Mbowe ajiuzulu`
na dennis luambano
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, ameombwa kujiuzulu nafasi yake kutokana na kudaiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Deni analodaiwa ni wastani wa Sh milioni 43 ambalo ni limbikizo la riba la mkopo wa Sh milioni 15 ambao ulichukuliwa mwaka 1990 kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli ya Mbowe.
Ombi hilo limetolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Mwenyekiti wa Chama cha Social Democratic (SDP) ambacho hakijapata usajili wa kudumu, Nathaniel Mlaki, wakati alipozungumza na MTANZANIA.
Huu ni ushauri wangu ambao ni kama wa kindugu kwamba namuomba ajiuzulu nafasi yake na awaachie wengine kwa sababu kwa kutokufanya hivyo anakivunjia heshima chama chake.
Haiwezekani alimbikize deni kwa kipindi cha miaka 17 na awe anakwepa kulipa mpaka suala lake likafikishwa mahakamani, halafu pamoja na kufikishwa huko bado anaendelea kukwepa kulimalizia, alisema Mlaki.
Alisema kwa kufanya hivyo atakisafisha chama chake na kukifanya kiendelee kuaminiwa na wananchi walio wengi.
Kashfa hii ni nzito na ili aonekane yeye ni muungwana, basi ajiuzulu nafasi hiyo kama nilivyosema hapo mwanzo na asipojiuzulu, basi CHADEMA itumie katiba yake kumuondoa kwenye nafasi hiyo, alisema Mlaki.
Alisema kwa kuwa Mbowe ni mpinzani, basi suala hilo linawahusu wapinzani wote na ili wapinzani waendelee kuonekana ni watu makini, hana budi kuuacha wadhifa wake. Mimi nikiwa kama mpinzani mwenzake na kwa kuutakia upinzani wetu mafanikio, basi kiustaarabu aachie ngazi na kuwaachia wengine waendeleze mapambano hayo, kwa sababu haiingii akilini kusikia mtu aliyewahi kugombea nafasi ya urais leo hii anadaiwa baada ya kukopa fedha za Serikali, alisema Mlaki.
Alisema leo hii ni aibu kwa Mbowe kusimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kuisakama Serikali ya CCM kuhusu mambo ya ufisadi na rushwa huku naye akiwa ni kiongozi anayedaiwa.
Alimtaka Mbowe asilichanganye deni analodaiwa na masuala ya kisiasa kwa sababu kufanya hivyo ni kujitetea pasipo na maana, ilhali ukweli wa kudaiwa kwake uko wazi.
Nathaniel Mlaki is another mercenary.
Alianzisha chama cha SDP kikanyimwa usajili kwa kushindwa kutimiza masharti, mwaka 2005 akagombea ubunge kupitia CHADEMA.
Leo anazungumza tena kama SDP. Nalishangaa gazeti la Habari Corruption ya fisadi Rostam Aziz kwa kumtumia malaya wa uandishi Balille wanaweza kumnukuu huyu.
Gazeti la Mtanzania limekiuka sheria ya vyama vya siasa ambayo inatamka bayana kwamba chama chenye usajili wa muda, hakiruhusiwi kutoa matamko yoyote zaidi ya yale ya kutafuta wanachama wa kukiunga mkono kipate usajili wa kudumu.
Mbaya zaidi ni kuwa SDP hata usajili wa muda hakina; hakuna Tanzania kabisa chama kama hicho hivi sasa iwe chenye usajili wa muda au wa kudumu.
Hii inaonyesha wazi mkakati wa Rostam wa kuokota watu barabarani na kusema kasemeni hiki.
Huyu Nathaniel Mlaki ana hasira binafsi na CHADEMA. Mwaka 2005 alichukua fomu za ubunge akidhani kwamba atapewa mapesa ayatafune. Akanyimwa kwa kuwa alikuwa mgombea feki. Matokeo yake ni kuwa akapata kura chini ya elfu moja(1000). Lakini bado akaandika madai CHADEMA alipwe zaidi ya milioni 30 kwa kupata kura hizo. CHADEMA wakamnyima akaamue kwenda kwenye vyombo vya habari kulalamika kwa kunyimwa fedha kiasi hicho kutokana na ruzuku kwa kuchangia fedha hizo. Wakati kuna wagombea wamepata zaidi ya kura elfu 40 pamoja na kushindwa lakini hawapewi chochote, na wala fedha za ruzuku ya chama sio za kifuta jasho!
Akatoweka kwa muda, akaibuka tena kwenye sakata la mahakama ya kadhi akijiita mwenyekiti wa kamati ya kutetea wakristu. Wakati huo alipewa hongo na kambi ya nje ya mtandao iliyokuwa inataka kichwa cha Ditopile akaanza kuingilia kesi ya Ditto. Lakini pia akapewa mshiko mwingine na kundi lingine apinge mahakama ya kadhi kwa staili ya kummaliza nayo Kikwete.
Waandishi nao bado wanashika kalamu na kumsikiliza. Kwa mwandishi yoyote aliyewahi kukaa karibu na huyu jamaa anajulikana kabisa kuwa una cheti ya matatizo ya akili.
Wengine wameshaanza kumpuuza tayari siku nyingi siku hizi akisema habari haziandikwi- ni Rostam na Ballile na Habari Corruption tu ndio wenye kuweza kutumia mercenaries kama hawa.
Cha kujiuliza, kwanini huyu hajawahi kuzungumzia wadeni wa EPA amekurupuka leo katika deni la milioni 15 la Mbowe ambaye ameshalipa milioni 65, NSSF haijui inamdai bado bei gani na ni yeye mwenyewe kwa hisani yake ndiye ametangaza kwamba anadaiwa milioni 43? Je angesema milioni 65 alizolipa zimeshatosha NSSF wangesemaje? Maana wamesema wenyewe kuwa hawajui anadaiwa bei gani?
Mnajua yaliyomkuta Ballile wiki hii?
Mod Chinga aonywe kwa kujaribu kunisema mimi ndiye Kitila. Kwanza anavunja kanuni kwa kujaribu kutoa ID za watu. Pili, ananizalilisha kijinsia kwa kuniita mwanamke
Asha