Sikubaliani nawe juu ya "Diaspora hakuna kitu wanaingizia Taifa".
Inaweza kuwa ni kidogo, lakini ukweli ni kwamba hawa watu wana ndugu zao hapa nyumbani. Hawawezi kamwe wasiwe wanawatumia hata hicho kidogo kusaidia hao ndugu zao, hata kama hawawekezi kwenye miradi, kama ya ujenzi wa makazi, au kuanzisha vimiradi vidogo vidogo, hata kama ni vya aina ya mama lishe.
Hicho kiasi cha pesa ndicho kingeonyeshwa na Wakala wa Takwimu au Benki Kuu, kama wanavyofanya hao jirani uliowataja.
Tatizo letu hapa ni huko kutokuwa na uwezo wa kukusanya takwimu kama hizo, na kama zipo, kwa nini zinafichwa kama ni siri?
Huu ni uzembe.
Na mkuu, 'Course Coordinator', jibu lako hapo linaakisa kabisa tabia mbaya tuliyonayo waTanzania; ya kujifanya wajuaji na kumbe hatujui kitu.
Unajitokeza tu na jibu la kipuuzi kabisa kama hilo, linasaidia kitu gani?