Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Elias Mdao, ametangaza rasmi nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kongwa katika Uchaguzi Mkuu ujao, akieleza dhamira yake ya kulihudumia taifa kupitia jimbo hilo.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dodoma, Mdao amesema atachukua fomu pindi dirisha la uchukuaji fomu litakapofunguliwa na chama, akieleza kuwa amesukumwa na ari ya kutaka kuwainua wananchi wa Kongwa kiuchumi na kijamii.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Kipaumbele changu cha kwanza ni kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM. Nitatumia nafasi hiyo kuhakikisha tunaimarisha sekta zisizo rasmi, hususan kwa kuweka mazingira rafiki kwa wakulima na wafugaji, ili kuinua kipato cha wananchi," amesema Mdao.