Kadari Singo aliyeteuliwa na Rais Samia ni Raia wa Marekani?

Kuna wahindi, waarabu na wasomali wangapi wapo utumishi wa umma? eg Karia, Nchambi, Zungu na wengine kibao
 
Wewe Bashiru utazidi kuumia.

Kama humtambui kuwa huyu ni Rais wa JMT basi kaa kwa kutulia utuachie sisi Watanzania atuletee maendeleo.

Kosa la mama ni kukuondolea ulaji baada ya yeye kujiridhisha kwamba mlikuwa mnamdanganya hayati??
Bashe ni Waziri lakini ni msomali na hakuna anaye lalamika
 

Kuna watu wanaamini mtu akikaa sana nje basi lazima ni raia..wa huko.

US unaweza hata kuishi kwa miaka 50 ukiwa na Greencard ambayo kila miaka 10 una renew.

Hii imekaa kima jungu jungu sana...
 
Kuna watu wanaamini mtu akikaa sana nje basi lazima ni raia..wa huko.

US unaweza hata kuishi kwa miaka 50 ukiwa na Greencard ambayo kila miaka 10 una renew.

Hii imekaa kima jungu jungu sana...
Mleta thread hana hoja. Kuzaliwa au kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu hakukufanyi Usiwe Mtanzania au kukuondolea haki yako ya Utanzania.

Kuna watanzania wengi tu wamezaliwa nje na wanakulia huko lakini hiyo haiwanyimi haki yao ya uraia kwa kuwa wazazi wao ni watanzania hata kama hawazungumzi kiswahili. Of course waliozaliwa nje wanaweza wakawa advantage zaidi na choice ya kuwa watanzania au kuchukua uraia wa nchi nyingine lakini hiyo isiwe sababu ya kuwatenga pale wanspoamua kuchukua uraia wa Tanzania.
 
Diaspora hakuna kitu wanaingizia Taifa.
Zaidi Rais akitembelea nchi flani huwaalika kula chakula cha jioni na Mh.Rais au waziri aliyetembelea pale.
Bado kama Nchi hatujawatambua hadi turuhusu uraia pacha.Kenya katika hili wametupiga gape sana.
 
Hii kweli kabisa na pia hata hapa kwetu kuna tatizo hili. Utakuta mtu babu na bibi yake ni waliingia kama wakimbizi, lakini wakiambiwa kuwa wao sio raia ni wakazi tu wanahamaki. Kuna umuhimu wa kuwaambia watu kuzaliwa Tanzania na kuishi Tanzania kwa muda mrefu hakuna maana wewe ni mtanzania kama wzazi wako si watanzania.

We also need to help our government to educate our fellow citizens who are not nationals, inafika wakati wengine wanaanza hata kung'ang'ania madaraka.
 
Diaspora hakuna kitu wanaingizia Taifa.
Zaidi Rais akitembelea nchi flani huwaalika kula chakula cha jioni na Mh.Rais au waziri aliyetembelea pale.
Bado kama Nchi hatujawatambua hadi turuhusu uraia pacha.Kenya katika hili wametupiga gape sana.
Sikubaliani nawe juu ya "Diaspora hakuna kitu wanaingizia Taifa".

Inaweza kuwa ni kidogo, lakini ukweli ni kwamba hawa watu wana ndugu zao hapa nyumbani. Hawawezi kamwe wasiwe wanawatumia hata hicho kidogo kusaidia hao ndugu zao, hata kama hawawekezi kwenye miradi, kama ya ujenzi wa makazi, au kuanzisha vimiradi vidogo vidogo, hata kama ni vya aina ya mama lishe.

Hicho kiasi cha pesa ndicho kingeonyeshwa na Wakala wa Takwimu au Benki Kuu, kama wanavyofanya hao jirani uliowataja.

Tatizo letu hapa ni huko kutokuwa na uwezo wa kukusanya takwimu kama hizo, na kama zipo, kwa nini zinafichwa kama ni siri?

Huu ni uzembe.

Na mkuu, 'Course Coordinator', jibu lako hapo linaakisa kabisa tabia mbaya tuliyonayo waTanzania; ya kujifanya wajuaji na kumbe hatujui kitu.
Unajitokeza tu na jibu la kipuuzi kabisa kama hilo, linasaidia kitu gani?
 
Kalamu 1:
Tunaposema diaspora hakuna mapato wanayoingizia kama Taifa nimemaanisha ila kama unataka tuseme misaada hapo sawa.
Lakin tunapopima pato la Taifa yaani GNP na GDP tunamaanisha ,sasa ndugu zetu huko walipo hawaja invest chochote na hata kama wame-invest sisi hatufaidiki na nacho hata kidgo,kodi hatupati zaidi ya wao kutuma zawadi nyumban, sasa wakiwekeza nyumbani ile kodi tunasema na GDP bado.
 
Kuna watu wanaamini mtu akikaa sana nje basi lazima ni raia..wa huko.

US unaweza hata kuishi kwa miaka 50 ukiwa na Greencard ambayo kila miaka 10 una renew.

Hii imekaa kima jungu jungu sana...
Hata yeye anaweza pata green card tena humuhumu mtandaoni
 
Tumekuwa tukisema uraia pacha hauna madhara ila unafaida kedekede
 
Nadhani kuna mkanganyiko hapa usiokuwa wa lazima mkuu wangu 'Coordinator'.
Msaada wowote unaoletwa kwa ndugu hapa nyumbani, iwe ni dola 10 au 20, na hao diaspora wetu, hiyo ni fedha ya kigeni inayoingizwa nchini, na inahesabika na Benki Kuu kama pato la taifa.

Ni rahisi tu, Benki Kuu au hata waweka takwimu waeleze, ni pesa kiasi gani kinachoingia Tanzania toka kwa hao jamaa, kwa mwezi au kwa mwaka.
Hii kazi ndogo itakuwaje ikawa ngumu?
 
Takwimu za remittances ziko BOT nadhani ni hulka yetu kupenda kuchangia hoja bila kufanya tafiti. Haiwezekani kuwa BOT hawaweki takwimu za mirahaba ya Western Union, Moneygram and the like.
Diaspora wanamchango wao katika katika uchumi, jamii kwa kiwango chake given the political circumstances za hapa nyumbani. Contribution ya Diaspora Kenya ni lazima iwe kubwa kwasababu nchi yao imewakubali na kuwa integrate kwenye uchumi.
 
Fafanua mkuu,kwa nini unasema kuzaliwa us hakukuondolei uraia wa tanzania?
Sawa. Ili uwe Mtanzania, sifa mojawapo ni kuwa mmoja kati ya wazazi wako kuwa Mtanzania, popote alipo. Kwa hiyo, kama mmoja wa wazazi wa huyo anayezungumziwa hapa ni Mtanzania, basi yeye anayo hiyo haki ya Utanzania. Ni hicho ndiyo nilichotolea mfano kwa watoto wangu pia.
 
Nadhani ulipokwenda ni mbali zaidi. Issue ya kugombea Uraisi nadhani hata huku kwetu inaweza kuwa ngumu kwa Mtanzania aliyezaliwa nje. Ila ukiwa na mzazi Mtanzania popote duniani una haki ya Utanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…