Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Sio siri wafuasi na wanachama wa CHADEMA walijitutumua kuonyesha chama chao kipo hai na hili walilikomalia zaidi pale Lissu aliporejea toka Ubelgiji na kisha kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.
Lakini kadiri siku za kupiga kura zinapokaribia,wanakata tamaa,nini kimewasabu? Au kwa sababu kila hoja wanayoibua inaonekana haina mashiko? Mfano waliibua hoja kuwa uwanja wa ndege Chato ulijengwa kwa upendeleo wa rais JPM kupendelea eneo analotoka, lakini CCM waliijibu hii hoja vizuri na kueleza jinsi ilivyojenga viwanja vya ndege sehemu mbali mbali kwa manufaa ya umma.
Ikaja hoja nyingine ambayo mpaka leo imewafanya waonekane ni majuha wa kisiasa, kwamba CCM inatekeleza miradi mikubwa kama kujenga Hospital, SGR, JNHPP kuwa ni miradi ya vitu na haina manufaa kwa watu, mgombea wao akaita ni white elephant projects. Hili limewatia aibu sababu miradi yote inayotekelezwa na CCM ni kwa manufaa ya watu. Na hili lipo wazi na wala halihitaji ufafanuzi. (Hii ni mifano tu).
Sasa wana hoja gani ya kuwanyanyua siku hizi 19 zilizobaki? Maana wanaibua mambo ambayo kwenye box la kura hayana msaada,mfano Lissu kuongea kiingereza na balozi wa Usa, je Maalim Seif na Mbatia hawakuongea nae Kiingereza?
Lakini hoja kuu hapa mbona wamekata tamaa na kutepeta maana bado kama wiki mbili.