Kada ya Engineering, ualimu Tamisemi

ilala yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
1,451
Reaction score
2,348
Wakuu naomba tupeane tips jins ya kuomba hizo ajira za ualim kwa sisi wa kada ya engineering.

Nimeona kwenye tangazo kua tuta ajiriwa kama walimu daraja la 111b kwa wenye astashahada na 111c kwa wenye shahada za civil, electrical na mechanical.

Naomba tupeane elimu kidogo tunaombaje ombaje, kuanzia uandikaji wa barua inakuaje, na hiyo system yao inatusuport vipi sie.
 
Kiukweli Magufuli natimu yake wametudharau sana wahandinsi, nchi hii yaviwanda,Serikali iliyoanzisha viwanda kila mahala kwa kadri wana CCM wanavyodai, miradi ya ujenzi kila mahala unamchukua kijana aliejiandaa kuwa muhandisi unataka akafundishe shule, kwa nini hawasemi na madoctor waombe kufundisha shule, kiukweli Magufuli na timu yako mmetudharau sana wahandisi.
 
Mkuu usiongee ivyo hivi Unajua kuna Engineers wapo mtaani wanataabika. Na kama MTU ana njaa afanyeje na hakuna kazi hata za kujitolea. Ishu ni demand and supply ndiyo inayo determine soko ama market value ya products. Pia hujashikiwa bunduki kuziomba mkuu.

Hivi unaijua njaaa ama unaisikiliziaga kwa jirani tu my friend.
 
Naifahamu njaa mkuu, nimeiishi natoka familia masikini kabisa, nawala siwalaumu wahandinsi watakaoomba, bali nailaum Serikali kwakutaka kupoteza nguvu kazi katika kada ya uhandisi, hakuna hata graduate mmoja wauhandisi ataenda kufundisha kwa kuipenda kazi, naamini wengi wao wataenda kwasababu yanjaa, Serikali iangalie kwakweli namna yakusaidia wahandisi aisee. Hii nifedheha kwa Serikali inayojinasibu imeanzisha viwanda 8600 haliyakua kila kiwanda kikichukua wahandisi 2 graduate jumla wanapatikana wahandisi zaidi ya elfu 17.

Kiukweli Magufuli na tamisemi wametudharau sana wahandisi na walaniwe.
 
Nimekupata mkuu pasha,pamoja sana. Ila wapo wanaopenda kufundisha sana mkuu. MIE kufundisha nilipenda ile ya chuo sema GPA haikunipenda
 
Nimekupata mkuu pasha,pamoja sana. Ila wapo wanaopenda kufundisha sana mkuu. MIE kufundisha nilipenda ile ya chuo sema GPA haikunipenda
Mkuu umewaza kwa nini madoctor hawajaambiwa waombe?.

Kiukweli wahandisi pamoja na engineers registration body tunadharaulika sana mkuu.

Yaani ERB kazi yao nikula ada zetu zamwisho wamwaka,badala iangalie namna yakusaidia wahandisi, wamekaa tu pale ofisini nakujipangia kwenda kukagua miradi, ili wapate posho za 500,000 perday kila mtu. Hawana kazi kabisa nahawana namna yakusaidia graduate kabisa.

ERB huwa haina tofauti na chama cha walimu kiukweli.
 
Wangeshirikiana na erb wahakikishe kila mradi unaofanyika engineer kweli yupo hai ama wametumia tu CV yake kuwin tenda ya kazi.
Kuna kAMPUNI zinatumia CV za engineers bila ya wao kujua. Yaani utaratibu ukiwekwa nikagundua kuna kAMPUNI inatumia cv Yangu. Yaani Ninaina Mwanza fa kama walivyoifanyia tigo
 
Sisi wa Mining engineering tukae wapi?
 
Wahandisi siku hizi Ni jkt
 
ERB hamna kitu mzee, mwenyekiti wa bodi na management yake washaridhika, hawana jipya kabisa. Yaani wameshindwa kuongea hata naviwanda au taasisi mbalimbali wahitimu wanapomaliza wawapeleke kupata uzoefu, kiukweli ERB wanakera sana, mimi kipindi nilipomaliza walinipeleka kwenye mradi wamaji ziwa victoria kampuni fulani hivi ya wahindi wanaitwa WAPCOS nilikaa miez miwili nikaacha, nikarudi mjini kufanya mambo yangu.
 
Tanzania ya viwanda alafu wahandisi wanaenda kufundisha form 1.
 
Tanzania ya viwanda iko wapi


Leo engineer wanakuwa walimu

Magu kwanini

Why [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Lengo Magufuli hapa itakuwa namna gani atarudisha mkopo amesomesha vijana halafu hawarudishi kwa kisingizio cha kukosa ajira kaamua wahandisi wakale vumbi la chaki awakabe kisawasawa.​

Mshahara hapa ni 716,000 take home itachezea 540,000 lakini fursa naiona kwa wahandisi wa ujenzi maana halimashauri nyingi hazina wahandisi so wakurugenzi wanaweza kuwatumia wahandisi.​

TAMISEMI ni wizara kubwa ina taasisi kibao mfano TARURA, IDARA ZA UJENZI, DMDP nk kwahiyo unaweza omba kama ticha ukifika kwa mkurugenzi tengeneza connection akubakize.​

Ukienda kushangaa huko utaishia kuchomekea mashati ya kung'aa na suruari za vitamba na kulima kilimo cha mbogamboga, kuandaa andalio la somo mpaka ukome.​

Hii ndiyo Tanzania anayoitaka Mkuu wa Nchi. ERB wapo tu kazi kutumbua ada zetu na Hamna wanachokifanya wameshindwa kusimamia weledi wanaangalia pesa tu wamekomaa kuchangisha michango wajenge jengo sijui la maonesho gani.​

Wanatakiwa wajitathimini hawa kazi kukuza vitambi tu na wanapeana ajira tu kwenye board yao hutwahi kusikia wametangaza kazi pale ni kujuana.
 
Hao wenye taaluma za engineering watapelekwa kwenye technical schools mbalimbali wakawanoe vijana zaidi, good idea.
 
Eti wahandisi wanalamika kuwa hakuna kazi duh! Na hapo sio kudhalauliwa watapelekwa kufundisha Veta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…