Kabla ya kupunguza gharama za kuingiza umeme kuwa 27000, wangefanya huduma hiyo kuwa ya haraka kwa bei ya zamani

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Natamani inchi yangu ijifunze kuangalia kipaumbele cha kero!

Ni kweli kabisa gharama za kuingiza umeme hazitakiwi kuwa kubwa namna ile kutokana na mazingira kwamba Luku na miundo mbinu si Mali ya mteja Bali ni Mali ya mtoa huduma!

Lakini kutokana na mipangilio mibovu, pamoja na kuwepo ile gharama kubwa ya awali lakini wateja walioomba umeme walikaa miezi na miezi kusubiri kuunganishiwa umeme huo!
Hivyo ukitazama hapo kero haikuwa bei kubwa mjini, Bali kero kubwa ilikuwa kwenye ucheleweshwaji wa huduma!

Hivyo kitaalam katika utatuzi wa kero; kama kweli serikali inania njema na wananchi ingehakikisha inaboresha huduma kwanza kiasi cha kufunga luku ndani ya siku 1,2 au 3 mwisho, kwa bei ile ile kubwa ya awali! Halafu ndipo baadae waje na mpango mkakati wa kupunguza bei mijini!

Nasema hivyo kwasababu;

1. Kama bei kubwa walishindwa kuitumia kwa faida ya kutoa huduma bora na haraka, sasa hivi watawezaje kwa bei ya 27000? (Simple logic)..

Yaani ni kama vile magari ya mwendokasi yatangaze kupakia bure wakati pamoja na kulipia nauli msongamano ni mkubwa itakuwaje ikiwa bure watu si watakalia hadi kiti cha dereva?

2. Ukitembelea China na south afrika watengenezaji/ Viwandani wanauza luku kwa bei ya jumla ($1~$3) chini kabisa kati ya 2700 ~10000 kulingana na kiwanda, Je, selikali ilishindwaje kubajeti pesa za wateja wa awali walizolipia gharama kubwa mijini ili iagize Luku nyingi za kutosha ili ziwe zinasubiri wateja ofisini, badala ya wateja kusubiri Kuwekewa luku kwa mda mrefu? Haioni kwamba kipaumbele kilikuwa ni huduma fasta na si bei?

3. Ni matarajio yangu kama serikali wangekuwa serious na bei ile ile kubwa ya mwanzo! Wangeweza hata kulink na halimashauri ili mtu anapoanza ujenzi wa msingi tu Dawasco na Tanesco wamtembelee mteja na kumsogezea huduma ya mda (temporary), halafu akikamilisha ujenzi wanamfungia permanent. Ujenzi unahitaji umeme kwa ajili ya kukata nondo,drill na kupump maji! Hivyo hata mauzo ya Unit yangeongezeka sana!

4. Kwa bei ile ile ya zamani mijini, wangeweza kuwachukulia masaveyor mikopo ya vigari vidogo vyenye 4wheel (mf;Suzuki Jimmy) ambavyo vingekuwa rasmi kwa ajili ya kufanya savey tu, kwanza vinatumia mafuta kidogo, pia wangevifunga GPS, hivyo zoezi la savey lingekuwa rahisi mno kuwafikia wateja!

Yapo mengi sana kuwashauri...lakini kusema ukweli KUPUNGUZA BEI YA KUUNGANISHA UMEME PASIPO KUYAFANYIA KAZI HAYO mmejidanganya! HII BEI YA 27000 Lazima serikali itachemka tu siku si nyingi!

Serikali itaaibika kwa msongamano mkubwa utakaojitokeza!

Halafu mahitaji yatakuwa Mara NNE zaidi ya mwanzo! Maana yake automatically na mda wa kusubili LUKU utakuwa Mara dufu hadi mwaka au miaka miwili!

MTAWAPA KAZI BURE TAKUKURU KUFUATILIA RUSHWA zitakazojitokeza kwa mipango mibovu ya kisiasa! Nashauri Rudisheni bei ya zamani fasta lakini muongeze ufanisi wa kuwahisha Luku

Mijini kero kubwa haikuwa bei kwa sasa, Bali huduma kwanza!

Na hayo ili yawezekane!
Tanesco walitakiwa wajiendeshe kwa makusanyo wanayopata, ili wabajeti wasipange foleni hazina kusubiri pesa zilizolipwa na wateja wao kwa ajili ya huduma!

Maana inasemekana pesa tunazolipia huduma ya umeme huwa zinaenda hazina(Kapu kubwa), zinapangiwa kujenga barabara na huduma nyinginezo kama madawa n.k

( wanajikopesha kwanza pesa zetu kufanya mengine)

Halafu tanesco hugawiwa fungu kidogo kidogo ndiyo maana wanashindwa kuleta vifaa kwa wakati!

