Natamani inchi yangu ijifunze kuangalia kipaumbele cha kero!
Ni kweli kabisa gharama za kuingiza umeme hazitakiwi kuwa kubwa namna ile kutokana na mazingira kwamba Luku na miundo mbinu si Mali ya mteja Bali ni Mali ya mtoa huduma!
Lakini kutokana na mipangilio mibovu, pamoja na kuwepo ile gharama kubwa ya awali lakini wateja walioomba umeme walikaa miezi na miezi kusubiri kuunganishiwa umeme huo!
Hivyo ukitazama hapo kero haikuwa bei kubwa mjini, Bali kero kubwa ilikuwa kwenye ucheleweshwaji wa huduma!
Hivyo kitaalam katika utatuzi wa kero; kama kweli serikali inania njema na wananchi ingehakikisha inaboresha huduma kwanza kiasi cha kufunga luku ndani ya siku 1,2 au 3 mwisho, kwa bei ile ile kubwa ya awali! Halafu ndipo baadae waje na mpango mkakati wa kupunguza bei mijini!
Nasema hivyo kwasababu;
1. Kama bei kubwa walishindwa kuitumia kwa faida ya kutoa huduma bora na haraka, sasa hivi watawezaje kwa bei ya 27000? (Simple logic)..
Yaani ni kama vile magari ya mwendokasi yatangaze kupakia bure wakati pamoja na kulipia nauli msongamano ni mkubwa itakuwaje ikiwa bure watu si watakalia hadi kiti cha dereva?
2. Ukitembelea China na south afrika watengenezaji/ Viwandani wanauza luku kwa bei ya chini kabisa kati ya 2700 ~10000 kulingana na kiwanda, Je, selikali ilishindwaje kubajeti pesa za wateja wa awali walizolipia gharama kubwa mijini ili iagize Luku nyingi za kutosha ili ziwe zinasubiri wateja, badala ya wateja kusubiri Kuwekewa luku kwa mda mrefu? Haioni kwamba kipaumbele kilikuwa ni huduma na si bei?
3. Ni matarajio yangu kama serikali wangekuwa serious na bei ile ile kubwa ya mwanzo! Wangeweza hata kulink na halimashauri ili mtu anapoanza ujenzi wa msingi tu Dawasco na Tanesco wamtembelee mteja na kumsogezea huduma ya mda, halafu akikamilisha ujenzi wanamfungia permanent. Ujenzi unahitaji umeme kwa ajili ya kukata nondo,drill na kupump maji! Hivyo hata mauzo ya Unit yangeongezeka!
4. Kwa bei ile ile ya zamani mijini, wangeweza kuwachukulia masaveyor mikopo ya vigari vidogo vyenye 4wheel (Suzuki Jimmy) ambavyo vingekuwa rasmi kwa ajili ya kufanya savey tu, kwanza vinatumia mafuta kidogo, pia wangevifunga GPS, hivyo zoezi la savey lingekuwa rahisi mno kuwafikia wateja!
Yapo mengi sana kuwashauri...lakini kusema ukweli KUPUNGUZA BEI YA KUUNGANISHA UMEME PASIPO KUYAFANYIA KAZI HAYO mmejidanganya!
Serikali itaaibika kwa msongamano mkubwa utakajitokeza!
Halafu mahitaji yatakuwa Mara NNE zaidi ya mwanzo! Maana yake automatically na mda wa kusubili LUKU utakuwa Mara dufu hadi mwaka au miaka miwili!
MTAWAPA KAZI BURE TAKUKURU KUFUATILIA RUSHWA zitakazojitokeza kwa mipango mibovu ya kisiasa!
Mijini kero kubwa haikuwa bei kwa sasa, Bali huduma kwanza!