Kadi tatu za njano alizopata Fakhi mchezaji wa Kagera sugar hizi hapa

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
KADI TATU ZA NJANO ALIZOPATA FAKHI MCHEZAJI WA KAGERA SUGAR

1. Mchezo namba 122 uliopigwa Sokoine tarehe 17 December dhidi ya Mbeya City.

2. Mchezo namba 165 uwanja wa Kaitaba mchezo dhidi ya African Lyon . Ulipigwa tarehe 18 January.

3. Mchezo namba 190 uwanja wa Kaitaba tarehe 4 March , mechi dhidi ya Majimaji.

Mechi hizi ndizo ambazo zimewafanya Simba SC kuikatia rufaa Kagera Sugar kwa kumchezesha mlinzi wao Mohamedi Fakhi katika mechi ya April 2, 2017 Kaitaba ambapo Simba alifungwa goli 2-1.

Kama madai haya yatakuwa kweli kwa ushahidi wa mechi hizo tatu , ina maana Simba watapewa alama tatu za mchezo huo waliopoteza.
 
Yaani mnataka ushindi wa mezani hahahaha inamana simba mmefikia hatua hiyo wapi mavugo wapi kichuyaaaa
 
Hata hivyo hakuna sheria ya kupokonywa pointi zaidi ya faini tu hapo kwa timu husika..
 
Kama ni kweli Simba wapewe haki yao na timu zijifunze kuweka rekodi ya kadi zinazotolewa uwanjani
 
Hata Serengeti wanatua Gabon kwa maamuzi ya mezani. Haitaki hasira kikubwa taratibu za mchezo zizingatiwe.
Ile sheria ya kuchagua mechi ya kukosa haipo tena ?

Mmesahau nyingine kiongozi wenu Hans Pope alisema Mbaraka Yusuph ni mchezaji halali wa Simba

Sent from my NokiaX2DS using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…