mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 47,054
- 58,689
Hatoki mtu hapa. Kumbekeni mlisema Oktoba 28 mwaka jana mlimsema mngempeleka kwake Chato!???
Hawa viongozi wa dini waache upuuzi. Jpm akifanya hivyo ajue atakua amehalalisha na wengine baadae kuja fanya hivyo. Cha msingi ni waanze mtengeneza mtu kama yeye kama bado hajatengenezwa.KANISA LA ROHO KAZI YA MESSIHA WAFUNGA MWAKA KWA MAOMBI YA KULIOMBEA TAIFA HUKU WAKITEUA UONGOZI MPYA
Na, mwandishi wetu
Kanisa la roho kazi ya messiha afrika mashariki(ukanda wa maziwa makuu) lenye makao makuu mkoani mara ikoma wilayani rorya chini ya kadinari wa kanisa hilo Joseph Ariyo nyamwanga wamemaliza mwaka kwa kufanya maombi ya siku mbili(2) yalio anza tarehe 30 desemba 2020 na kumalizika tarehe 1,januari 2021 kwenye makao makuu ya kanisa hilo yaliyoko mkoani mara wilayani rorya
Katika maombezi hayo ya kitaifa yaliyo shirikiasha waumini wa kanisa hilo na wasio waumini kuombea wagonjwa na wenye shida mbalimbali, kusumbuliwa na mapepo na magonjwa ualiyo shindikana hospitalini,hivyo watanzania wote walio fanikiwa kufika kwenye maombi hayo waliweza kubarikiwa na kuuona utukufu wa bwana
Aidha kadinali Joseph aliyo nyamwanga ametumia fulsa hiyo kutengua uongozi uliopita na kisimika uongozi mwingine na kuwaaga viongozi walio maliza muda wao.ikiwemo nafasi ya katibu mkuu wa kanisa hilo kuchukuliwa na ndugu samweli amosi atendo(sam mtetezi) baada ya aliyekua katibu wa kanisa hilo ndugu washton maebo kifariki dunia mwanzoni mwa mwezi desemba mwaka 2020.kadinari huyo pia amewaasa viongozi walio chaguliwa kufanya kazi ya mungu kikamilifu bila kupinda pinda."uongozi unatoka kwa mungu hivyo tendeni kazi kwa kumuogopa mungu kama raisi magufuli anavyo mtanguliza mungu katika uongozi wake, mimi binafsi napenda angeongoza mpaka 2030 "
Kanisa hilo la roho kazi ya messiha lilianzishwa mwaka 1997 na kusambaa hadi nchi jirani ya Kenya nakujizolea umaarufu mkubwa kwa kuwaponya wagonjwa na kuwatoa watu mapepo, hadi kufikia mwaka 2020 kumekua na jumla ya makanisa 38 yakiwa upande wa Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda
Pia kadinari wa kanisa hilo amempongeza raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kumtanguliza mungu mbele katika uongozi wake na hvyo kumtaka aendelee na kazi hyo ya kiuongozi maana uongozi ni tunu kutoka kwa mungu
"Uongozi ni tunu kutoka kwa mungu hata raisi magufuli amechaguliwa na mungu".amesema kadinali Joseph aliyo nyamhanga.
View attachment 1664701
View attachment 1664702
Endelea kuwa Mkatoliki. Hawa ni Kanisa jipya kabisa limeanzishwa huko Kanda Maalum na kuvuka mipaka hadi nchi jirani.Kadinari anapotetea walio nyonga haki ili kuingia madarakani. Nit abaki kuwa Mkatoliki moyoni.
Kuna mmoja alijiita "Mungu". Alikwisha rejea watu wasikorudi.Hayo makanisa ya kutoka kenya yana shida sana.. yamejaa mno pale Tarime mjni, kuna wakati huamua kupiga ngoma na kucheza mji mzima... Na asilimia kubwa ya wafuaai wao ni wajaluo..
Ona usivyo chembe ya hekima sasa, hata kwenye sikukuu ya mwaka mpya. Ingekuwa mwezi wa saba wa nane huko sijui ungesemaje!???Asipotoka mwenyewe watamtoa.
