Kabla ya Kumchagua Mwenyekiti CHADEMA Wafanye Uamuzi Huu Kwanza

... mapendekezo mazuri, ila, kisheria, inabidi yaingizwe kwenye Katiba ya chama!
Hoja nje ya Katiba ni HOJA-MFU!
NB: ... UNAWEZA KUTUNGA SHERIA KATIKATI YA UCHAGUZI?
Raisi wa nchi madaraka yake yapo kwenye katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania (ambayo aitambui katiba ya vyama vya siasa) akishaapishwa.

Raisi anatekeleza ilani ya chama

Katiba ya Tanzania inasema raisi ashitakiwi akiwa madarakani (ni sheria mama) chochote kilichopo kwenye sheria ya chama chako ni inferior.

Sana sana mwenyekiti wa chama anaweza endesha shughuli za chama tu, lakini mtu akishakuwa raisi. Chama akiwezi hata kumfanyia impeachment.

Japo raisi hatoweza kuingilia shughuli za chama chake kama katiba yao ilivyo; Iła chama chake nacho hakiwezi kum-control na yeye. Katika kipindi chake cha uraisi.

Iwapo mwenyekiti wa chama na raisi wa nchi awaelewani; raisi si anakuwa anaenda kwa mtindo wake tu.

Matter of fact huo ndio utaratibu wa CDM toka 2010. Kuna sababu za msingi raisi kutambulika kama kiongozi wa chama kwa namna moja au nyingine anahitaji ushirikiano wa chama hasa kwenye nchi zenye mfumo wa unitary constitution.
 
Mkuu Mwanakijiji
Ninapenda kutofautiana nawe kwenye hili. Kumfanya mgombea urais ama rais kuwa na madaraka ya juu ndani ya chama ni sawa na kurithi usultani wa CCM ambapo rais hawajibiki wala kuwajibishwa na chama. Rais lazima awe obedient kwa chama ili kuchechemiza uwajibikaji....
Labda kama una ufafanuzi wa kina kwenye hili
Ume miss point ya Mzee Mwanakijiji. Kuna mstari amesema '' Mgombea Urais anakuwa kiongozi mkuu wa Chama hadi uchaguzi UTAKAPOMALIZIKA.
 
Mgombea wa Urais atakuwaje juu ya Mwenyekiti wa Chama? Huo ni mfumo wa Marekani ambako mgombea ndie anahesabika kuwa kiongozi wa chama. Mfumo watu wa supremacy ya chama, Mwenyekiti wa Chama Tawala ana nguvu sawa au hata zaidi ya Rais. Tunakumbuka ilivyokuwa wakati wa Mwalimu na Mwinyi. Wote tunajua nani ndie alikuwa mwenye nguvu. Rais atakuwa ana mamlaka zaidi pale tu nafasi za kiutawala hazitaunganishwa na chama. As long as mgombea wa urais atakuwa anachaguliwa na chama Mwenyekiti wake atakuwa na nguvu juu yake. Kuepuka hili ndio maana CCM wakaanzisha utamaduni wa kuviunganisha vyeo hivi.

Amandla...
Binafsi ninachopendekeza ni kuwa wakati wa uchaguzi mgombea wa Urais anakuwa na ukuu katika chama kuondoa migongano kama hii. Linaloendelea CDM sasa hivi ni suala la mgombea Urais na siyo uenyekiti.
 
... mapendekezo mazuri, ila, kisheria, inabidi yaingizwe kwenye Katiba ya chama!
Hoja nje ya Katiba ni HOJA-MFU!
NB: ... UNAWEZA KUTUNGA SHERIA KATIKATI YA UCHAGUZI?
Kumbuka inawezekana kwani kinachokaa sasa hivi ni Mkutano Mkuu wa chama ambacho ndicho chombo cha juu cha chama. Wanaweza kubadilisha Katiba wakitaka. Unless, kuna chombo kingine ambacho kiko juu ya Mkutano Mkuu wa chama.
 
Chama cha siasa ni taasisi (organisation).

Organisation (yeyote) ina malengo (goals and aim) iwe ya biashashara, chama siasa au Charity/NGO/Quasi-Quango.

