KERO Kada ya Afya Ajira Mpya, Wilaya ya Rungwe hatujapata fedha za kujikimu na Viongozi wapo kimya

KERO Kada ya Afya Ajira Mpya, Wilaya ya Rungwe hatujapata fedha za kujikimu na Viongozi wapo kimya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Watumishi wa Kada ya Afya Ajira Mpya, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya bado hatuchapokea hela ya kujikimu, ajabu ni kwamba viongozi hawaongei chochote kuhusu hizo hela.

Utaratibu wa malipo hayo ya kujikimu mwajiriwa inabidi apewe ndani ya wiki mbili tangu aripoti kazini ila sisi mwezi wa tatu sasa tunaenda wa nne ila bado atujapata chochote.

Malipo hayo yamekuwa changamoto kutolewa, kwa halmashauri nyingine huwa hazitolewi kwa wakati na sehemu nyingine hawapewi kabisa.
 
Acha kulia lia kaza ww wenzako walikaa miezi sita hakuna pesa ya kujikimu wala mshahara walikua wanakopeshwa laki moja we wiki nne ushakuja jf halafu jitahid uwe msiri serikali ni kama baba ako sasa baba ako akifanya kosa unaenda tangaza nje
 
Hizi mada zishakuwa nyingi humi kama mnapata Salary achananeni na hayo
 
Halmashauri ya Rungwe, mkoa wa Mbeya ajira mpya 2026 Kada ya Afya wanadhurumiwa haki yao.

Ipo hivi:

Mnamo February 2026 kada ya walimu ajira mpya waliingiziwa pesa ya kujikimu laki tisa na kwa upande wa afya hawakuingiziwa kitu chochote.

Ilivyofika March 2026, kada ya afya wakaanza kudai haki yao kwenye groups za viongozi, walipodai kwa nguvu baada ya siku mbili wakawekewa hela kidogo ambayo hata haifiki nusu ya stahiki zao; ambapo waliingizia laki nne na nusu (wote, haijalishi ni daktari, nurse msaidizi wa afya - wote walingiziwa laki nne na nusu) bila hata kupewa taarifa kuhusu hela yao nyingine imeenda wapi na wanapewa lini.

Na baada ya hapo, lile group la ajira mpya Katibu wa Afya akarifunga ili watu wasihoji juu ya haki zao
 
Screenshot_20260618_193254_WPS Office.jpg


Mnamo tarehe nne mwezi wa 6 mwaka huu kuna kuna barua kutoka kwa katibu mkuu ilisambaa mtandaoni ikielekeza kuwa serikali imeshapeleka fedha za kujikimu kwenye halmashauri na kufikia tarehe kumi na tano mwezi huu tutakuwa tumeishalipwa stahiki zetu ila sasa halmashauri ya Rungwe ya mkoa wa mbeya mpaka sasa hawajatupa mrejesho wowote na tukifatilia hatupewi majibu ya kueleweka na wengine wanatishiwa kuamishwa vituo kupelekwa kijijini
 
Back
Top Bottom