Kadinali wa Kanisa la Roho Kazi ya Messiah asema Rais Magufuli apewe miaka 10 tena ya Uongozi

Kadinali wa Kanisa la Roho Kazi ya Messiah asema Rais Magufuli apewe miaka 10 tena ya Uongozi

Kadinari anapotetea walio nyonga haki ili kuingia madarakani. Nit abaki kuwa Mkatoliki moyoni.
Hizi umbwa zinazojiita viongozi wa dini zinatakiwa,ziisome namba people should change tusalie nyumbani tu ili wakose sadaka zetu maana wakivimbiwa sadaka wanajikuta wanaropoka bila kushirikisha ubongo.
 
Hizi umbwa zinazojiita viongozi wa dini zinatakiwa,ziisome namba people should change tusalie nyumbani tu ili wakose sadaka zetu maana wakivimbiwa sadaka wanajikuta wanaropoka bila kushirikisha ubongo.
Kwa kweli
 
Kadinali ninani?

Nibinadamu kama wewe, tofauti yake nasisi ni

1. Mwizi wa sadaka
2. Mnafiki sio mkweli
3. Tapeli tu kama walivo matapeli wengi duniani
Duuuu! Waheshimu viongozi wa dini sheikh
 
Wakampime mkojo, inamaana ccm wote mwenye sifa ni huyo tu?
Yewezekana ni huyu huyu pekee.
Ccm iko madarakani toka 51.
Ccm wenye sifa walikuwa wapi? Mpaka jiwe kasimama?
 
Haya makanisa ya vichochoroni kwa kutafuta kiki hayajambo! Utakuta hajui hata maana ya Kadinali! Pathetic
 
Kadinari ni cheo kinachotolewa na papa kwa baadhi ya washauri wake na kuwapa haki ya kumchagua au kuchaguliwa kuwa papa ajaye, sasa hawa watani zangu wajaruo wakajua ukiitwa kadinari unakua mtu mkubwa sana kidini, wakaamua kujipachika cheo hiko...anyway hawajakosea sana kivile ila hata kuiga sio kila kitu sasa.
 
Kanisa unaniasa niache kutamani vyeo,na wewe unajihusisha na siasa
 
KANISA LA ROHO KAZI YA MESSIHA WAFUNGA MWAKA KWA MAOMBI YA KULIOMBEA TAIFA HUKU WAKITEUA UONGOZI MPYA

Na, mwandishi wetu

Kanisa la roho kazi ya messiha afrika mashariki(ukanda wa maziwa makuu) lenye makao makuu mkoani mara ikoma wilayani rorya chini ya kadinari wa kanisa hilo Joseph Ariyo nyamwanga wamemaliza mwaka kwa kufanya maombi ya siku mbili(2) yalio anza tarehe 30 desemba 2020 na kumalizika tarehe 1,januari 2021 kwenye makao makuu ya kanisa hilo yaliyoko mkoani mara wilayani rorya

Katika maombezi hayo ya kitaifa yaliyo shirikiasha waumini wa kanisa hilo na wasio waumini kuombea wagonjwa na wenye shida mbalimbali, kusumbuliwa na mapepo na magonjwa ualiyo shindikana hospitalini,hivyo watanzania wote walio fanikiwa kufika kwenye maombi hayo waliweza kubarikiwa na kuuona utukufu wa bwana

Aidha kadinali Joseph aliyo nyamwanga ametumia fulsa hiyo kutengua uongozi uliopita na kisimika uongozi mwingine na kuwaaga viongozi walio maliza muda wao.ikiwemo nafasi ya katibu mkuu wa kanisa hilo kuchukuliwa na ndugu samweli amosi atendo(sam mtetezi) baada ya aliyekua katibu wa kanisa hilo ndugu washton maebo kifariki dunia mwanzoni mwa mwezi desemba mwaka 2020.kadinari huyo pia amewaasa viongozi walio chaguliwa kufanya kazi ya mungu kikamilifu bila kupinda pinda."uongozi unatoka kwa mungu hivyo tendeni kazi kwa kumuogopa mungu kama raisi magufuli anavyo mtanguliza mungu katika uongozi wake, mimi binafsi napenda angeongoza mpaka 2030 "

Kanisa hilo la roho kazi ya messiha lilianzishwa mwaka 1997 na kusambaa hadi nchi jirani ya Kenya nakujizolea umaarufu mkubwa kwa kuwaponya wagonjwa na kuwatoa watu mapepo, hadi kufikia mwaka 2020 kumekua na jumla ya makanisa 38 yakiwa upande wa Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda

Pia kadinari wa kanisa hilo amempongeza raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kumtanguliza mungu mbele katika uongozi wake na hvyo kumtaka aendelee na kazi hyo ya kiuongozi maana uongozi ni tunu kutoka kwa mungu
"Uongozi ni tunu kutoka kwa mungu hata raisi magufuli amechaguliwa na mungu".amesema kadinali Joseph aliyo nyamhanga.

View attachment 1664701
View attachment 1664702
Hawa ndo MAKADINALI sasa, hawachanganyi dini na siasa. Wale wengine kila siku kuchanganya dini na siasa tumewachoka sasa.
 
Back
Top Bottom