Au tutamuita Yule Bibi wa Lindi afanye kazi yake tena
Mfate mtu kwa anachokiongea uaufate matendo yake maana na yeye ni binadamu pia kama wewe
Mungu ana sauti yake, hata kumaliza mwaka ni issue.Ndo kasema kadinari sasa
KANISA LA ROHO KAZI YA MESSIHA WAFUNGA MWAKA KWA MAOMBI YA KULIOMBEA TAIFA HUKU WAKITEUA UONGOZI MPYA
Na, mwandishi wetu
Kanisa la roho kazi ya messiha afrika mashariki(ukanda wa maziwa makuu) lenye makao makuu mkoani mara ikoma wilayani rorya chini ya kadinari wa kanisa hilo Joseph Ariyo nyamwanga wamemaliza mwaka kwa kufanya maombi ya siku mbili(2) yalio anza tarehe 30 desemba 2020 na kumalizika tarehe 1,januari 2021 kwenye makao makuu ya kanisa hilo yaliyoko mkoani mara wilayani rorya
Katika maombezi hayo ya kitaifa yaliyo shirikiasha waumini wa kanisa hilo na wasio waumini kuombea wagonjwa na wenye shida mbalimbali, kusumbuliwa na mapepo na magonjwa ualiyo shindikana hospitalini,hivyo watanzania wote walio fanikiwa kufika kwenye maombi hayo waliweza kubarikiwa na kuuona utukufu wa bwana
Aidha kadinali Joseph aliyo nyamwanga ametumia fulsa hiyo kutengua uongozi uliopita na kisimika uongozi mwingine na kuwaaga viongozi walio maliza muda wao.ikiwemo nafasi ya katibu mkuu wa kanisa hilo kuchukuliwa na ndugu samweli amosi atendo(sam mtetezi) baada ya aliyekua katibu wa kanisa hilo ndugu washton maebo kifariki dunia mwanzoni mwa mwezi desemba mwaka 2020.kadinari huyo pia amewaasa viongozi walio chaguliwa kufanya kazi ya mungu kikamilifu bila kupinda pinda."uongozi unatoka kwa mungu hivyo tendeni kazi kwa kumuogopa mungu kama raisi magufuli anavyo mtanguliza mungu katika uongozi wake, mimi binafsi napenda angeongoza mpaka 2030 "
Kanisa hilo la roho kazi ya messiha lilianzishwa mwaka 1997 na kusambaa hadi nchi jirani ya Kenya nakujizolea umaarufu mkubwa kwa kuwaponya wagonjwa na kuwatoa watu mapepo, hadi kufikia mwaka 2020 kumekua na jumla ya makanisa 38 yakiwa upande wa Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda
Pia kadinari wa kanisa hilo amempongeza raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kumtanguliza mungu mbele katika uongozi wake na hvyo kumtaka aendelee na kazi hyo ya kiuongozi maana uongozi ni tunu kutoka kwa mungu
"Uongozi ni tunu kutoka kwa mungu hata raisi magufuli amechaguliwa na mungu".amesema kadinali Joseph aliyo nyamhanga.
View attachment 1664701
View attachment 1664702
Watu tunasahau uwepo wetu hapa duniani na usitawi/maendeleo yetu kuwa ni mpangilio (plan) ya yule aliyetujaalia kuwapo hapa duniani; Mungu Mwenye-enzi. Kwa wale wanaofuatilia maandiko matakatifu, watakubaliana na mimi kuwa toka dunia ilipoumbwa, na vitu vyake na bianadamu, Mungu mwenyewe ndiye aliyewaweka viongozi wake (viongozi wake haimaanishi wa kumuongoza yeye).Sasa hapo mambo ya kuwa mkatoliki yanaingiaje wakati kadinari tajwa hapa sio mkatoliki.
watu wote humu JF wangemwelewa kadinali kama ulivyo muelewa wewe,nadhani tusinge pingana shida ya wengi humu hawaelewi alichokisema kadinali bali wao wanasoma heading tu then wanashusha coment zao bila kufikiri.Watu tunasahau uwepo wetu hapa duniani na usitawi/maendeleo yetu kuwa ni mpangilio (plan) ya yule aliyetujaalia kuwapo hapa duniani; Mungu Mwenye-enzi. Kwa wale wanaofuatilia maandiko matakatifu, watakubaliana na mimi kuwa toka dunia ilipoumbwa, na vitu vyake na bianadamu, Mungu mwenyewe ndiye aliyewaweka viongozi wake (viongozi wake haimaanishi wa kumuongoza yeye).
