumia nguvu na maarifa mengi, wakikuyu,wachaga na wakinga, wahindu, waoman, washiraz ni mifano halisi.
 
si kla mtu amezaliwa ili awe tajiri na si kla mtu anaepata pesa mingi basi atakua tajiri, lakini pia utajiri una vinasaba vya ukoo, kabila,dini na ukanda mfano kuna koo ambazo ili utajirike huitaji kutumia nguvu na maarifa mengi, wakikuyu,wachaga na wakinga, wahindu, waoman, washiraz ni mifano halisi.
[/QUOTE]

dah hapo mwisho umeongea maneno mazito sana, kuna watu wao ni kugusa tu wanatoboa ila kuna watu inabidi itumike nguvu kubwa sana..
 
Mbona unajitetea mapema? Huenda hakuna utajiri kutoka kwa Mungu! Yesu alipopandishwa mlimani aliambiwa nini na shetani? Au ndio unapandishwa mlimani?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sawa ndugu mjumbe.
 
Back
Top Bottom