Aim and objectives za taasisi zina tengeneza strategy ya kufikia malengo
(tunaita ilani kwenye siasa). Vyama vya kijamaa na ubepari vinatamaduni tofauti ya kuandaa ilani.

Watekelezaji wa strategy ni senior civil servant, na wapangaji ni senior management (or dedicated teams) vyama vya siasa. Either way the process is top down approach.

Mawaziri wanasimamia ilani (intervene, how best) ilani yao ifanikiwe au kusimamia kuona civil servants wanafanya kazi sahihi (kuna strategic monitoring measures kupima performance, trouble shooting, risk mitigation planning and so forth).

Raisi ana mandate ya juu kwenye kutekekeza plan ya chama ndio chief executive serikalini na ndani ya chama kwa sababu ndie anaesimamia ilani ilani (mission, goals, objectives and strategy).

Sasa mtu akishakuwa raisi anawezaje kuwa na mwingine wa kumpangia (labda vyama vya siasa viwe na managent board) inayotambulika kwenye katiba ya Tanzania, that’s the only way chama cha siasa kinaweza kum-control raisi.

Kama utasoma kwa makini, utaona upuuzi wa mapendekezo yako.

Kuna wasaa inabidi muambiwe ukweli; you can’t just write things from your heads. Lazima mjue kwanza how things work. Before you write nonsense which doesn’t make sense.

I don’t care about people feelings at times, it’s tiring reading nonsense too.
Wewe kosoa chochote usijali hisia za watu; hakuna watoto hapa. Inaonekana unawaza vilivyoandikwa vitabuni. Hakuna kilichopendekezwa ambacho ni nje ya Katiba ya Tanzania au kinachoenda kinyume na dhana ya supremacy of the party. Soma vizuri usikurupuke.
 
Mawazo yako yafanyiwa kazi baada ya uchaguzi mkuu,
Inawezekana kabisa. Kwa mfano, atakayekuwa Mwenyekiti wa Chama atangaze kutokuwa mgombea wa Uraisi na kuwa atafanya jitihada zote kwa mgombea wa Urais. Ikumbukwe Magufuli alipokuwa mgombea wa Urais hakuwa mwenyekiti wa chama na hivyo ilitokea hata kwa Kikwete wakati wa Mkapa. Tatizo lililopo kwenye katiba za vyama ni kuwa zinasema mwenyekiti ana nguvu kubwa sasa ikitokea mwenyekiti na Rais si mtu mmoja basi watu wanakuwa na hofu ya migongano ndio maana huwa inatokea (kwenye CCM) kuunganisha kofia hizi mbili ukishapita uchaguzi. Binafsi, siamini kama ni lazima kwa kadiri ya kwamba mipaka inawekwa wazi na vizuri.
 
Haitowezekana kwa sasa, msingi wa kwanza kabisa wa mabambano ni kuiondoa ccm madarakani , hii bila kujali mtu ni mwenyekiti au sio mwenyeti ili hali tu , yupo na ushawishi atapeperusha ,Pendera, msitutoe kwenye reli, kwani shida nini ,si ndo maana yupo Makam wake
 
Unafikiri kuiondoa CCM madarakani kunakuja kwa kutamani tu? Ni mikakati na sasa hivi CDM hawana mikakati...
 
Chadema wamejenga utaratibu wa fisi.

Yaani wanasubiria mkono wa CCM udondoke.

Wale wasioridhika na mchakato CCM huwa wanawabeba.
Hata ccm ndio hivyo kwa sehemu ya ubunge kama tulivyoona enzi za Magu
 
Wewe kosoa chochote usijali hisia za watu; hakuna watoto hapa. Inaonekana unawaza vilivyoandikwa vitabuni. Hakuna kilichopendekezwa ambacho ni nje ya Katiba ya Tanzania au kinachoenda kinyume na dhana ya supremacy of the party. Soma vizuri usikurupuke.
Shida yako ni kuchanganya siasa za federal constitution na unitary constitution.

Sio swala la vitabu rather how realistic and practicle in party politics za kwetu (a unitary constitution).

Soma vizuri post yangu #19 siasa za unitary constitution hazina tofauti na taratibu za organisation strategic planning.

