Kadinali wa Kanisa la Roho Kazi ya Messiah asema Rais Magufuli apewe miaka 10 tena ya Uongozi

Kadinali wa Kanisa la Roho Kazi ya Messiah asema Rais Magufuli apewe miaka 10 tena ya Uongozi

waterproof

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2020
Posts
388
Reaction score
352
KANISA LA ROHO KAZI YA MESSIHA WAFUNGA MWAKA KWA MAOMBI YA KULIOMBEA TAIFA HUKU WAKITEUA UONGOZI MPYA

Na, mwandishi wetu

Kanisa la roho kazi ya messiha afrika mashariki(ukanda wa maziwa makuu) lenye makao makuu mkoani mara ikoma wilayani rorya chini ya kadinari wa kanisa hilo Joseph Ariyo nyamwanga wamemaliza mwaka kwa kufanya maombi ya siku mbili(2) yalio anza tarehe 30 desemba 2020 na kumalizika tarehe 1,januari 2021 kwenye makao makuu ya kanisa hilo yaliyoko mkoani mara wilayani rorya

Katika maombezi hayo ya kitaifa yaliyo shirikiasha waumini wa kanisa hilo na wasio waumini kuombea wagonjwa na wenye shida mbalimbali, kusumbuliwa na mapepo na magonjwa ualiyo shindikana hospitalini,hivyo watanzania wote walio fanikiwa kufika kwenye maombi hayo waliweza kubarikiwa na kuuona utukufu wa bwana

Aidha kadinali Joseph aliyo nyamwanga ametumia fulsa hiyo kutengua uongozi uliopita na kisimika uongozi mwingine na kuwaaga viongozi walio maliza muda wao.ikiwemo nafasi ya katibu mkuu wa kanisa hilo kuchukuliwa na ndugu samweli amosi atendo(sam mtetezi) baada ya aliyekua katibu wa kanisa hilo ndugu washton maebo kifariki dunia mwanzoni mwa mwezi desemba mwaka 2020.kadinari huyo pia amewaasa viongozi walio chaguliwa kufanya kazi ya mungu kikamilifu bila kupinda pinda."uongozi unatoka kwa mungu hivyo tendeni kazi kwa kumuogopa mungu kama raisi magufuli anavyo mtanguliza mungu katika uongozi wake, mimi binafsi napenda angeongoza mpaka 2030 "

Kanisa hilo la roho kazi ya messiha lilianzishwa mwaka 1997 na kusambaa hadi nchi jirani ya Kenya nakujizolea umaarufu mkubwa kwa kuwaponya wagonjwa na kuwatoa watu mapepo, hadi kufikia mwaka 2020 kumekua na jumla ya makanisa 38 yakiwa upande wa Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda

Pia kadinari wa kanisa hilo amempongeza raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kumtanguliza mungu mbele katika uongozi wake na hvyo kumtaka aendelee na kazi hyo ya kiuongozi maana uongozi ni tunu kutoka kwa mungu
"Uongozi ni tunu kutoka kwa mungu hata raisi magufuli amechaguliwa na mungu".amesema kadinali Joseph aliyo nyamhanga.

IMG-20201231-WA0016.jpg

IMG-20201231-WA0011.jpg
 
Mwehu

Anayatendaje ya kaisali na kuacha ya Mungu?
 
Sadaka imeongezeka naona new year's subili January sasa.
 
Kadinali nina?

Nibinadamu kama wewe, tofauti yake nasisi ni

1. Mwizi wa sadaka
2. Mnafiki sio mkweli
3. Tapeli tu kama walivo matapeli wengi duniani
Mfate mtu kwa anachokiongea uaufate matendo yake maana na yeye ni binadamu pia kama wewe
 
Hayo makanisa ya kutoka kenya yana shida sana.. yamejaa mno pale Tarime mjni, kuna wakati huamua kupiga ngoma na kucheza mji mzima... Na asilimia kubwa ya wafuaai wao ni wajaluo..
 
Hayo mavazi nani kawashonea? Hao viongozi wamejipa madaraka yooote kati ya waamini wao bado wanatafuta cheo cha juu zaidi maana tamaa zimewazidi wanatamani kujiita Pope lakini wanakosa sifa za kuwa Pope maana Kiongozi wa Kanisa Katoliki hajichagui kama hawa .
 
Eti Cardinali huyo ni Omelaaa kabugia kamongo huko anakuja kuzingua hapa
 
Back
Top Bottom