Hivyo ilitakiwa Tanesco wangejisimamia fungu lao la pesa! Wachukue kwanza gharama za material (Running cost) mfano 30% ya pesa ya mteja iwe ya tanesco, halafu 70% kinachobaki kama faida ndiyo kitumwe hazina kama faida inayobaki!.

Hii itaongeza uharaka
LAKINI PIA TANESCO wanaweza ishauri Serikali kuwepo mpango wa LUKU FASTA (hii iwe kama kifurushi)
Mpango wa LUKU FASTA Iwe kama fast track ambapo itawafaa wajenzi, na wale wote ambao wangependa LUKU CHAP CHAP yaani unaomba Leo unapewa Leo! Nitaandaa Uzi/thread kwa ajili ya kifurushi cha LUKU FASTA Tanesco
 
Wanasiasa hufanya maamuz kutafuta sifa.

Ila Tanesco huduma nyingine wangekuwa wana outsource tu sio lazima wakomae na kila kitu. Maana hii strategy yao imeprove failure, nchi za dunia ya 3 tunaishi kama manyani tu.
 
Zoezi la 27000 halina logic ya kiutendaji uwezekano wa kubuma ni mkubwa sana!

Inakuwa kama MTU aliyelala uchi na mwanamke usiku kucha kashindwa kula mzigo, sasa kumekucha mbele ya macho ya watu kibao ndo anajitutumua kumpetipeti ili watu waone anaweza! Kumbe hanithi mkubwa!
 
Kuna tatizo kubwa sana hapa. hii kitu italeta rushwa sana. Mimi nashauri bei iwe ileile ya awali ila huduma iwe ya haraka. alafu kama ni kwa mpango wa kuhamasisha basi ili punguzo la elfu 27 liwe na timeframe
 
Yes
 
Kwa maisha ya kiafrika
Jitahidi kwenye simu yako kwenye sile namba muhimu muhimu zisikosenane za TRA, Tanesco, uhamiaji, NEMC, halmashauri ya wilaya, mkuu wa shule etc etc kutegemeana feeding yako😅😅
 
Hahahah
 
TANESCO jamani mnatukwaza Sana sisi wananchi Huduma zenu ni mbovu mmno ishu ndogondogo tu mf mita kukataa kusoma token kushughulikiwa sijui temper Namba hadi utoe rushwa ndio unashughulikiwa
Mnatia aibu embu mjirekebishe
Kuna sehemu na vifrem vyangu 3 nataka niweke kila kimoja mita yake kabla walikuwa wanashare mita moja.
Imekuwa tabu Sana nimeambiwa kwasasa sijui kwa sababu bei ineshuka (27000) shirika haliweki mita mpya kwenye jengo ambalo tayari Lina mita ( mita separation).
Tanesco naomba jibu ni kweli kwamba mita separation haipo tena baada ya bei kushuka?
 
Duh utazani mita ni chakula yaani
 
Kuna mtu anahitaji nguzo mbili ili umeme ufike kwake. Kalipa laki 6.3 huu unaenda mwezi tatu hajaungiwa umeme wanadai nguzo hazitoshi.
Sasa kwenye 27,000/= sijui itakuwaje?
Alipata risiti halali? Hawa ndio wanafanya waliolipia 27,000/= wasipate huduma TANESCO wajitathmini
 
Wanasiasa hufanya maamuz kutafuta sifa.

Ila Tanesco huduma nyingine wangekuwa wana outsource tu sio lazima wakomae na kila kitu. Maana hii strategy yao imeprove failure, nchi za dunia ya 3 tunaishi kama manyani tu.
Wanasiasa hufanya maamuzi kutafuta sifa😁!
 
NI WAKATI SASA TANESCO KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA KWA NGUVU ZOTE ILI TUPATE PROPERTY TAX ZA KUTOSHA JAMENI.
 
Natamani inchi yangu ijifunze kuangalia kipaumbele cha kero!

Ni kweli kabisa gharama za kuingiza umeme hazitakiwi kuwa kubwa namna ile kutokana na mazingira kwamba Luku na miundo mbinu si Mali ya mteja Bali ni Mali ya mtoa huduma!

Lakini kutokana na mipangilio mibovu, pamoja na kuwepo ile gharama kubwa ya awali lakini wateja walioomba umeme walikaa miezi na miezi kusubiri kuunganishiwa umeme huo!
Hivyo ukitazama hapo kero haikuwa bei kubwa mjini, Bali kero kubwa ilikuwa kwenye ucheleweshwaji wa huduma!

