Kabla sijazaliwa Tanzania nilikuwa mzungu niliyeishi Marekani

bishororo

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2017
Posts
254
Reaction score
358
Habari za sikukuuu wapendwa,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 19 nimezaliwa ktk familia ya kawaida tu hapa tz tangu nipo ktk umri mdogo nimekuwa nikiota na kukumbuka mambo mengi ambayo kiuhalisia sijawahi kuyafanya tangu nimezaliwa.

Nimekuwa nikiota mara kwa mara ndoto nipo ktk mazingira tofauti ya ughaibuni na umbo pia na rangi tofauti na mimi yaani white person ikafikia kipindi usiku ninaota ndoto fulani hivi niko na familia yangu ambyo ni watu wenye asili ya kizungu pamoja tupo tunaongea kwa lugha ya kizungu hiki kitu kimenisumbua sana toka nilipoanza kujitambua kwani ni watu wale wale ninawaotaa kila mara nimeombewa sana lakini wapi imefikia kipindi mpaka nikajua kiingereza japo mimi sikusoma kiivo lakini kizungu naongea vizuri.

Sasa katika kupitia zile ndoto ambazo naota na kwakuwa majina ya wale kupitia zile ndoto ninawajua nikaanza kuwatafuta katika mitandao ya kijamii nikiambatanisha na sehemu niliyokuwa naisikia mara kwa mara ndipo nilipopata confirmation ya hiyo familia na historia yao kiufupi kuwa the day mtoto wao pekee alipofariki ndio day mimi nilizaliwa.

Yaani the same year day mpaka saa nilishangaa sana nilipoona picha ya yule jamaa yaani tunafanana kabisa tofauti rangi, ningependa niwaoneshe picha but kutokana na hii JF ilivo sitoweza .

Yaani wale watu niliokuwa nawaota ndo wale wale niliowaona facebook yale mazingira kiufupi nahisi nilikuwa mwanzo naishi huko, nikaamua kutafuta mawasiliano nao nikapata, nikapiga simu niongee nao nilipopiga akapokea mama fulani iv alipopokea akaniita jina ambalo ninasikiaga ndotoni huku akilia akisema my son you still alive? yaani mpaka sasa sijielewi hii no inanitafuta kila mara sasa sijui nifanye nini.

Ushauri wenu plzzzz
 
Unaambiwa maisha ya baadae baada ya kifo Nyerere atazaliwa Tausi na ataishi ikulu.Sasa wewe na kina sie sijui mwanzo tulikuwa nini??!!!Labda wewe ulikuwa hata punda ulaya mkuu
Afu mkuu una dalili zote za mapepo mkuu,unahitaji maombi maana utajua vipi kingereza bila kusoma wala kufundishwa!!!!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka saaaaaaana mkuu eti una dalili za mapepo
 
Hahahhah ili tuanze kukupa ushauri naomba ututhibitishie kwa picha ukiwa mzungu na sa hv ulivyo...pili kama kweli unajua kingereza bila kusoma hebu geuza uzi wako kwa kingereza,,,,nawasalisha hoja
 
sasa kama ushaipata familia yako huko facebook unasubiri nini bongo. nenda zako kwenu mkuu. ila ningekushauri kabla hujaenda onana na Ray kwanza akupe formula yake ya maji, maana ukienda na weusi wako katika familia ya kizungu utajikuta aidha kituo cha polisi au hospitali za vichaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…