'Mteremsho wa Kitabu hiki (Qur'an) umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mwenye Hekima.
'Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki (Qur'an) kwa Haki.Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye tu.
'Hakika Dini safi ni ya Mwenyezi Mungu tu, na wale wanao wafanya wenginewe kuwa ni walinzi wakisema: Sisi hatuwaabudu ila wapate kutusogeza kumkaribiu Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu atahukumu baina yao katika wanayo khitilafiana. Mwenyezi Mungu hamwongoi aliye mwongo (na) kafiri.
'Lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka kuwa na mwana basi bila shaka angeli mteua amtakaye katika alio waumba. Subhanahu, ametakasika na hayo ! (ya uzushi kuwa ana mwana !) Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda atakalo.
'Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchna juu ya usiku. Na amefanya jua na mwezi vitumike. Kila kimoja wapo kinakwenda kwa kipindi kilicho wekewa. Jueni (ili) mtanabahi ! Yeye ndiye Mwenye Nguvu, Mwenye Kusamehe!
'Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe (Hawa) katika nafsi ile ile. Kisha akakuleteeni wanyama wa mifugo jozi nane. Akakuumbeni katika matumbo ya Mama zenu, umbo baada ya umbo (hatua kwa hatua !) katika viza (mifuko) mitatu. Huyu Ndiye Mwenyezi Mungu. Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Hapana mungu (mwingine) isipokuwa Yeye. Basi nyinyi (makafiri) mnageuzwa wapi !? (nani anaye wadanganya !?)
'Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kukufuru kwa waja wake. Na mkishukuru, Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakuambieni mlokuwa mkiyafanya. Hakika Yeye (Mwenyezi Mungu) ni Mwenye kuyajua yaliyomo vifuani (mwenu).
.................................Starehe na ukafiri wako (ni) kwa muda mchache. Kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa motoni.
....................ati watakuwa sawa wale wanao jua na wasio jua !? Hakika wanao kumbuka ni wale walio na akili.
Qur'an: 39:1-9