Kadari Singo aliyeteuliwa na Rais Samia ni Raia wa Marekani?

Mkuu, ninakubaliana nawe kwamba "Takwimu za Remittance BOT...", lakini sio kila raia anayo access na BOT.

Kwani maana ya kuwa na takwimu ni nini, kuziweka tu kwenye mafaili au huko kwenye database?

Labda tupanue zaidi lawama ziwafikie pia waandishi wetu wa habari wasiotafuta habari hizi na kuwapelekea walaji huko waliko!

Hii tabia ya kuweka tu taarifa muhimu limekuwa ni tatizo la muda mrefu, na linawanyima watu fursa ya kunufaika na taarifa za aina hii.

Bila kuandika mengi na kukuchosha, ngoja nikupe mfano mmoja tu: tenda nyingi zinazotolewa na serikali, na pengine kuchapishwa kwenye baadhi ya magazeti, ni nani hasa hufaidika na tenda hizo? Huu mfano unaweza usikufanye uone mantiki ya ninayokazia hapa kuhusu umuhimu wa kueneza taarifa kama hizo walizonazo BOT.
Kenya wao ni tofauti sana, wanatumia magazeti kusambaza taarifa ili watu wazione.
 
Kama kakulia Marekani ni jambo jema, Muhimu ni kujenga nchi tu, Hata angeteua Beberu ndio ingekua vizuri Zaidi. Makuzi ya TZ yanaathiri mno akili zaetu ndio mana tunakua watu wa ovyo sana
 
Kama kakulia Marekani ni jambo jema, Muhimu ni kujenga nchi tu, Hata angeteua Beberu ndio ingekua vizuri Zaidi. Makuzi ya TZ yanaathiri mno akili zaetu ndio mana tunakua watu wa ovyo sana
Kwa lafudhi yake huyo hajakulia huko
Alafu sheria ya bongo ya uraia pacha bado
Haijakubaliwa!

Ova
 

Mkuu umefanya utafiti au copy and paste. JF imekuwa na watu wa ajabu sana. Mtu anaanzisha uzi hana data. Na watu wanacomment wakosimamia hoja ya Mtoa mada ambayo haijitoshelezi, najiuliza Hivi reasoning capacity yetu tumeuza wapi. Kijana andika kitu kieleweke na data zake sio umbeya wakati unataja na kudhalilisha mteuliwa na mteua.
 
Tanzania haina uraia pacha

Bwana Singo si mzaliwa wa Marekani ni mbongo mzaliwa wa kanda ya ziwa Mkoa wa Mara kama atakuwa ajadanganya CV yake

Alikuwa anaishi Marekani akaukataa utanzania na kwa wale wanaokumbuka bunge la Katiba wakati linaanza alikuwa anashiriki mikutano ya Membe akiwa Waziri wa mambo ya nje, ukicheki mikutano ya viongozi waandamizi waliotembelea ulaya yumo pia

Wakati akiwa tayari na Uhakika wa Uraia wa Marekani alipigana sana kwa kulipwa gharama zake na Diaspora ili Tanzania ikubali hoja wa Uraia pacha iingizwe kwenye Katiba. Ila alikwama kwa sababu si mtaalumu wa Mambo haya na hajui kujenga hoja, ila pia hana uwezo mkubwa kiivyo kiakili. Nenda yutube fuatilia michango yake utamsikia nakuelewa ni mtu wa aina gani.

Taarifa zake zilizagaa sana Mara tu Rais alipomteua na walioanza kushangaa ni wanadiaspora wenzake wakaanza kumjadili mitandaoni. Ndiyo maana hata sisi wengine tukavutiwa kugoogle taarifa zake, na zipo mtandaoni si taarifa zakusikia kwa watu

Naamini hata walioteua may be hawakujua kwamba alishapata uraia wa Marekani, ila wakiuliza America wataambiwa ni raia wao. Lakini inawezekana anapokuja bongo anadanganya uraia wake kitu ambacho nikinyume kabisa na sheria na maadili ya kiongozi mwadilifu anayeweza kuaminiwa na Rais.

Kwa vyombo tulivyonavyo na kwakuwa mama kasema tushauri kwa star ndo maana ukaanzishwa uzi huu kuvishtua vyombo vinavyofuatilia haya mambo kuchunguzwa na kisha kuchukua hatua ya kumshauri ipasavyo Mhe. Rais. Lakini pia Mhe. Rais kupitia hoja Kama hizi anajifunza na kuona sehemu zilizopwaya ili aweze kutengeneza safu strong. Si busara taarifa zilizopo Google vyombo vishindwe kuzipata.

Dunia hii inahitaji mitandao kuliko kitu kingine, mitandao inasadia taifa kujukinga na maadui kwasababu raia mwema mwenye fake ID anaweza kuingia mtandaoni nakueleza Jambo la sirini aliloliona kisha watu wakalifahamu nakuchukua hatua stahiki. This is romours but it needs investigation and interrogation before giving Singo chance to step to public office.
 
