Kada CCM amvaa Mkurugenzi Moshi DC uuzwaji shamba la Shule,ni Deo Mushi

Kada CCM amvaa Mkurugenzi Moshi DC uuzwaji shamba la Shule,ni Deo Mushi

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Deo Mushi kada was CCM na Diwani wa zamani wa Kata ya Kibosho Magharibi amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi Vijijini kuacha mzaha juu ya uuzwaji wa shamba la Shule ya msingi WERENI.

Shamba hilo ambalo miaka mingi limekuwa likitumiwa kwa ajili ya kulima mahindi kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo linadaiwa kuuzwa kwa mfanyabiashara mmoja (jina tunalihifadhi hadi apatikane)ambaye inadaiwa anataka kujenga kituo Cha mafuta .
Kada Huyo anadai kuwa wapo viongozi wanahusika na uuzwaji was shamba hilo na kumunyooshea kidole Moja kwa moja Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,
Amemuomba Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi kuingilia kati jambo Hilo na shamba Hilo lirejeshwe kwa wananchi .
Anasema kwa miaka mingi shamba Hilo mali ya shule ya WERENI limekuwa likitumiwa na wananchi kulima mahindi kwa ajili ya watoto wao.

Je unajua nani kauziwa shamba Hilo,?kesho yunamuweka hapa live akipatikana
 
Back
Top Bottom