Kadogosa: Kuna njama zinafanywa Kuhujumu treni ya SGR na hazijaanza Leo na tumeshawabaini Wanaotuhujumu!

Kadogosa: Kuna njama zinafanywa Kuhujumu treni ya SGR na hazijaanza Leo na tumeshawabaini Wanaotuhujumu!

Uzembe na lack of competency anasingizia hujuma kama anawajua awataje hao wahujumu
 
Weka majina wazi tuwajue hao wahujumu.

Watasema jakujafungwa camera, wanasema wanainchi wasilalamike hadi mwaka uishe ndio watakuwa na majibu yote kwa kuwa bado wapo mda wa mpito.

Taarifa iliyotolewa na TRC imeeleza kuwa kilichotokea Novemba 3, mwaka huu na kusababisha kusimama kwa treni ya EMU kwa takriban saa 6 ni hujuma kutokana na kukatika ama kukatwa kwa nyaya (catenary) zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.
 
Duuh.

Hao ni wauwaji kabisa sio hata wahujumu uchumi.
 
Hapo sasa ndio huwa tunataka kuona kazi ya TISS, JW, POLISI ETC. Tulindieni vitu vyetu vizuri. Nchi inamapungufu mengi ila kwenye mambo ya maana kama SGR tuwe wakali wakuu.
Mkuu hao ulio wa mention ndio wanao tumwa na ccm kufanya vitendo vya kihuni kama kupigisha shoot
 
Kufuatia changamoto za hapa na pale zinazoipata TREN ya SGR boss wa TRC Masanja Kadogosa amesema Kuna njama zinafanywa Kuhujumu mradi huo

Njama hizi hazijaanza Leo ni za muda mrefu na tayari wameshawabaini miongoni mwa wanaowahujumu na watawashughulikia ipasavyo

Source Mwananchi

Mlale unono 😃
CDM
 
Baada ya kuona hakuna tija yyt ya kimaendeleo katika miradi na mashirika yaliyokuwa yakiendeshwa na Serikali, Mkapa aliamua kuyabinafsisha, huyo ni mkapa....sembuse mama Samia!

Dhamira inaweza kuwa njema tatizo wasimamizi. Magufuli alitumbua watu bandarini sio mara moja kiasi cha kufikia hatua ya kuvunjika moyo baada ya kuwa madudu na makandokando yalikuwa ni yaleyale
Nasikia Mkapa alikuja jutia baadae uamzi wake huo!

Ni hivi mkuu 'mbalizil', ni swala la kukosekana kiongozi mwenye dhamira ya kuyafanya hayo kwa ufanisi.
Kwa mfano, swala la kuendesha bandari kwa ufanisi lina ugumu gani kwa kiongozi aliye amua kwa dhati kabisa ifanyike hivyo.
Kila eneo sasa tunasema hatuwezi kufanya sisi wenyewe kwa ufanisi, kweli? Sisi tumekuwa binaadam wa aina gani tusioweza kufanya hata mambo madogo kwa faida yetu wenyewe? Hata vyoo vya mashimo, hadi tuombe msaada wa kuvijenga?

Taifa linapo kuwa na 'mentality' ya aina hiyo, kupata maendeleo sahau kabisa. Taifa litakuwa ni la kutegemea tu wengine toka nje.

Nirudi kwenye mfano wako wa bandari na Magufuli. Pamoja na dhamira yake ya kupata mafanikio hapo bandarini, lakini hakutumia njia sahihi ya kuparekebisha; alikuwa na papala nyingi. Huwezi kubadilisha mahali palipo kuwa na ubovu mwingi kwa muda mrefu kwa njia ya zima moto. Alitakiwa awe na subira, na aelewe ubovu upo wapi hasa, na ni njia zipi zifanyike kudhibiti ubovu huo. Huwezi kubadili hali kwa kutumbua na kuteua watu tu bila kushughulikia mfumo unao endesha ubovu huo.
 
Kufuatia changamoto za hapa na pale zinazoipata TREN ya SGR boss wa TRC Masanja Kadogosa amesema Kuna njama zinafanywa Kuhujumu mradi huo

Njama hizi hazijaanza Leo ni za muda mrefu na tayari wameshawabaini miongoni mwa wanaowahujumu na watawashughulikia ipasavyo

Source Mwananchi

Mlale unono 😃
Lini wanapandishwa kizimbani au yatakuwa yale yale ya kuvuna mabua baada ya kucheka na nyani?
 
