Kadi ya gari la Gurumo anayo Ruge

Kadi ya gari la Gurumo anayo Ruge

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Gari alilokuwa akitumia marehemu Maalimu Mhidini Gurumo huku pia gazeti hili likibaini kuwa kadi ya gari hilo ipo kwa Ruge Mutahaba.

Diamond Platinum akimkabidhi ufunguo ya gari aina ya Toyota Fun Cargo marehemu Gurumo.nRuge ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa kampuni ya Clouds Media Group ya jijini Dar esSalaam. Mbali na kujulikana kuwa kadi hiyo ipo mikononimwa Ruge, gazeti hili lilichimba na kugunduammiliki halali wa gari hilo aliyeteuliwa namarehemu Gurumo kabla mauti kumkuta.

Sikia chanzo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, chanzo chetu kilisema: "Mgogoro uliopo kati ya watotowa marehemu ni kazi bure tu. Lile gari ameachiwa mke wa marehemu, huo ndiyo ukweli wa mambo."Akaongeza: "Ndiyo maana hata marehemu alimwagiza Diamond (Nasibu Abdul) ampatie Ruge kadi ya gari ili abadilishe jina liwe namkewe. Watoto wanazozana bure tu.

Diamond naye ni, kweli kabisa, mzee (marehemu Gurumo) aliniagiza nimpe kadi Ruge ili ashughulikie ubadilishwaji wa jina, ndivyo nilivyofanya. Mpakasasa bado Ruge anaendelea kushughulikia. Diamond hakufafanua zaidi, hata pale alipoulizwa maswali mengine, alisema atafutwe Ruge kwa maelezo kuwa anaweza kutoaufafanuzi mzuri zaidi.

Ruge sasa alipopatikana kwa njia ya simu hakuuma maneno, aliweka wazi kuwa ni kweli kadi ipo kwake na kwamba alipewa na Diamond ikiwa ni maagizo ya marehemu Gurumo ibadilishwe jina, liwe na mkewe. Ujue marehemu Gurumo kabla hajatutoka alishtukia kuwepo na mgogoro juu ya gari hilokwa wanaye hivyo akamuomba Diamond kwa kipindi hicho asimpatie kadi ya gari mpaka itakapobadilishwa na kuwa na jina la mkewe,"alisema Ruge na kuongeza:"

Baada ya marehemu kuulizwa sababu yakuchukua uamuzi huo alisema kuwa anayestahilikuwa mmiliki wa gari hilo ni mkewe kwanialiyempatia gari alikuwa na lengo la kumsaidiayeye na si watoto wake, sasa gari lingeandikwa jina lake lingeleta utata zaidi wa hayayanayoanza kujitokeza sasa.

"Mzee Gurumo enzi za uhai wake Ruge anaendelea kufafanua, marehemu alisema watoto bado wana nguvu tofauti na mkewe ambaye tayari ameshazeeka hivyo ni vyema ikitumika kumsaidia, kwa hiyo mrithi halali wa hilo gari kwa mujibu wa marehemu mwenyewe ni mkewe na si vinginevyo."
 
Hivi hao watoto wa marehemu hawana kazi?
walikuwa wanangoja mzee arudishe jezi ndo watajirike?pambafff zao....
 
John John mimi dunia imenitenga, chanzo cha mateso ni kufariki baba na mama nimekuwa mkiwa mbele yangu zanguuu..... Tunatoana roho yalabiiiiii
 
Itakuaa alitoa ruge,domo kabisaaaa

Atakuwa ruge , ndomo alikuwa kibarua tu , sasa ruge na ndomo wap na wap had ampe kadi yeye? Nilitak kushangaa maana mama ubaya tu ata vits hajamnunulia augue tu uchiz amnunulie gurumo ??
 
Atakuwa ruge , ndomo alikuwa kibarua tu , sasa ruge na ndomo wap na wap had ampe kadi yeye? Nilitak kushangaa maana mama ubaya tu ata vits hajamnunulia augue tu uchiz amnunulie gurumo ??

Mama Ubaya si alishawezeshwa HARRIER na Clemente....
 
Kubadiri ownership inachukua miezi mingi namna hii? tangu mwezi wa nane mwaka jana hadi leo ruge hajamkabidhi mkewe gulumo kadi?
 
Kubadiri ownership inachukua miezi mingi namna hii? tangu mwezi wa nane mwaka jana hadi leo ruge hajamkabidhi mkewe gulumo kadi?

Walikuwa wanatafuta kick tu kwenye media , ndomo augue tu kumnunulia gurumo gari , baba ake mwenyew hajamnunulia ningemuona chiz , watakuwa wanatuchezea mchezo mchafu tu hawana lolote
 
Walikuwa wanatafuta kick tu kwenye media , ndomo augue tu kumnunulia gurumo gari , baba ake mwenyew hajamnunulia ningemuona chiz , watakuwa wanatuchezea mchezo mchafu tu hawana lolote
kama ni kiki inamaana mzee wetu angekuwa hai si bado lingekuwa kwake?
 
Back
Top Bottom