Sasa ili kufanikisha strategic goals mwenyekiti na raisi kama sio mtu mmoja they have to be on the same page (in unitary constitution) popote duniani, kwa sababu luluki.

Chama ndio kinatoa ilani (sio mtu kama US), chama ndio kina control kura za serikali bungeni (ndio maana kuna whips), chama ndio kinatoa mawaziri (wakigoma kufanya kazi na raisi) hana serikali na mambo luluki kwa mtazamo wa siasa za unitary.

Ni hivi kwenye unitary constitution raisi lazima awe ‘in toe na chama’ na raisi kama sio mwenyekiti wa chama basi hao watu wawili lazima wawe on the same page.

Shida yenu ni kufahamu siasa za marekani na kudhani huo ndio utaratibu wa siasa duniani kote (us politics ni very complicated) and not suitable for developed nations (it needs a serious educated society for those politics).

Yaani ukileta siasa za US nchi zetu na kwa uwezo wetu wa fikra ni shida sio ndogo.

Ukiacha siasa maswala ya kodi US nilikuwa naangalia mshahara wa KAT ambao $61 million dollars mwaka huu, baada ya federal taxes, state taxes (kila state ina mkata tax akicheza) mwisho wa mwaka Ana bąki na net income ya kama $23 million; hawa ni watu hata hesabu ya VAT kwao shida.

Unacheza wewe, be realistic.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hakuna jinsi. Kinachotokea CHADEMA ni matokeo tu..

Nashauri wafanye uamuzi kuwa atakaye peperusha bendera ya mgombea wa Urais HATOKUWA Mwenyekiti wa chama na kuwa Mwenyekiti wa chama hatokuwa mgombea Urais au Ubunge. Jukumu lake liwe kwenye chama.

Wakati wa kampeni za uchaguzi atakayetangazwa kuwa mgombea wa Urais anakuwa mara moja kuwa ndiyo kiongozi mkuu wa chama hadi baada ya uchaguzi. Mgombea wa Urais kimadaraka anakuwa juu ya Mwenyekiti wa chama.

Faida za hili ni rahisi kuziona. Kubwa ni itaondoa mvutano wa madaraka. Maaana yake ni kuwa wamuombe mtu ambaye anaweza kweli kupeperusha bendera ya ugombea ili awavushe bila mtu huyo kuutaka uenyekiti wa chama.
Yaani Mgombea Urais awe mkubwa kimadaraka kuliko Mwenyekiti wa Chama? Au sijaelewa?
 
Nondo imeenda shule sana hii mkuu, watu wasitake kututoa kwenye reli
 
Binafsi ninachopendekeza ni kuwa wakati wa uchaguzi mgombea wa Urais anakuwa na ukuu katika chama kuondoa migongano kama hii. Linaloendelea CDM sasa hivi ni suala la mgombea Urais na siyo uenyekiti.
Kinachogombewa ni nani ataongoza chama kikuu cha upinzani na hivyo kuamua strategy ya upinzani huo. Sidhani kama Mbowe ana nia ya kugombea urais mwaka huu maana anajua hawezi kushinda.
Kwa pendekezo lako, Lowassa angekiongoza chama wakati anagombea urais!

Amandla...
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hakuna jinsi. Kinachotokea CHADEMA ni matokeo tu..

Nashauri wafanye uamuzi kuwa atakaye peperusha bendera ya mgombea wa Urais HATOKUWA Mwenyekiti wa chama na kuwa Mwenyekiti wa chama hatokuwa mgombea Urais au Ubunge. Jukumu lake liwe kwenye chama.

Wakati wa kampeni za uchaguzi atakayetangazwa kuwa mgombea wa Urais anakuwa mara moja kuwa ndiyo kiongozi mkuu wa chama hadi baada ya uchaguzi. Mgombea wa Urais kimadaraka anakuwa juu ya Mwenyekiti wa chama.

Faida za hili ni rahisi kuziona. Kubwa ni itaondoa mvutano wa madaraka. Maaana yake ni kuwa wamuombe mtu ambaye anaweza kweli kupeperusha bendera ya ugombea ili awavushe bila mtu huyo kuutaka uenyekiti wa chama.
Tatizo wamevuana nguo sana.
 
Back
Top Bottom