Kufuatia changamoto za hapa na pale zinazoipata TREN ya SGR boss wa TRC Masanja Kadogosa amesema Kuna njama zinafanywa Kuhujumu mradi huo

Njama hizi hazijaanza Leo ni za muda mrefu na tayari wameshawabaini miongoni mwa wanaowahujumu na watawashughulikia ipasavyo

Source Mwananchi

Mlale unono 😃

Miradi mikakati mikubwa kama njia za gridi na kusambaza umeme kupewa wageni kuptia PPP ya David Kafulila, bwawa la Umeme JNHPP mikononi mwa Misri, SGR Reli mikononi mwa Waturuki, Wareno, waChina, Bandari DP World n.k ni hatari kwa usalama wa nchi na taifa letu.

hawafanyi bure, wanalipwa pesa na ilitangazwa tenda. sio fadhila.

Egypt omeangalia mbali hadi sasa no vinu 3 tu kati ya jumla ya vinu 9 bwawa la JNHPP Rufiji Stiegler's Gorge ndiyo vinazalisha umeme.

Je taifa hili linaloona mbali litakubali liburuzwe kwa kunyimwa maji ya ziwa Victoria, kwa kisingizio mkataba wa mwaka 1929 ni wa kikoloni ?

SGR reli mpya treni ya umeme kukwama maporini ni kwa sababu ya nyani, ngedere, bundi wanaochezea nyanya za umeme au ni michezo mikubwa zaidi ya ujasusi wa kidola? Kwa kuwa kampuni ya kidola ya jeshi la Egypt linalofanya ujenzi wa bwawa na kusimika mitano wamepata maelekezo toka Cairo Misri wafanya vurugu isiyo umiza kama vita kutuma ujumbe?

1730903219657.jpeg

1730903331697.jpeg

HABARI ZA ZIADA
Toka Maktaba:

Waziri wa Makazi akagua Maendeleo ya Mradi wa Bwawa na Kituo cha Umeme wa Maji cha Julius Nyerere, na kupewa ripoti kazi ya kina​

Jumanne - 14 Mei 2024

El-Gazzar: Misri yatilia maanani sana mradi huu mkubwa, unaojumuisha uhusiano wake pamoja na Tanzania…hufanikisha maendeleo na hutoa umeme unaohitajika kwa Tanzania

Dkt. Assem El-Gazzar, Waziri wa Makazi, Huduma na Jumuiya za Mijini, alikagua maendeleo ya shughuli za mradi wa Bwawa la Julius Nyerere na kituo cha kuzalisha umeme cha maji, unaotekelezwa na Muungano wa Kampuni za Misri wa “Arab Contractors” na “Elsewedy” kwenye Mto Rufiji huko nchini Tanzania.

Mheshimiwa waziri Dkt. Assem El-Gazzar aliambatana na Balozi Sherif Ismail, Balozi wa Misri nchini Tanzania, Meja Jenerali Mahmoud Nassar, Mkuu wa Taasisi kuu ya Maendeleo, Mhandisi Ahmed Al-Assar, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanzania.

Kampuni ya Arab Contractors, Mhandisi Hisham Hegazy, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Elsewedy Electric (PSP), Mhandisi Hossam El-Din Al-Rifi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Arab Contractors, na Mhandisi Ayman Attia, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni, Mhandisi Darem Dibsi, mratibu wa mradi, Mhandisi Mohamed Samaha, Naibu Mkurugenzi wa Muungano, na Mhandisi Mohamed Zaki, Naibu Mkurugenzi wa Muungano.

19_2024-638511906904781305-478.jpeg

Dkt. Assem El-Gazzar alisisitiza kuwa Serikali ya Misri inatilia maanani sana utekelezaji wa mradi huu mkubwa, unaohusu mahusiano ya kipekee kati ya Misri na Tanzania, na unafuatwa mara kwa mara na Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.

Na ziara hii inakuja katika muktadha wa kufuatilia maendeleo ya kazi katika ardhi, ili kufikia maendeleo kwa ndugu zetu katika Nchi ya Tanzania, kutoa nishati muhimu ya umeme kwa Jamhuri ya Tanzania, kudhibiti mafuriko ya Mto Rufiji, na kuhifadhi mazingira.

Maafisa wa Muungano wa Misri wanaotekeleza mradi huo wamesema kuwa mradi huo unajumuisha ujenzi wa bwawa lenye urefu wa mita 1025 na umekamilika na uwezo wa kuhifadhi bwawa hilo kufikia bilioni 34 na pia unajumuisha kituo cha kuzalisha umeme cha maji chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2115

Na kituo hicho kipo pembezoni mwa Mto Rufiji katika hifadhi ya asili katika eneo la “Morogoro”, kusini magharibi mwa jiji la Dar es Salaam (mji mkuu wa kibiashara) na mji mkubwa zaidi nchini Tanzania, ambapo mita za ujazo bilioni 33 zilihifadhiwa katika ziwa la bwawa na maji yalifikia kiwango cha mita 184 kutoka usawa wa bahari, ambapo kiwango cha chini cha uendeshaji wa mitambo ni 163 kutoka usawa wa bahari.

