Habari za sikukuuu wapendwa,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 19 nimezaliwa ktk familia ya kawaida tu hapa tz tangu nipo ktk umri mdogo nimekuwa nikiota na kukumbuka mambo mengi ambayo kiuhalisia sijawahi kuyafanya tangu nimezaliwa.
Nimekuwa nikiota mara kwa mara ndoto nipo ktk mazingira tofauti ya ughaibuni na umbo pia na rangi tofauti na mimi yaani white person ikafikia kipindi usiku ninaota ndoto fulani hivi niko na familia yangu ambyo ni watu wenye asili ya kizungu pamoja tupo tunaongea kwa lugha ya kizungu hiki kitu kimenisumbua sana toka nilipoanza kujitambua kwani ni watu wale wale ninawaotaa kila mara nimeombewa sana lakini wapi imefikia kipindi mpaka nikajua kiingereza japo mimi sikusoma kiivo lakini kizungu naongea vizuri.
Sasa katika kupitia zile ndoto ambazo naota na kwakuwa majina ya wale kupitia zile ndoto ninawajua nikaanza kuwatafuta katika mitandao ya kijamii nikiambatanisha na sehemu niliyokuwa naisikia mara kwa mara ndipo nilipopata confirmation ya hiyo familia na historia yao kiufupi kuwa the day mtoto wao pekee alipofariki ndio day mimi nilizaliwa.
Yaani the same year day mpaka saa nilishangaa sana nilipoona picha ya yule jamaa yaani tunafanana kabisa tofauti rangi, ningependa niwaoneshe picha but kutokana na hii JF ilivo sitoweza .
Yaani wale watu niliokuwa nawaota ndo wale wale niliowaona facebook yale mazingira kiufupi nahisi nilikuwa mwanzo naishi huko, nikaamua kutafuta mawasiliano nao nikapata, nikapiga simu niongee nao nilipopiga akapokea mama fulani iv alipopokea akaniita jina ambalo ninasikiaga ndotoni huku akilia akisema my son you still alive? yaani mpaka sasa sijielewi hii no inanitafuta kila mara sasa sijui nifanye nini.
Ushauri wenu plzzzz