Kabla ya Kumchagua Mwenyekiti CHADEMA Wafanye Uamuzi Huu Kwanza

... mapendekezo mazuri, ila, kisheria, inabidi yaingizwe kwenye Katiba ya chama!
Hoja nje ya Katiba ni HOJA-MFU!
NB: ... UNAWEZA KUTUNGA SHERIA KATIKATI YA UCHAGUZI?
Raisi wa nchi madaraka yake yapo kwenye katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania (ambayo aitambui katiba ya vyama vya siasa) akishaapishwa.

Raisi anatekeleza ilani ya chama

Katiba ya Tanzania inasema raisi ashitakiwi akiwa madarakani (ni sheria mama) chochote kilichopo kwenye sheria ya chama chako ni inferior.

Sana sana mwenyekiti wa chama anaweza endesha shughuli za chama tu, lakini mtu akishakuwa raisi. Chama akiwezi hata kumfanyia impeachment.

Japo raisi hatoweza kuingilia shughuli za chama chake kama katiba yao ilivyo; Iła chama chake nacho hakiwezi kum-control na yeye. Katika kipindi chake cha uraisi.

Iwapo mwenyekiti wa chama na raisi wa nchi awaelewani; raisi si anakuwa anaenda kwa mtindo wake tu.

Matter of fact huo ndio utaratibu wa CDM toka 2010. Kuna sababu za msingi raisi kutambulika kama kiongozi wa chama kwa namna moja au nyingine anahitaji ushirikiano wa chama hasa kwenye nchi zenye mfumo wa unitary constitution.
 
Ume miss point ya Mzee Mwanakijiji. Kuna mstari amesema '' Mgombea Urais anakuwa kiongozi mkuu wa Chama hadi uchaguzi UTAKAPOMALIZIKA.
 
Binafsi ninachopendekeza ni kuwa wakati wa uchaguzi mgombea wa Urais anakuwa na ukuu katika chama kuondoa migongano kama hii. Linaloendelea CDM sasa hivi ni suala la mgombea Urais na siyo uenyekiti.
 
... mapendekezo mazuri, ila, kisheria, inabidi yaingizwe kwenye Katiba ya chama!
Hoja nje ya Katiba ni HOJA-MFU!
NB: ... UNAWEZA KUTUNGA SHERIA KATIKATI YA UCHAGUZI?
Kumbuka inawezekana kwani kinachokaa sasa hivi ni Mkutano Mkuu wa chama ambacho ndicho chombo cha juu cha chama. Wanaweza kubadilisha Katiba wakitaka. Unless, kuna chombo kingine ambacho kiko juu ya Mkutano Mkuu wa chama.
 
Wewe kosoa chochote usijali hisia za watu; hakuna watoto hapa. Inaonekana unawaza vilivyoandikwa vitabuni. Hakuna kilichopendekezwa ambacho ni nje ya Katiba ya Tanzania au kinachoenda kinyume na dhana ya supremacy of the party. Soma vizuri usikurupuke.
 
Mawazo yako yafanyiwa kazi baada ya uchaguzi mkuu,
Inawezekana kabisa. Kwa mfano, atakayekuwa Mwenyekiti wa Chama atangaze kutokuwa mgombea wa Uraisi na kuwa atafanya jitihada zote kwa mgombea wa Urais. Ikumbukwe Magufuli alipokuwa mgombea wa Urais hakuwa mwenyekiti wa chama na hivyo ilitokea hata kwa Kikwete wakati wa Mkapa. Tatizo lililopo kwenye katiba za vyama ni kuwa zinasema mwenyekiti ana nguvu kubwa sasa ikitokea mwenyekiti na Rais si mtu mmoja basi watu wanakuwa na hofu ya migongano ndio maana huwa inatokea (kwenye CCM) kuunganisha kofia hizi mbili ukishapita uchaguzi. Binafsi, siamini kama ni lazima kwa kadiri ya kwamba mipaka inawekwa wazi na vizuri.
 
Haitowezekana kwa sasa, msingi wa kwanza kabisa wa mabambano ni kuiondoa ccm madarakani , hii bila kujali mtu ni mwenyekiti au sio mwenyeti ili hali tu , yupo na ushawishi atapeperusha ,Pendera, msitutoe kwenye reli, kwani shida nini ,si ndo maana yupo Makam wake
 
Unafikiri kuiondoa CCM madarakani kunakuja kwa kutamani tu? Ni mikakati na sasa hivi CDM hawana mikakati...
 
Chadema wamejenga utaratibu wa fisi.

Yaani wanasubiria mkono wa CCM udondoke.

Wale wasioridhika na mchakato CCM huwa wanawabeba.
Hata ccm ndio hivyo kwa sehemu ya ubunge kama tulivyoona enzi za Magu
 
Shida yako ni kuchanganya siasa za federal constitution na unitary constitution.

Sio swala la vitabu rather how realistic and practicle in party politics za kwetu (a unitary constitution).

Soma vizuri post yangu #19 siasa za unitary constitution hazina tofauti na taratibu za organisation strategic planning.

Sasa ili kufanikisha strategic goals mwenyekiti na raisi kama sio mtu mmoja they have to be on the same page (in unitary constitution) popote duniani, kwa sababu luluki.

Chama ndio kinatoa ilani (sio mtu kama US), chama ndio kina control kura za serikali bungeni (ndio maana kuna whips), chama ndio kinatoa mawaziri (wakigoma kufanya kazi na raisi) hana serikali na mambo luluki kwa mtazamo wa siasa za unitary.

Ni hivi kwenye unitary constitution raisi lazima awe ‘in toe na chama’ na raisi kama sio mwenyekiti wa chama basi hao watu wawili lazima wawe on the same page.

Shida yenu ni kufahamu siasa za marekani na kudhani huo ndio utaratibu wa siasa duniani kote (us politics ni very complicated) and not suitable for developed nations (it needs a serious educated society for those politics).

Yaani ukileta siasa za US nchi zetu na kwa uwezo wetu wa fikra ni shida sio ndogo.

Ukiacha siasa maswala ya kodi US nilikuwa naangalia mshahara wa KAT ambao $61 million dollars mwaka huu, baada ya federal taxes, state taxes (kila state ina mkata tax akicheza) mwisho wa mwaka Ana bąki na net income ya kama $23 million; hawa ni watu hata hesabu ya VAT kwao shida.

Unacheza wewe, be realistic.
 
Yaani Mgombea Urais awe mkubwa kimadaraka kuliko Mwenyekiti wa Chama? Au sijaelewa?
 
Nondo imeenda shule sana hii mkuu, watu wasitake kututoa kwenye reli
 
Binafsi ninachopendekeza ni kuwa wakati wa uchaguzi mgombea wa Urais anakuwa na ukuu katika chama kuondoa migongano kama hii. Linaloendelea CDM sasa hivi ni suala la mgombea Urais na siyo uenyekiti.
Kinachogombewa ni nani ataongoza chama kikuu cha upinzani na hivyo kuamua strategy ya upinzani huo. Sidhani kama Mbowe ana nia ya kugombea urais mwaka huu maana anajua hawezi kushinda.
Kwa pendekezo lako, Lowassa angekiongoza chama wakati anagombea urais!

Amandla...
 
Tatizo wamevuana nguo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…