Halmashauri ya Rungwe, mkoa wa Mbeya ajira mpya 2026 Kada ya Afya wanadhurumiwa haki yao.
Ipo hivi:
Mnamo February 2026 kada ya walimu ajira mpya waliingiziwa pesa ya kujikimu laki tisa na kwa upande wa afya hawakuingiziwa kitu chochote.
Ilivyofika March 2026, kada ya afya wakaanza kudai haki yao kwenye groups za viongozi, walipodai kwa nguvu baada ya siku mbili wakawekewa hela kidogo ambayo hata haifiki nusu ya stahiki zao; ambapo waliingizia laki nne na nusu (wote, haijalishi ni daktari, nurse msaidizi wa afya - wote walingiziwa laki nne na nusu) bila hata kupewa taarifa kuhusu hela yao nyingine imeenda wapi na wanapewa lini.
Na baada ya hapo, lile group la ajira mpya Katibu wa Afya akarifunga ili watu wasihoji juu ya haki zao