Viongozi wa mataifa waliitwa wafalme (bado kuna nchi zinaenzi uongozi huu), viongozi hawa, uwepo wao ( kuchaguliwa kwao), kulitokana na mapendekezo (uchaguzi) wa Mwenyezi Mungu. Angalia kuteuliwa kwa mfalme Daudi. Mataifa yote yalikuwa na wafalme walioteuliwa na Mwenyezi Mungu. Najuwa ninapoongelea haya kuna watu wanasema: hiyo ilipitwa na wakati; mimi nasema ushindwe na ulegee, Mungu hapitwi na wakati.
Baadaye, wakafuata viongozi walioteuliwa na Mungu, ili wawaongoze watu kufuata sheria za Mwenyezi Mungu na wakati huohuo kuwaongoza katika masuala ya kidunia, hawa ni kama nabii Samuel. Kwa wakati huu, hawa ndio tunawaita wanasiasa.
Watu tusirudi nyuma (retardation), tuendeleze mfumo alioweka Mwenyezi Mungu, dunia sio ya kwetu, mwenye nayo ndio anayetupangia tufanye nini na kwa wakati gani. Viongozi wetu wana mkono wa Mungu. Najuwa hapa baadhi ya watu hawatanielewa; kwa kuwa viongozi hawa tunawachagua sisi, na sio Mungu! Jibu lake ni rahisi. Sisi ni wa Mungu, Mungu anachagua kiongozi wa kuwatumikia watu wake kwa kutumia watu wake.
Kiongozi tuliyenaye, anatuongoza sio tu katika harakati za maendeleo ya kidunia ( kiuchumi), lakini pia anatuhimiza tuwe kwenye mstari mnyofu, kuwa karibu na Mwenyezi Mungu, na ndio maana kwenye kila hotuba zake anatukumbusha tumtangulize Mwenyezi Mungu katika kila jambo tufanyalo. Asante sana kiongozi wetu kwa kutukumbusha hili, tulijisahau sana! Tukiwa wazima wa afya, tunaona kuwa dunia ni ya kwetu, kumbe sisi ni wageni tu (wapita njia), mwenye nayo ndio huamua afanye nini na kwa wakati gani.
Mungu alipomleta binadamu duniani, hakumleta ili ateseke, na ndio maana binadamu wa kwanza alimuweka katika bustani nzuri. Kiongozi wetu ana maono ya kutuweka katika Tanzania iliyostawi, lakini kwa bahati mbaya sana, baadhi ya watu hawamwelewi. Hivi watanzania tumelogwa na nani? Mbona hatueleweki miongoni mwa mataaifa? Mara ooooh hatuna kiongozi shupavu, mara kiongozi huyu mpole, mara sijuwi nini.....Mlitaka Mungu atupatie nini......? Au mlitaka atupe gunia la chawa, watung'ate, jujikune na mapele yatutoke ndio akili ikae sawa. Baadhi ya mataifa wanamhitaji kiongozi wetu akawaongoze angalau kwa miezi mitatu tu, ili awafanyie aliyotufanyia sisi, sisi tunaye, halafu bahati hiyo hatuioni; ama kweli mwenye bahati habahatiki.
Hivi kweli hatuoni madege yetu huko angani, maji, umeme, kwa sisi wa Dar, hata pale Ubungo hatuoni, na je, kule Saleder? Jana nimetoka Rock City (Mwanza), daah, ujenzi wa daraja la Busisi-Kigongo......niseme tu kuwa Mwenyezi Mungu aendelee kumpa afya njema, busara, na hekima huyu kiongozi wetu (Rais wetu) ili atufikishe pale Mungu alipomuonyesha.
Kardinali amesema angependa Rais aongoze mpaka 2030, mimi nasema, kwa kuwa tunahitaji kasi hii ili tuwafikie wenzetu (Ulaya, Marekani, Asia, Australia, n.k.), basi, aongoze mpaka 2040.