Kadogosa: Kuna njama zinafanywa Kuhujumu treni ya SGR na hazijaanza Leo na tumeshawabaini Wanaotuhujumu!

Kadogosa: Kuna njama zinafanywa Kuhujumu treni ya SGR na hazijaanza Leo na tumeshawabaini Wanaotuhujumu!

Kufuatia changamoto za hapa na pale zinazoipata TREN ya SGR boss wa TRC Masanja Kadogosa amesema Kuna njama zinafanywa Kuhujumu mradi huo

Njama hizi hazijaanza Leo ni za muda mrefu na tayari wameshawabaini miongoni mwa wanaowahujumu na watawashughulikia ipasavyo

Source Mwananchi

Mlale unono 😃
Bwana Kado tuanze na aliyepewa tender ya mabehewa ya royal😀😀😀
 
Wakati mwalimu Nyerere anang'atuka madarakani aliacha miradi mingi iloyokuwa ikiendeshwa chini ya usimamizi wa Serikali, miradi hiyo ilikufa kwasababu ya kukosekana kwa wasimamizi waadilifu .

Hili linaenda kutokea katika mradi wa treni ya mwendokasi (SGR).
Nina mashaka makubwa na mradi huo wa SGR; na hasa kama 'Chura Kiziwi' kwa miujiza ataendelea kwenye hiyo nafasi aliyopo sasa.
 
Huyo kadogosa kazi imemshinda anatafuta ppakutokea.

Kama ni kweli kasema hivyo, kwa usemi wake huo tu, kishajibainisha maji yamemzidi kimo.

Awachie ngazi awape watu wapige hiyo kazi kimya kimya na wapige pasi changamoto zote kimya kimya.

Anatenda kwa maneno badala ya vitendo? ukondoo huo.
 
Nina mashaka makubwa na mradi huo wa SGR; na hasa kama 'Chura Kiziwi' kwa miujiza ataendelea kwenye hiyo nafasi aliyopo sasa.
Baada ya kuona hakuna tija yyt ya kimaendeleo katika miradi na mashirika yaliyokuwa yakiendeshwa na Serikali, Mkapa aliamua kuyabinafsisha, huyo ni mkapa....sembuse mama Samia!

Dhamira inaweza kuwa njema tatizo wasimamizi. Magufuli alitumbua watu bandarini sio mara moja kiasi cha kufikia hatua ya kuvunjika moyo baada ya kuwa madudu na makandokando yalikuwa ni yaleyale
 
Kufuatia changamoto za hapa na pale zinazoipata TREN ya SGR boss wa TRC Masanja Kadogosa amesema Kuna njama zinafanywa Kuhujumu mradi huo

Njama hizi hazijaanza Leo ni za muda mrefu na tayari wameshawabaini miongoni mwa wanaowahujumu na watawashughulikia ipasavyo

Source Mwananchi

Mlale unono 😃
Kweli..
Kutokuwajibika kwenu
Uzembe
Kufanya kazi kwa mazoea
Kushinda maofisini badala kuwa field
Kutokusikiliza maoni na kujifanya mnajuwa
Ukosefu wa ujuzi
...........
 
Atapangiwa kazi nyingine sasa hivi,hawezi akagusa maslahi ya wakubwa akabaki salama. Amuulize Jerry Slaa😉😉
 
Ndio suluhisho. Serikali ibakie kusimamia ukusanyaji kodi, uendeshaji wafanye wawekezaji
Walifanya kwenye dhahabu matokeo yake tumeachiwa Mpango ya Tora Bora na benki Kuu kutokuwa na mapato yatokanayo na uuzaji wadhahabu
 
Ni uzembe wa vyombo vya Usalama. Wanaujua ukweli maana wana taarifa nyingi lkn wanafukia vichwa mchangani kama mbuni. Watu wa namna hii hawakusitahili kuzaliwa kimsingi wanajilaani wenyewe kwa kununulika
 
Back
Top Bottom