Kadari Singo aliyeteuliwa na Rais Samia ni Raia wa Marekani?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Katika uteuzi wa Tarehe 21/04/2021 Mhe. Rais amemteua Kadari Singo ambaye anadaiwa kuwa Raia wa Marekani.

Je, huyu bwana ameteuliwa kimakosa au huko Marekani yupo special mission?

Kama siyo special mission kateuliwa kwa sheria gani inayoruhusu wageni kusimamia taasisi za umma? Jalada au jina lake limefikaje kwa Mhe Rais? Au katibu Mkuu kiongozi amempendekeza huyu bwana bila kujua utaifa wake?
 

Tumeambiwa tufunguke bila uoga awamu hii ya sita ya uongozi wa serikali chini ya CCM, basi weka nyama zaidi ktk uzi huu. Singo ameteuliwa kuwa kiongozi wa idara gani ya serikali, Taasisi ya Kimataifa n.k

Na vigezo gani taasisi hiyo ya kimataifa au idara hiyo ya serikali inahitaji mtu calibre ya 'Singo' ili kukidhi umataifa au utumishi wa serikali nk

Mfano uteuzi huu uliofanywa na hayati John Magufuli mwaka 2018
 
24 April 2014
Dodoma, Tanzania

Mwaka 2014 bunge maalum la katiba, mwana diaspora Kadari Lincoln Singo

24 Apr 2014
Mwakilishi wa diaspora Kadari Lincoln Singo, katika Bunge maalumu la katiba akiwa anaelezea umuhimu wa kuwatambua watanzania wanaishi nchi zingine katika kikao cha bunge maalumu la katiba cha siku ya Alhamisi tarehe 24 april 2014 huko Dodoma.
 
Ameteuliwa kuwa nani? Msaidizi wa Rais? Kama ameteuliwa kuwa msaididi wa Rais mambo ya DIASPORA ni uteuzi nzuri kwa nchi. Hawa Ndugu zetu wanaoishi nje wamesaidia sana uchumi wa nchi kwa kuongezeka kwa REMMTTANCES zao kuja nyumbani na hivyo kuziba pengo kubwa kwenye reserves zetu!
 
 
Nikuulize mkuu, Ngapi?

Mbona Tanzania huwa hatuamnbiwi mchango wa hawa jamaa kila mwaka unaingiza kiasi gani?

Hapo jirani yetu kaskazini, kila mwaka inajulikana mchango wa wananchi wao, 2020 ikafika hadidola za kimarekani bilioni 3 na zaidi!

Hapa kwetu kuna siri gani na hizi takwimu? Mbona kila kitu hapa ni lazima uhangaike kutafutiza?
 
Mama yenu kasema atakuwa akiweka "wataalamu" ili wafanye marekebisho. Kumbuka pia hutuba zake zinaonesha kuwa nchi yetu haina wataalam. Pia hao wataalam wanapokuja, serikali yake itawaharakishia vibali vya kazi!

Nchi imepatwa tena kwa mara nyingine.
 
Bado kuzaliwa US hakumnyimi mtu uraia wa Tanzania. Watoto wangu wawili wamezaliwa Europe na ni raia halali wa Tanzania hata sasa.
Ukizaliwa Marekani ina maana kuwa wewe ni raia wa Mmarekani, kwa kuwa sheria ya urais wa Marekani ina jus-soli na Jus Sanguinis. Yaani urai halali wa Marekani unapatikana kwa kuzaliwa kwenye ardhi ya Marekani, na kuwa kuzaliwa na damu ya mmarekani. Ulaya inafuata sheria tofauti, kuzaliwa Ulaya hakukufanyi uwe m-ulaya automatically.

Lakini hoja hapa ni kuwa kama kuna mtanzania (au mtu mwenye damu ya Tanzania) mwenye nia na uwezo wa kuchangia maendeleo ya nchi kuna ubaya gani akishiriki? Au ndio dhambi ya kuwabagua watanzania waliozaliwa nje ya Tanzania, kwa kisingizio cha sheria?
 
Tanzania damudamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…