Maafisa hao wa mradi wameongeza kuwa kiwango cha ukamilishaji wa mradi kilifikia asilimia 97.74, wakati bwawa kuu likiwa limekamilika, mabwawa madogo 4 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la maji, kazi za plagi, mahandaki 3 kwa ajili ya kupitisha maji muhimu kwa jengo la mitambo, kituo cha usambazaji na umeme, na daraja la kudumu la saruji kwenye Mto Rufiji, na kiwango cha kukamilika kwa kituo cha umeme cha maji kilifikia asilimia 93.8, na barabara za kudumu kuwezesha harakati na kuunganisha sehemu za mradi, asilimia 87.43, na kiasi cha saruji kilichounganishwa na bwawa kuu kilifikia milioni 1.4, na milango kuu ya bwawa hilo iliwekwa na kuendelea Utekelezaji wa kazi za mwisho za kumaliza, na kiasi cha kujaza nyuma kilichotumika katika mabwawa madogo kilikuwa milioni 5.5 m3 pamoja na 350 elfu m3 ya saruji.

Maafisa wa mradi wa Misri wanaotekeleza mradi huo walielezea kuwa kazi ya muunganiko mkuu wa njia zinazounganisha maji na jengo la turbine inaendelea kulingana na viwango vilivyopangwa.

Kwani ujenzi wa njia kuu ndani ya mlima umekamilika na urefu wa zaidi ya mita 1500, na kazi ya kitambaa halisi kwa njia kuu 3 imekamilika, na milango yote ya plagi imewekwa na kukusanywa, na handaki linaloongoza kwa nambari za turbine / vinu nambari kuanzia (7 – 8 – 9) limejazwa baada ya kufanya kazi ya majaribio kwa mafanikio.

Na kazi inaendelea kwenye muundo kuu wa jengo la turbine, ambayo ni moja ya vitengo muhimu zaidi Mradi huo, ambapo kazi za kiraia za jengo la mkutano wa turbine (Erection Bay) zimekamilika, na korongo kubwa za 3 zimewekwa – na mzigo wa hadi tani 400 kwa kila winch – muhimu kwa ufungaji wa vitengo kuu vya mitambo, na sehemu zinazotolewa za mitambo kwa sasa zinawekwa, ambazo ni kazi zinazotekelezwa kulingana na viwango vya juu vya ubora vinavyohitajika.

Kazi hizo pamoja na mifumo ya msaidizi wa umeme, na ufungaji wa transfoma kwa transfoma 27, minara na kuunganisha mistari kati ya kituo cha ujenzi wa turbine na kituo cha kiungo kimekamilika, Ufungaji wa mitambo miwili Na. (8-9) imekamilika, na turbine Na. 7, ikiwa ni pamoja na mifumo ya msaidizi na udhibiti, inakamilishwa na kuunganishwa na jengo kuu la kudhibiti.

Walieleza kuwa kazi ya upimaji inafanyika kwa mitambo Na. (8-7), na operesheni ya mwisho ya mitambo Na. 9, kuzalisha megawati 235 na kuipandisha kwenye mtandao wa nje wa Nchi ya Tanzania, na ufungaji wa kifurushi cha mitambo unaendelea baada ya kazi halisi za ujenzi kukamilika kikamilifu, na awamu ya kwanza na ya pili ya kazi za saruji zimekamilika, ujenzi wa mitambo ya kutoka, na kukauka kwa mto na jumla ya 250 elfu m3, na kukamilika kwa kumaliza ndani,Kazi za kumalizia nje ya jengo zimekamilika, tabaka za msingi za barabara za kudumu zimekamilika, tabaka za mwisho na kazi za kutengeneza vifaa vya ujenzi zinakamilika, kituo cha usambazaji na uunganishaji chenye uwezo wa KVA 400 kimekamilika.

Na kituo cha usambazaji umeme kuunganishwa na kituo cha Chalinze kilichopo eneo la mkoa wa Pwani na kuunganishwa na mji mkuu, Dar es Salaam, na majaribio na uendeshaji vimefanyika kwa ufanisi, kwani laini ya kuunganisha imejaribiwa na umeme unaohitajika kwa operesheni ya awali na vipimo vya mitambo vimejaribiwa, na uzalishaji wa umeme kutoka kwa mitambo umeanza na kuinuliwa kwenye mtandao wa nje
1730903276062.jpeg
 
Nasikia Mkapa alikuja jutia baadae uamzi wake huo!