Hivyo kitaalam katika utatuzi wa kero; kama kweli serikali inania njema na wananchi ingehakikisha inaboresha huduma kwanza kiasi cha kufunga luku ndani ya siku 1,2 au 3 mwisho, kwa bei ile ile kubwa ya awali! Halafu ndipo baadae waje na mpango mkakati wa kupunguza bei mijini!

Nasema hivyo kwasababu;

1. Kama bei kubwa walishindwa kuitumia kwa faida ya kutoa huduma bora na haraka, sasa hivi watawezaje kwa bei ya 27000? (Simple logic)..

Yaani ni kama vile magari ya mwendokasi yatangaze kupakia bure wakati pamoja na kulipia nauli msongamano ni mkubwa itakuwaje ikiwa bure watu si watakalia hadi kiti cha dereva?

2. Ukitembelea China na south afrika watengenezaji/ Viwandani wanauza luku kwa bei ya chini kabisa kati ya 2700 ~10000 kulingana na kiwanda, Je, selikali ilishindwaje kubajeti pesa za wateja wa awali walizolipia gharama kubwa mijini ili iagize Luku nyingi za kutosha ili ziwe zinasubiri wateja, badala ya wateja kusubiri Kuwekewa luku kwa mda mrefu? Haioni kwamba kipaumbele kilikuwa ni huduma na si bei?

3. Ni matarajio yangu kama serikali wangekuwa serious na bei ile ile kubwa ya mwanzo! Wangeweza hata kulink na halimashauri ili mtu anapoanza ujenzi wa msingi tu Dawasco na Tanesco wamtembelee mteja na kumsogezea huduma ya mda, halafu akikamilisha ujenzi wanamfungia permanent. Ujenzi unahitaji umeme kwa ajili ya kukata nondo,drill na kupump maji! Hivyo hata mauzo ya Unit yangeongezeka!

4. Kwa bei ile ile ya zamani mijini, wangeweza kuwachukulia masaveyor mikopo ya vigari vidogo vyenye 4wheel (Suzuki Jimmy) ambavyo vingekuwa rasmi kwa ajili ya kufanya savey tu, kwanza vinatumia mafuta kidogo, pia wangevifunga GPS, hivyo zoezi la savey lingekuwa rahisi mno kuwafikia wateja!

Yapo mengi sana kuwashauri...lakini kusema ukweli KUPUNGUZA BEI YA KUUNGANISHA UMEME PASIPO KUYAFANYIA KAZI HAYO mmejidanganya!

Serikali itaaibika kwa msongamano mkubwa utakajitokeza!
Halafu mahitaji yatakuwa Mara NNE zaidi ya mwanzo! Maana yake automatically na mda wa kusubili LUKU utakuwa Mara dufu hadi mwaka au miaka miwili!

MTAWAPA KAZI BURE TAKUKURU KUFUATILIA RUSHWA zitakazojitokeza kwa mipango mibovu ya kisiasa!

Mijini kero kubwa haikuwa bei kwa sasa, Bali huduma kwanza!
2. Ukitembelea China na south afrika watengenezaji/ Viwandani wanauza luku kwa bei ya chini kabisa kati ya 2700 ~10000 kulingana na kiwanda, Je, selikali ilishindwaje kubajeti pesa za wateja wa awali walizolipia gharama kubwa mijini ili iagize Luku nyingi za kutosha ili ziwe zinasubiri wateja, badala ya wateja kusubiri Kuwekewa luku kwa mda mrefu? Haioni kwamba kipaumbele kilikuwa ni huduma na si bei?

Mbona hujaweka currency katika hiyo hiyo 2,700~10,000?
 
Hilo shirika la umeme limekuwa takataka tu Kama,ttcl.Hawana mbinu mpya wamekaa kizamani sana,halafu ni kikwazo kwa discovery zingine.
 
2. Ukitembelea China na south afrika watengenezaji/ Viwandani wanauza luku kwa bei ya chini kabisa kati ya 2700 ~10000 kulingana na kiwanda, Je, selikali ilishindwaje kubajeti pesa za wateja wa awali walizolipia gharama kubwa mijini ili iagize Luku nyingi za kutosha ili ziwe zinasubiri wateja, badala ya wateja kusubiri Kuwekewa luku kwa mda mrefu? Haioni kwamba kipaumbele kilikuwa ni huduma na si bei?

Mbona hujaweka currency katika hiyo hiyo 2,700~10,000?
Tshs
 
Back
Top Bottom