Hawezi akawa amedanganya. Ila uraia pacha ni jambo ambalo wanatakiwa waliangalie. Pia kama ni yeye alikuwa anapambania diaspora, basi kuna hatua nzuri zimefikiwa. Mfano kibali cha kazi kwa diaspora ni bei ndogo kuliko mzawa wa nje. Ila bado hatua zaidi zinahitajika ili kuwapatia diasapora wepesi zaidi walete utajiri nyumbani kama ilivyo kwa wakenya.
 
Hebu kwanza.

Jaribu kutafakari uliyoandika wewe mwenyewe hapa na kulaumu wengine.

Huu mchango wako una tofauti gani na unaowalaumu? "Data ziko wapi"?

Kama mteuliwa sio raia wa Marekani, na wewe unajua kwamba sio kweli, si eleza tu hapa badala ya wewe kujionyesha mjuaji na kulaumu wengine!

Kwa hiyo, wewe huna tofauti yoyote na huyo mleta mada. Huna data, lakini bado unaona ni bora kwako kujadili mada!
 
Duh
 
Nadhani hapa kuna mkanganyiko katika tafsiri nzima ya Diaspora. Ifahamike kuwa Diaspora ina cover watanzania wote wanaoishi nje ya nchi ( wanaishi kwa status za resident permits, wanaoishi ktk nchi za kigeni illegally na walioukana utanzania). Hivyo Mr. Si kuwakilisha Diaspora katika bunge la katiba haimaanishi moja kwa moja kuwa si raia wa Tanzania unless kuna factual information ku prove that fact. Shida kubwa tuliyonayo watanzania tumekuwa jamii inayoshadadia udaku ( maneno yasiokuwa na facts).
 
Ukitaja jina SINGO hilo linatokea upareni kati ya Mwanga na Same, labda kama ulilowea na kuchukua uraia wa Marekani kwa kazi maalum na kwa muda maalum.

GT dig deeper to unearth the concealed cell
 
Hivi unajua unachokisema kweli. Remittance gani wanafanya na zinaonekana katika financial statement ipi. Tusaidie sisi mambumbu kwenye masuala ya uchumi.

Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
 
Hapa kunahitajika mjadala mpana ,aisee!
 
Kuhusu umuhimu wa Diaspora, nadhani watanzania wengi hawana ufahamu wa kutosha. Nchi nyingi sana duniani zilizotambua na kutumia vizuri fursa ya kuwa na Diaspora zimeweza kupiga hatua katika maendelo haswa in terms of trasnfer of skills and technology. Serikali inabidi kuchukua hatua ya ku encourage Watanzania walioko nje kuwekeza zaidi nchini.
 
Diaspora hakuna kitu wanaingizia Taifa.
Zaidi Rais akitembelea nchi flani huwaalika kula chakula cha jioni na Mh.Rais au waziri aliyetembelea pale.
Bado kama Nchi hatujawatambua hadi turuhusu uraia pacha.Kenya katika hili wametupiga gape sana.
JK alifanya kazi kubwa sana kuwatambua, shawishi wengine kurudi, kuwekeza na nk..
Ni yeye mpk alianzisha dawati la diaspora pale Foreign Ministry.
Akaja mshamba mmoja akavuruga kila kitu kwa visingizio vya beberu...
Zanzibar dogo ashaanza, na I am sure na huku Mama ataanza pia.
Wenzetu wachache walio na nafasi nzuri ktk sector kadhaa wanataka sana kuleta channels na hata resources bongo lkn jitu linakataa...
Nina uhakika kwa sasa na awamu hii, na credibility ya foreign Minister tutafika mbali sana...
 
Majirani zetu waliliona hilo siku nyingi sana, ukipatiwa takwimu za kiasi kinachopelekwa nchini mwao kwa mwaka huwezi amini. Na inasaidia ajira kwa vijana. Hii dunia ya sasa haitaki siasa za kiburi, tunahitaji siasa za utafiti zenye malengo maalum.
 

Uko sahihi mkuu, tumezidi chuki! Tunachukia mtu kwa wasiwasi kabla hajafanya hata kosa. Kama tuna sheria, taratibu nzuri - hata asiyekuwa raia anaweza kufanya kazi na asiweze kutudhuru kwa lolote. WaTanzania wengi bado wana chuki na asiyekuwa mTanzania. Ni chuki hii inatufanya nasi tuone tunaonewa wivu, tunaibiwa, wanatamani amani yetu nk.

Lakini ni watanzania hawa hawa wanapenda vya wageni kama misaada ya maendeleo, wanaipenda dola na pauni kuliko shilingi, matibabu ya kigeni, vacation ugenini, masomo ng’ambo nk. Hivi mnapoenda huko, hamkuti watu wageni katika nchi hizo na kujifunza??? Hii ni mada nyingine kabisa lakini iko mulemule - dunia ya sasa imevuka mipaka ya nchi. Sisi sote tujione ni raia wa dunia hii inayoshirikiana badala ya kutengana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…