Mkuu wangu Kada, heshima mbele ndugu yangu sijui kinachoendelea behind hii ishu, lakini viongozi safi wa taifa letu ni lazima tuwape heshima zao kama inavyotakiwa, na hasa Dr. Slaaa, ninasema hivyo kwa sababu zifuatazo,
1. Mimi nilikuwa JKT Oljoro, ambako sio mbali sana na Karatu, ambako tulikuwa tunaedna kucheza mpira wa miguu kila wakati, na hata kambi yetu ilikuwa na mashamba kule kwa hiyo mara kwa mara tulikuwa tukienda kule na kukaa kwa zamu za miezi, ninajua kuwa wananchi wa kule wanampenda sana huyu mkuu, wala sio ishu kabisa, kutokana na uongozi wake shupavu kule jimboni, toka akiwa kanisani.
2. Yeye alikuwa CCM, yalikuwa ni makosa ya Mkapa, akiwa rais yaliyomfanya Dr. Slaa ahamie upinzani, kamati ya kutathmini na kupendekeza wagombea ubunge wa CCM ilikuwa imemchagua Dr. Slaa kuwa apewe nafasi hiyo na cc, mkapa kwa ujeuri wa makusudi akaamua kuliengua jina la Dr. Slaa, na kumuweka rafiki yake nafikiri ni Quaress, ushauri wote aliopewa kuwa huyu mtu wake hawezi kushinda, akaukataa, matokeo Dr. Slaa, akaingia upinzani na kushinda kiti kile cha ubunge mpaka leo.
3. Dr. Slaa, sasa hivi ni mmoja wa viongozi wachache sana wanaoheshimika sana na hata uongozi wa juu na chini wa CCM, na hasa wabunge kutokana na accuracy ya hoja zake, huwezi kumkuta kiongozi yoyote wa juu wa CCM akimponda Dr. Slaa in private, ukilinganisha na kina Mrema, au Mtikila, ni kwa sababu ni kiongozi makini sana.
Sasa kwa kweli sielewi haya malumbano yalikotokea na yanakokwenda, lakini nimeshitushwa kuona Dr. Slaa akijadiliwa kwa lugha ambayo kwa kweli hastahili kabisaa, yeye ni mmmoja wa viongozi wachache sana wa taifa letu, ambao kuwepo kwao bungeni kunatoa changamoto nzito kwa viongozi wengine wote kuanzia wa upinzani mpaka CCM, kufikiria mara mbili ni kwa nini wapo kule bungeni. sina mpango wa kujiunga na haya malumabano, lakini please tuwape heshima viongozi wanaostahili heshima kama Dr. Slaa.
Ahsante.