Kada wa Chadema adai hata Chifu Mangungo hakuwa mpumbavu namna hii. Huu mkataba una nini mbona ukakasi kila kona?

Magungo hakujuwa kusoma na kuandika kwa lugha yoyote alimtegemea mkalimani Ramzan ambaye pia hakujua kusoma tofauti na hawa ma Professor na ma Docter wa kweli na feki wanao ongoza nchi yetu.
Watu kama Musukuma na Kibajaji ndio wa kutafsiri mikataba hawa hawana tofauti na Ramzan wa Mtemi Mangungo na yule Sultan wa Uzigua asiyetajwa sana.
 
Mangungo alidanganywa na Mkalimani mweusi mwambata wa Karl Peters.

Mkalimani huyo alikuwa anamtafsiria Chief Mangungo tofauti kabisa na kilichoandikwa katika mkataba!.

Tofauti ya Mangungo na hawa ni kuwa HAWA WANAJUA KILA KITU KUWA TUNAPIGWA, ILA KWA KUWA HAWATAKI KUJISHUSHA, KUWEKA EGO ZAO PEMBENI NA KUKIRI KUWA TUMEPOTOKA , WANAONA TWENDE HIVYOHIVYO MBELE BILA KUJALI CHOCHOTE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…