Kada aliyefukuzwa kwa kutomheshimu Rais Mwinyi adai kuna jambo linafichwa kujiuzulu kwa Waziri Simai

Kada aliyefukuzwa kwa kutomheshimu Rais Mwinyi adai kuna jambo linafichwa kujiuzulu kwa Waziri Simai

View attachment 2884263
ZANZIBAR: Mwanachama zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Shamte amedai kuwa suala la kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohamed Said lina kitu ambacho hakiwekwi wazi juu ya uamuzi huo.

Shamte ambaye alifukuzwa uanachama wa CCM mwaka 2022 kwa kilichoelezwa kuwa ni kutomheshimu Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, amesema kama kitu hicho kitaendelea kufichwa, kuna Mawaziri wengine watajiuzulu.

Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akitajwa kuwa na misimamo inayopingana waziwazi na kilichokuwa chama chake (CCM) ameongeza kuwa kujiuzulu kwa Simai ni sehemu ya Demokrasia ya Vyama vingi.

Ikumbukwe, Januari 24, 2024 Simai aliilalamikia Bodi ya Vileo kubadilisha Mawakala wa kuingiza Vinywaji Zanzibar. Januari 26, 2024, Simai aliamua kuachia nafasi yake katika Serikali ya Zanzibar akidai mazingira yake ya kikazi si rafki kwake.
Wacha wagonjwa wauguzane
 
Interests za nani? 🤔
kila kiongozi wa kisiasa ana political interests zake,

and thus nature of politics,
ndio maana huyu anafanya vile, huyo angependelea iwe hivi na yule mwingine ana taka iwe vile,
na saa zingine mwingine kwa interest zake mpaka anagoma, anazira, ana susa au anaandamana 🐒

yote na yote hiyo ndio siasa...
 
Siasa Siasani, Fitna, Chuki, Husda, Roho Mbaya, Umimi, Undugunization
CCM Jamani Imetushinda Tabia Imeoza Sana
na kwa hulka za kinyumbu na mihemko ya kikenge ya Upinzani nchini,
CCM itawashinda kweli kweli miaka nenda miaka rudi haitawezekana 🤣
 
Wanadamu tuna mengi, ajabu kazi anayoifanya Mwinyi Zanzibar bado ina wapinzani, wakati kwangu ungeniambia nichague kati ya Mwinyi na Samia ningemchagua Mwinyi..

Au hao wakina Shamte tuwapelekee Samia watupe Mwinyi? naona inawezekana, ni suala la kukaa mezani tu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ungejua Rais Samia ndiye anapeleka fedha za miradi kutoka mfuko wa Serikali ya Muungano, usingeandika utopolo huo.

Una chuki tu na Samia inayokufanya usione mapungufu ya Rais Mwinyi
 
kila kiongozi wa kisiasa ana political interests zake,

and thus nature of politics,
ndio maana huyu anafanya vile, huyo angependelea iwe hivi na yule mwingine ana taka iwe vile,
na saa zingine mwingine kwa interest zake mpaka anagoma, anazira, ana susa au anaandamana 🐒

yote na yote hiyo ndio siasa...
Ok. Kwa hiyo hapa hizo tuhuma za “maslahi binafsi na maokoto” zinafit category ya political interests. Sawa.
 
Ok. Kwa hiyo hapa hizo tuhuma za “maslahi binafsi na maokoto” zinafit category ya political interests. Sawa.
kabisaaaa kabisa thr might be political interests over the issue,

tuhuma zinabaki tuhuma tu mpaka zitakapothibitishwa ni makoso pasina shaka na hiyo sasa inakua ajali ya kisiasa, political mistake or political blunder
 
Wanadamu tuna mengi, ajabu kazi anayoifanya Mwinyi Zanzibar bado ina wapinzani, wakati kwangu ungeniambia nichague kati ya Mwinyi na Samia ningemchagua Mwinyi..

Au hao wakina Shamte tuwapelekee Samia watupe Mwinyi? naona inawezekana, ni suala la kukaa mezani tu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Anayepeleka maendeleo Zanzibar ni samia kwa fedha za bara na si mwinyi
 
BREAKING: Chanzo chetu cha uhakika kinatutaarifu kwamba, Mh. Simai amejiuzulu kutokana na swala la ufutwaji wa leseni za kampuni 3 za vileo. Huu ni uamuzi ambao umefanywa na Rais Hussen Mwinyi ili makampuni yake yachukue hizo nafasi. Tuna taarifiwa kuwa Mwinyi ana ikamua ZanzibarView attachment 2884417View attachment 2884418

Sent using Jamii Forums mobile app
Ina maana waziri lilikuwa deal lake la hayo makampuni ya vileo aliponyang'anywa akaanza mdomo.
Bosi anapokunyang'anya deal unatakiwa kuwa mvumilivu na una set mipango mingine
 
Back
Top Bottom