Kadari Singo aliyeteuliwa na Rais Samia ni Raia wa Marekani?

Tunahitaji damu ya watanzania tujenge nchi yetu
 
Tunahitaji damu ya watanzania tujenge nchi yetu
Mkubwa hii ni tata kidogo. Hapa Tanzania kuna watu wengi wasio watanzania na hawana damu ya mtanzania na wanaijenga Tanzania. Lakini pia kuna watu wenye damu ya watanzania
 
Mkubwa hii ni tata kidogo. Hapa Tanzania kuna watu wengi wasio watanzania na hawana damu ya mtanzania na wanaijenga Tanzania. Lakini pia kuna watu wenye damu ya watanzania
Wakati umefika waruhusu tu uraia pacha tu
Maana wabongo wengi wana uraia za nchi
Za nje ila wakija bongo wanafanya kinyemela

Ova
 
Mchango wa Diaspora utaonekana baada ya kundi hili kurasimishwa.
Kama ambavyo imekuwa kwenye Madini.
Mchango wa Wachimbaji wadogo kwenye pato la Taifa umeongezeka sana baada ya kundi hilo kutambuliwa na Serikali na kujengewa Masoko ya Madini.
Kabla ya hapo, Uchimbaji mdogo ilikuwa shughuli ya magendo, isiyolipa kodi.
Turasimishe Diaspora.
Tuache kujirudisha nyuma na kujenga hisia za kuwabagua ndugu zetu waliopo nje ya Tanzania
 
Watu wake wa karibu wamethibitisha amepata taarifa za utenguzi wa nafasi hiyo baada yakuthitisha yeye kwa Sasa ni raia wa Marekani.

Serikali sikivu usikiliza wananchi na ndio maana zamani enzi za mwalimu tuliambiwa serikali ipo kila mahali, maana yake serikili si viongozi Bali ni kila mwananchi .
 
Haya mawazo mgando tu, wapo watz wengi nje ambao wa mitaji na wangeweza kuchangia maendeleo ya nchi yao, kama tukirekebisha mawazo mgando ya kutoruhusu uraia pacha... jirani zetu Kenya, Diaspora wanaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa kutokana na sera rafiki za nchi hivyo mtu anajua akiwekeza nyumbani, anajua atasaidia ajira kwa nchi yake na pesa yake itakuwa salama...haya mambo ya siasa mgando zimepitwa na wakati... mambo ya eti kuwa na uraia pacha sijui itahatarisha usalama wa nchi ni propaganda laini tu, kwani vyombo vya usalama vya nchi, kazi yake itakuwa ni nini kama vitashindwa kuwadhibiti wale watakaojaribu kuhatarisha usalama!... Dunia yaenda kasi, na tumechelewa au nadanganya jamani....
 
Kweri kweri kabisa hujakosea mzee baba
Waruhusu tu uraia pacha

Ova
 
Nchi hawezi kuona positive contributions za Diaspora kama haijawakubali na kuwawekea mazingira wezeshi ya kuchangia katika uchumi. " unawezaje kukamua ngombe maziwa ihali humlishi" huwezi ku - expect the best out of nothing!
 
Remittances za diaspora ni double edged. Rwanda ina remittances nyingi kwa sababu Watusi wengi walikimbia nchi yao kukwepa mauaji ya kimbari mwaka 1994. Susi hatuna mauaji. Diaspora wengi Kenya ni Majaluo wengi walikimbia utawala wa Rais Moi, remittances zao ni nyingi. Sisi hatuna.

Baada ya mapinduzi matukufu Zanzibar 1964, Waarabu wengi walienda Oman na Finland, Sultani aenda Uingereza. Hapo napo kuna remittances. Je, tufanye mapinduzi mengine ili tuongeze remittances? Kuna tundulissu na Gaspat Ngurumo, wakimbizi, nao wataleta remittances. Is this what we want? In short, remittances si kitu cha kushabikia sana.

On the other hand, Wachagga wengi hupekeleka remittances kwao nyongi wakati wa Christmas, hawalazimishwi ni haki yao ni raha yao. Ni kitu gani kinawazuia diaspora wetu Marekani na EU kuleta remittances? Kumbuka, remittances haziendi Ikulu wala kanisani, ni hela wanatumiwa ndugu zao kulisha wazazi wao au kujenga nyumba. Ni wajibu wai, ni ndugu zao.

Nchi yenye amani na mshikamano haina remittances. Kama zipo hazitangazwi kwa sababu hakuna sababu. Tusubiri za tundulissu.
 
Nchi hawezi kuona positive contributions za Diaspora kama haijawakubali na kuwawekea mazingira wezeshi ya kuchangia katika uchumi. " unawezaje kukamua ngombe maziwa ihali humlishi" huwezi ku - expect the best out of nothing!
 
Samahani mkuu, lakini ni hoja ya kipuuzi, na sijui kwa nini umeni'quote' mahali ambapo hayo unayoeleza hayahusiani kabisa na mada yenyewe.

Tueleze, wewe unajua diaspora wetu huingiza dola ngapi?

Hatuhitaji kujua sababu zilizowafanya wawe huko waliko.
 
Diaspora hakuna kitu wanaingizia Taifa.
Zaidi Rais akitembelea nchi flani huwaalika kula chakula cha jioni na Mh.Rais au waziri aliyetembelea pale.
Bado kama Nchi hatujawatambua hadi turuhusu uraia pacha.Kenya katika hili wametupiga gape sana.
Sio kweli vipo vitu/misaada wanayoitoa ila haitangazwi hata ule msaada wa thamani za shule ulioleta purukshani wakati wa Makonda ulitolewa na diaspora
 
Sio kweli vipo vitu/misaada wanayoitoa ila haitangazwi hata ule msaada wa thamani za shule ulioleta purukshani wakati wa Makonda ulitolewa na diaspora
Ndugu yangu tunachoongelea ni mapato yao yanahesabiwa
Yaan Kwa mfano huko waliko je wamewekeza na kama wamewekeza kipato chao tunakikata kama kodi.
Mfano wazungu walioko huku wanaingiza mapato na serikali yao inachukua kodi inahesabu GNP .
 
Bado hujaipata maana ya hii mada. Jitahidi kusoma statistics za nchi nyingine. Wala usiende mbali jaribu kutafuta habari za diaspora wa Kenya utajiridhisha zaidi. Naona umeona fedha tu, hiyo siyo picha kubwa, zaidi tunachoangalia ni Transfer of skills and technology. Hili ni jambo ambalo nchi nyingi zilitambua na zikaweza kuendelea kiteknologia.
Mfano aliyeanzisha Kampuni ya Volvo alikuwa muajiriwa wa Ford Motors kule Marekani zamani sana. Walioanzisha kampuni ya Hyundai kule Korea Kusini walikuwa wafanya kazi wa Makampuni ya magari Japan. Sasa usizungumzie kibanda cha kichagga, panua mawazo zaidi utaona kinachoongelewa Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…