Ni hivi mkuu 'mbalizil', ni swala la kukosekana kiongozi mwenye dhamira ya kuyafanya hayo kwa ufanisi.
Kwa mfano, swala la kuendesha bandari kwa ufanisi lina ugumu gani kwa kiongozi aliye amua kwa dhati kabisa ifanyike hivyo.
Kila eneo sasa tunasema hatuwezi kufanya sisi wenyewe kwa ufanisi, kweli? Sisi tumekuwa binaadam wa aina gani tusioweza kufanya hata mambo madogo kwa faida yetu wenyewe? Hata vyoo vya mashimo, hadi tuombe msaada wa kuvijenga?

Taifa linapo kuwa na 'mentality' ya aina hiyo, kupata maendeleo sahau kabisa. Taifa litakuwa ni la kutegemea tu wengine toka nje.

Nirudi kwenye mfano wako wa bandari na Magufuli. Pamoja na dhamira yake ya kupata mafanikio hapo bandarini, lakini hakutumia njia sahihi ya kuparekebisha; alikuwa na papala nyingi. Huwezi kubadilisha mahali palipo kuwa na ubovu mwingi kwa muda mrefu kwa njia ya zima moto. Alitakiwa awe na subira, na aelewe ubovu upo wapi hasa, na ni njia zipi zifanyike kudhibiti ubovu huo. Huwezi kubadili hali kwa kutumbua na kuteua watu tu bila kushughulikia mfumo unao endesha ubovu huo.
Una hoja na mawazo mazuri sana kama ilivyokuwa kwa mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Jakaya, Magufuli na sasa Samia.

Hakuna raisi anayeingia Ikulu kwa lengo la kudhoofisha uchumi wa nchi. Tatizo ni misingi iliyojengwa tangu awali ambayo ukishachaguliwa unaikuta imeshakita mizizi yake. Ili urekebishe ni lazima uguse maisha ya watu wote hususani wale walio kwenye idara, sekta na vitengo mbalimbali . Sasa itategemea unagusa maisha ya hao watu katika muktadha upi (hasi au chanya).

Nafikiri ndio sababu mara kadhaa tumetolea nchi kama China huku tukisahau mifumo ya uendeshaji wa nchi kama China ni ujamaa ambao uongozi wake ni sharti utumie mabavu (dikteta) vinginevyo utafeli kama ulivyofeli kwa mwalimu Nyerere.

Kwa uhalisia sera ya nchi yetu kwa sasa ni ubepari ambao misingi yake ni walio nacho wanaongezewa wakati wasio nacho wananyang'anywa hata kile kidogo kilichopo.

Lakini watanzania wengi miongoni mwetu tu wavivu mno! na ukitaka kupata ukweli wa hili fuatilia makazini hasa Serikalini baadhi ya wafanyakazi na watumishi utendaji wao ni chini ya kiwango. Tunapoteza muda mwingi sana kupiga soga badala ya kuchapa kazi. Mbaya zaidi tu wepesi sana kuridhika, mtu akishamiliki nyumba na usafiri anajiona baasi kamaliza.

Mashirika yote aliyoyaacha mwalimu Nyerere yalikufa kwasababu ya uvivu, uzembe, ulafi, ufisadi ,tamaa ya kumiliki Mali ambayo hujaitolea jasho, wizi na kadhalika. Kurekebisha mifumo hii sio jambo jepesi japo inawezekana lakini uongozi ni lazima utumie mabavu na matokeo yake hayataoneka ndani ya muda mfupi
 
Kwa sasa nikushukuru mkuu 'mbalizil' kwa jibu/andiko lako hapa. Ninakuelewa vizuri unachosema; lakini sikubaliani na hoja zote zinazo tumika tu kutunyanyasa, kama hilo la "uvivu".

Nami naomba muda, nitakapo tulia vizuri ningependa kujibu haya uliyo andika hapa.
Uongozi wa nchi yetu tatizo lake lipo katika haya uliyo andika hapa.

Nitarudi baadae nikujibu kwa utaratibu na mpangilio wa jinsi ulivyo yaeleza maoni yako.
 
Mambo ya Ccm hayo, upo sahihi mkuu.

Kiongozi anayeonesha kuguswa kizalendo ni lazima ashughulikiwe, aidha kwa kuondolewa kwenye hiyo position wanaita 'mabadiliko madogo' ama zengwe kubwa la kutumbuliwa kabisa.
Na CCM wanaweza kumuua Kadogosa ili asitoe siri
 
Dodoma dar 120k, moro dar 50k hata kama ni business hii pia ni hujuma dhidi ya wananchi.
 
Back
Top Bottom